Bundi kwenye Paa la Nyumba Yangu na hataki kuondoka

Niliacha kuamini kuwa Bundi hana uchuro baada ya kuja na kukaa nyumbani kwangu juu ya bati zaidi ya masaa 12, kiukweli nilijawa na hofu hatari lakini mwisho wa siku alijiondokea zake na hakuna aliyekufa sio sisi wala majirani.

Baada ya hapo nikajisemea kumbe huwa tunamsingizia tu ndege wa watu.

Mi nadhani mchukulie tu kama ndege wengine ili usiishi na hofu ikifika muda akajisikia kuondoka ataondoka.
 
Bundi ni ndege(just a bird) tu kama ndege wengine, kama anakukera mtafutie manati.
 
Si umfungulie tu dirisha aingie ndani, mwenzio anapigwa baridi
 
Kama ni kweii, basi maeneo ya hospitali kungekuwa na bundi wengi sana.
Sio bundi tu hata paka. Kuna kipindi huko UK kuna paka wa hospitali alikuwa anajisogeza kwenye kitanda cha mgonjwa anaekaribia kufa. Huwa wananusa dead cells wakati mtu anakaribia kufa.
 
Sio bundi tu hata paka. Kuna kipindi huko UK kuna paka wa hospitali alikuwa anajisogeza kwenye kitanda cha mgonjwa anaekaribia kufa. Huwa wananusa dead cells wakati mtu anakaribia kufa.
Sio kwamba alikuwa anavizia mabaki ya vyakula anavyoletewa mgonjwa?
 
Huyo mwamba kuna kipindi alikuja akatua kwenye mojawapo ya miti kwenye compound yetu.

Ndani tulikuwa tunamuuguza mjomba wetu na alikuwa anaumwa vibaya Sana.
Baada ya bundi kuondoka mjomba akakata Moto😔
 
Kukiwa na miti mikubwa jirani na hospitali huwa wanakuwepo Bundi
Na ndege wengine pia huwa wapo.
Bundi akiwepo mahali ni kwa sababu kuna misosi yake anayopenda, kuanzia panya, popo na nyoka na baadhi ya ndege na wadudu kadhaa. Misosi ikiisha anaondoka.
 
Je huyu bundi ananiletea uchuro au amefurahia maisha kwenye mazingira ya nyumbani kwangu? Kama ameniletea uchuro unanishauri nifanye nini
Hapana hana madhara yoyote mkuu hakuna uchuro wowote na usichojua ni kwamba atakaa hapo kwa zaidi ya miezi in short amepapenda tu kwa hio ishi nae huyo ni ndege tu km ndege wengine, ni sawa na wewe upende kwenda kupozi sehemu fulani kila wakati ndio hivyo hivyo kwa huyo bundi amepapenda tu hapo ila hakuna uchuro wowote ninakwambia kwa experience

wewe unasema mmoja? huku walikua wanakuja mpaka watatu na nilikua nawasogelea kabisa hivi na kuwapiga picha sema mmoja sio muoga kabisa hata ukimsogelea mpaka umsogelee sana na uonyeshe namna fulani km unataka kumgusa ndio anaruka hakuna chochote kilichotokea na sasa hivi hawaji sana naona wamehamia sehemu nyingine
 
Na ndege wengine pia huwa wapo.
Bundi akiwepo mahali ni kwa sababu kuna misosi yake anayopenda, kuanzia panya, popo na nyoka na baadhi ya ndege na wadudu kadhaa. Misosi ikiisha anaondoka.
Ni sahihi
 
Ni kweli hadi leo bado yupo; siku ya tatu sasa.
 
Duh hii ni adhabu.
Sasa kuna uhusiano gani kati ya bundi na kuwasha/kuzima taa?
 
Ni kweli hadi leo bado yupo; siku ya tatu sasa.
Usihofu mkuu.
Ni ndege tu ambaye yupo kwenye mishe zake, wala hajui kama unamuwazia mabaya. Ana-chill tu kuvizia windo lake la usiku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…