Katika kile kinachoelezwa hali si shwari ndani ya Club ya Simba, inaelezwa Msemaji wa timu hiyo ndugu Ezekiel Kamwaga ameamua kukaa pembeni kuendelea na majukumu yake ndani ya club hiyo.
Tukio hili linatokea Ikiwa haijapita hata wiki moja tangu kujiuzulu nafasi ya Mwenyeketi wa Bodi wa timu hiyo MO Dewji. Sababu za kamwaga kubwanga manyanga bado hazijawekwa wazi ila za ndani zinasema kuwa amechoshwa kupelekeshwa na mtendaji mkuu wa timu hiyo.
Alipoulizwa Mwenyekiti wa Simba ndugu Mangungu kuhusiana na taarifa hizi amesema watalitoea tamko hapo baadae.