Pamoja na lawama zote kumwendea Rais, kwa nini tuwe na fikra za kutegemea akili ya mtu mmoja?
Cha ajabu kabisa, viongozi karibia wote ni wale wale waliokuwa na Magufuli. Tunaelekea wapi kama taifa?
Umegusa patamu sana hapo.
Kwa sababu Rais huyo huyo, ndiye 'mungu' wa hao wote ambao umewataja hapo. Uwepo wao kwenye nafasi yoyote ile ni kwa hisani ya 'mungu' huyo huyo.
Hii ni hitilafu kubwa sana iliyoingia vichwani mwa wananchi wetu.
Wewe angalia tu, humu JF, watu wanashangilia uteuzi wa mawaziri?
Kuteuliwa sasa kwa nafasi yoyote ile kumekuwa kama ni zawadi kubwa sana inayotolewa kwa wahusika?
Mimi sijui hili limeingiaingiaje vichwani mwa wananchi hawa.
EeenHeeee, umemtaja tena Magufuli na hao viongozi wake, akina Kabuti Kalamaganda, tuliokuwa tunawaona wakijivimbisha vifua kwa 'UZALENDO' wa kuigiza!
Magufuli kafa, na uzalendo wao ukayeyuka.
Inasikitisha sana kuwa na watu wa namna hii.
Lakini yote haya, naomba unielewe vizuri ninakolenga mimi.
Kama pale juu, kwenye kiti cha Rais, tungebahatisha kumpata mzalendo kwelikweli, anayejali maslahi ya nchi hii na watu wake; hawa wote wanaoigiza wangetumika hivyo hivyo na kuleta mabadiliko makubwa ndani ya nchi yetu.
Kwa hiyo, jambo muhimu sana kuliko yote, ni mtu anayekaa pale kwenye ile nafasi muhimu sana.
Tunapopata viongozi kama huyu mama, kila kitu kinasambaratika, na hao hao mawaziri wa kuigiza kila kitu wanakuwa kama vikaragosi wa huyo aliyewateua..
Hatuwezi kwenda popote kama nchi na uongozi wa namna hiyo.