Bundi kwenye Paa la Nyumba Yangu na hataki kuondoka

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
18,069
Reaction score
25,172
Leo wakati nakwenda kazini nilimwona ndege huyu kwenye sehemu ya paa langu hivi; asubuhi tulikuwa na snow kidogo.

​

Niliporudi nyumbani baada ya kazi saa 10 jioni nilimkuta bado yupo ila nilipofungilia geti, ule mlio wa geti ukamshtua akarukia juu ya paa kuu kama inayoonekana hapa huku akiacha kinyesi kingi sana kwenye sehemu aliyokuwa amekaa.

​

Jioni saa 12 nimekuta tana amerudi pale pale kama anavyoonekana hapa bila snow

​

Je huyu bundi ananiletea uchuro au amefurahia maisha kwenye mazingira ya nyumbani kwangu? Kama ameniletea uchuro unanishauri nifanye nini
 
Ndani ya week mbili kuna jirani ambaye ni mgonjwa atafariki au utaletewa habari ya msiba wa mtu wako wa karibu(ndugu ,jamaa au rafiki).
 
Wanasema et bundi anatambua seli zilizokufa kwa binadamu
Coz wanasema et kabla roho kutoka kwa binadamu seli za mwili ndio huanza kufa kwanza
Nb sina uhakika
Kama kuna mgonjwa maeneo hayo anaelekea kufa very soon.
 
Bundi ni ndege aliye na hisia za kusense na kujua mzoga ulipo. Asije kukuambia kuwa bundi ni wa bahati huyo mpge hata ngumi ya mdomo afu uondoke. Hapo jiran kama kuna mgonjwa jitayarishe mda wowote kupata taarifa za msiba au kuna kitu ambacho sio cha kawaida kitatokea kwani wachawi wa kwenu wapo kazin kukuwinda wewe. Kama unaweza ukapata chungu kilichopasusa mrushe kipisi kimoja akianza kuruka msindikize na kingne ni kama unamlenga kumpga utakuja nishukuru baadae. Na kama unaishi uzunguni sana funga bulb karibu na hapo anapokaa ila uifunike ili isinyeshewe afu ucku unaiwasha afu unazima unakaa kidogo unafanya hilo zoez la kuiwasha afu unazma hatarudi hapo. Usidharau!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…