Safi sana, kudo kwake! Na hili linatokea hapa hapa Tanzania? Sasa mwingine atasema "upinzani unazuiliwa kufanya mikutano ya nje"...
Hata udikteta kuweza kunawiri kunatokana na ulegevu wa umma. Lakini watu tukiwa imara kutetea katiba yetu, kutetea uhuru wetu, kutetea haki zetu, hakika kamwe hakutakuwa na mtu yeyote wa kutuburuza, si Polisi, si TISS, si Rais wala CCM.
Tunaburuzwa kwa sababu hatujitambui, tumekubali kuburuzwa, tumekubali katiba yetu ichezewe, tumekubali kura zeru zichezewe. Kabla ya kuwalaumu watawala, CCM na Polisi, yatubidi kujiuliza tumefanya nini kuyagomea kwa njia zote zinazowezekana yale ambayo katiba na sheria zetu haziruhurusu lakini yanafanywa.
Ester Bulaya, anajitambua, ni mpigaji na mlinzi wa katiba na haki zake. Lakini pia wapiga kura wake nao wanajitambua. Huyu ni mzalendo wa kweli. Huwezi kuwa bwege, mtu wa hewala kila kitu, mtu wa kusifia viongozi na serikali hata katika uovu, halafu ukasimama mvele ya watu na kusema wewe na mzalendo.