GE2025 Bundi ameweka kiota CCM: Mpasuko, Visasi, Tamaa ya Madaraka na Ufisadi vinaimong'onyoa

GE2025 Bundi ameweka kiota CCM: Mpasuko, Visasi, Tamaa ya Madaraka na Ufisadi vinaimong'onyoa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Rasmi,
Haya matukio yanayojiri ndani cha CCM ni kiashirio dhahiri kuwa jambo kubwa linaenda kutokea kwa manufaa ya Nchi.

Jakaya aliwahi kusema kuwa makundi ndani ya CCM ni afya. Lakini ukweli unadhihiri kuwa makundi yaliyopo ndani ya CCM yameendelea kuwa kitanzi dhidi ya lichama hilo. Kwa mfano yapo makundi ya CCM Halisi na CCM Maslahi, kuna makundi ya Mtandao na kundi la Sukuma Gang. Na kadhalika.

Kundi la Kizimkazi limekuwa bize kulipiza kisasi dhidi ya Sukuma Gang kwa msaada wa kundi la Mtandao. Mwendo wa mgambo wanaruka na kukanyaganya unatifua vumbi la mtafutano na mtafunano.

Leo tunashuhudia uvunjwaji mkubwa wa Katiba na Sheria za Uchaguzi ambapo CCM imeteua mgombea wa Urais kinyume na Katiba ya Nchi ibara ya 38 inayoelekeza teuzi za wagombea zifanyike baada ya Bunge Kuvunjwa..... Msajili wa vyama vya siasa ambaye amekuwa akionesha uwezo wake mkubwa kuwadhibiti CHADEMA ameufyata kwa ukiukwaji mkubwa dhidi ya CCM.

Mchakato wa kura za uteuzi wa wagombea nafasi za Udiwani na Ubunge ndani ya CCM, umeacha mpasuko mkubwa sana ndani ya CCM

View attachment 3440324
Video inajieleza na kuakisi yanayoendelea maeneo mengi nchini. Inasemwa kuwa hata mwamko wa wananchi kusheherekea kifo cha Ndugai Kongwa ni wanaCCM wasioridhishwa na mchakato wa kura za maoni zilizompa ushindi Ndugai...

Tarehe 12 Agosti 2025, CCM ilifanya harambee kusaka bilion 100. Dunia imeshuhudia kufuru ya wafanyabiashara wengi ambao baadhi ni walalamikiwa kushiriki ufisadi wakiwa ndiyo vinara wa uchangiaji. Namna ambavyo CCM imekionesha kukumbatia mafisadi ambao wanakichangia, ni wazi imejitenga na raia ambao ndiyo msingi mkuu wa madaraka.

Ni dhahiri kwamba, CCM imeshapasuka vipande. Ni suala la muda kufikia tamati yake. Endapo CCM itaondoka madarakani, ndiyo mwanzo wa Tanzania bora na mwisho wa madhila makubwa dhidi ya raia wa nchi hii.

Ni muhimu sana serikali ikaachana na kesi ya Tundu Lisu ambapo kinachoendelea kinyume na Katiba na sheria za nchi. Aibu tunayoipata kama.nchi itatutafuna kwa vizazi vingi vijavyo....
Endelea kupiga ramli siku ukikua huenda ukaacha.
 
SUKUMA GANG was more meaningful than KIZIMKAZI GANG . Kizimkazi gang inajua bara sio kwao ndio maana wanakula na kufànya uaribifu
Elewa maana ya umoja wa kitaifa. Hivi vyeo na hizi nafasi zinakuja leo na kesho zinaondoka, Tanzania inaendelea kuwepo.
 
Fursa za kiuchumi zipo kibao Rais Samua amefingua nchi, ni wewe tu kuamua kuwa positive.

Ukiwa na mtazamo hasi huwezi kuziona na utaishia kufungua threads za makasiriko tu. Na hii ni hatari kwako, waweza kupata sonona au kusukari maana utulivu wa akili haupo na mapigo ya moyo yanakwenda kasi
Samia anaendelea kuifungua nchi. Uzuri wake hana siasa za uoga, yupo chanya sana linapokuja wazo lenye mtazamo wa kimaendeleo.

Wengi wa wanaolalamikia ile harambee wamejaa wasiwasi na uoga, hayo ni matunda ya kuishi kijamaa kwa muda mrefu. Tunakuwa na hulka za kutozipokea changamoto mpya na tunaendelea kukariri maisha kwa kutaka kuishi ndani ya eneo tunaloamini linatufaa siku zote (comfort zone).
 
Hapo kwenye bold....
Natafutaje hela wakati asilimia 80 haipo kwenye mzunguko? Juzi tumeona nani wamezificha hela
Mkuu unataka pesa uletewe nyumbani kwako uambiwe hizi hapa!?. Hao mabilionea wamezichangamkia fursa za kujiinua wao wenyewe, chapa kazi, punguza kutafuta watu wa kuwanyooshea vidole siku zote hutawakosa na ulofa unabakia pale pale.
 
Mkuu unataka pesa uletewe nyumbani kwako uambiwe hizi hapa!?. Hao mabilionea wamezichangamkia fursa za kujiinua wao wenyewe, chapa kazi, punguza kutafuta watu wa kuwanyooshea vidole siku zote hutawakosa na ulofa unabakia pale pale.
Mtu anaamka asubuhi saa 11 kutoka Mbagala Charambe, anarukia daladala 2 ili aende Kisutu kusikiliza kesi ya Tundu. Wenzie Mbagala wanakimbilia Kariakoo kufunga bidhaa wakauze kwenye ule umati.

Sasa bwege kama huyu Msanii alilalamika hali mbaya ni wa kumdharau tu
 
Mtu anaamka asubuhi saa 11 kutoka Mbagala Charambe, anarukia daladala 2 ili aende Kisutu kusikiliza kesi ya Tundu. Wenzie Mbagala wanakimbilia Kariakoo kufunga bidhaa wakauze kwenye ule umati.

Sasa bwege kama huyu Msanii alilalamika hali mbaya ni wa kumdharau tu
Muda huu serikali inaweka mazingira mazuri ili biashara ya gesi iwafaidishe wananchi kwanza kupitia sheria za nchi.

Haya ni masuala nyeti na yenye kugusa hatima zetu moja kwa moja, lakini mwananchi wa kawaida hawezi kujadili namna anavyokwenda kunufaika na ugunduzi wa hiyo gesi akili kaziweka kwenye kesi za kisiasa na kuendekeza mada za kijinga mitandaoni.
 
Back
Top Bottom