Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Ni jambo lisiloeleweka kwanini Bunge kupitia kamati husika linashindwa kuichunguza na kuikagua NSSF ambayo kwa sasa ni mahututi. Kwa muda wa miaka miwili sasa NSSF imekuwa ikishindwa kuwalipa kwa wakati wastaafu, inachofanya kwanza ni kukusanya michango ya walio kazini (hand to mouth) ili iweze kuwalipa wastaafu. Katika miaka hii miwili NSSF imekuwa ikitumia kisingizio cha uhakiki, kabla ya hapo ilikuwa ikitumia kisingizio cha shirika la POSTA kuchelewesha malipo, hata hivyo sasa ni NSSF ndio wenye jukumu la kutoa malipo lakini wanashindwa.
Haitakuwa jambo jema Bunge kusubiri mpaka lione NSSF imekufa, wakati ni huu kabla mamia ya wastaafu hawajaathirika.
Haitakuwa jambo jema Bunge kusubiri mpaka lione NSSF imekufa, wakati ni huu kabla mamia ya wastaafu hawajaathirika.