Mzee mwenzangu
Mzee Mwanakijiji, sasa hapa unatufanya sisi wengine tushindwe kabisa kukuelewa. Tumetoka nawe mbali, tumeshuhudia mengi, tumeshauri mengi, tumekosoa mengi...lakini kwa sasa huku unakoelekea inatubidi tujiulize, kweli huyu ni mwenzetu yule yule au hapa tuna pandikizi linalotumia jina na avatar yake.
Hapa chini tunaye mbunge wa kuchaguliwa na tunaye afande, ambaye kiustaarabu na kiitifaki, anatakiwa awe na heshima kwa mwakilishi wa wananchi. Lakini badala ya kutoa ulinzi kama katiba inavyomtaka anamzuia mbunge asiongee na wananchi wake jimboni kwake eti lazima aombe na apewe kibali, kweli?
Yaani tunayo katiba ndani ya Jamhuri ya Muungano inayomtaka Mbunge apate kibali cha afande huyu ili aweze kuongea na wananchi wake waliompigia kura.
Mzee Mwanakijiji, unapopinga tena kwa kebehi kwamba hali kama hii haitokei haha hapa Tanzania, ungependa baadhi yetu tukueleweje? Please give us a break!