Hili lina ukweli lakini siyo kama watu wanavyohadithia. Ukweli uko hivi: Zamani sana mababu zetu walikuwa hawana hospital. Hivyo watu wengi walikuwa wanaugua na kufariki wakiwa nyumbani. Hebu fikiria mtu aliyepata ugonjwa ukamlaza kwa muda mrefu na pengine apoteze fahamu. Wagonjwa wa aina hii walikuwa wanaugua vindonda vilivyokuwa vinatoa harufu. And guess what? Zamani ndege na wanyama walao mizoga walikuwa wengi na walikuwa karibu na makazi ya watu. Hivyo basi, kitendo cha mtu kuwa karibu na umauti na kutoa harufu kilikuwa kinavutia ndege kama bundi wanatua karibu na makazi ya mwenye mgonjwa, wengine mpaka kwenye paa. Hii ndiyo ilifanya watu waamini kuwa bundi ni ishara ya kifo na imani imekuwepo mpaka l