Mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya, amesema sio sawa kwa Mtumishi aliyeitumikia Tanzania kwa miaka mingi kumpangia matumizi ya fedha ya fedha yake kwa kumpa asilimia 25 huku asilimia 75 unasema utamlipa polepole.
Bulaya amesema Uongozi wa Hayati Dkt. Magufuli ulilazimisha kuweka mfumo mbovu na wa kinyanyasaji na hata ripoti ya Waziri Mkuu iliyosomwa jana Bungeni haisemi wazi ni kwa namna gani Serikali itatatua malalamiko ya Wafanyakazi katika Mafao yao.
Aidha, ameitaka Serikali kuacha kuchukua mikopo kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwasababu fedha hizo sio za Serikali bali wao ni watunzaji tu.