Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Waziri wa Afya, Jenista Mhagama anatarajiwa kuwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26, jijini Dodoma leo Juni 2, 2025.
Wizara ya Afya imeliomba Bunge kuidhinishia TSh trilioni 1.6 kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele 10 katika mwaka wa fedha 2025/26.
Waziri wa Wizara hiyo, Jenista Mhagama amesema kati ya fedha hizo TSh bilioni 626 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na TSh bilioni 991 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Kwa mwaka wa fedha 2025/26, Wizara imepanga kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 62.433. kwa ajili ya matumizi ya kawaida sawa na Asilimia 39 ya bajeti iliyotengwa, ambapo kiasi cha Shilingi 475,418,119,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara ya Wizara na Taasisi zilizo chini yake, na kiasi cha Shilingi 151,015,017,000.00 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.
"Serikali kupitia Wizara ya Afya imeimarisha huduma za Mkoba za Madaktari Bingwa wa Dkt. Samia, kumewezesha kuwafikia Watanzania zaidi ya 154,015 katika Halmashauri zote nchini pamoja na kujengea uwezo watumishi 9,434"
"Akinamama 135,526 wameokolewa maisha yao wakati wa uzazi kupitia Mfumo wa rufaa za dharura wa Mama ulioasisiwa na Mheshimiwa Rais wa Jam-huri ya Muungano wa Tanzania unaotekelezwa nchi nzima."
"Maono ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu uzazi salama, mifumo bora ya rufaa, uwajibikaji katika utendaji, miundombinu, vifaa na vifaa tiba ikiwemo ushirikishwaji wa vyama vya kitaaluma vimewezesha kupunguza vifo vya akinamama vitokanavyo na uzazi kutoka 556 hadi 104 kwa kila vizazi hai 100,000."
"Wizara imejenga vituo vipya vya kutolea huduma za afya 580 katika ngazi zote ili kusogeza huduma karibu na wananchi na hivyo kufanya jumla ya vituo vya kutolea huduma kufikia 12,846. Kati ya vituo hivyo, vituo vya umma ni 7,627 na binafsi ni 5,219. Aidha, vitanda vya kulaza wagonjwa vimeongezeka kutoka 145,374 hadi kufikia vitanda 153,683."
"Jumla ya wananchi 39,386,226 walipata huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini kote. Takwimu za utoaji wa huduma za afya zinaonesha kwamba asilimia 81 ya wananchi wanapata huduma katika ngazi ya afya ya msingi, hali hiyo inaonesha juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali katika uwekezaji na uimarishaji wa huduma katika ngazi ya afya ya msingi na kuleta hudum karibu na wananchi."
"Hospitali ya Taifa, Hospitali maalum, Hospitali za rufaa za kanda na mikoa zimeweza kutoa huduma za afya kwa njia ya msamaha zenye thamani ya Shilingi Bilioni 34.7 kwa wananchi 268,244 wasio na uwezo waliopatiwa huduma katika Hospitali za Rufaa. Huduma zilizoongoza kutolewa misamaha ni huduma za uchujaji damu (Dialysis), huduma za mionzi kwa wagonjwa wa saratani, vipimo vya maabara, huduma za radiolojia, huduma za upasuaji, gharama za kumuona daktari, dawa na huduma za wagonjwa mahututi (ICU)."
"Wizara imeendelea kutekeleza Mpango Jumuishi wa Pili wa Taifa wa Lishe kwa kuwafikia watoto 9,456,378 kwa kuwapatia matone ya vitamin A sawa na asilimia 99.8 ya lengo la watoto 9,468,207."
"Katika kuwezesha wananchi kutumia vyakula vilivyoongezwa virutubishi muhimu jumla ya mashine 230 za kunyunyizia viru-tubishi (dosifiers) zimefungwa katika mikoa yote nchini na hivyo kufikia jumla ya mashine 1,402 ikilinganishwa na machine 1,172 mwaka 2024."
"Kufuatia uwepo wa mazingira wezeshi ya uzalishaji wa virutubishi, jumla ya kilo 65,946 zimezalishwa na kusambazwa nchini kote."
Vipaumbele vya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2025/26

- Kuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza yakiwemo magonjwa ya milipuko, magonjwa yasiyoambukiza, magonjwa yanayosababishwa na lishe duni pamoja na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
- Kuimarisha upatikanaji na ubora wa huduma za afya zinazotolewa katika ngazi zote kuanzia Zahanati hadi Taifa.
- Kuimarisha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya nchini, ikiwa ni pamoja na kuendeleza utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.
- Kuendeleza kufanya tafiti na kuhimiza matumizi ya matokeo ya tafiti hizo kwa maeneo ya kimkakati.
- Kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto, ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga.
- Kuimarisha upatikanaji na uendelezaji wa wataalam katika Sekta ya Afya kwa fani za kati, ubingwa na ubingwa bobezi.
- Kuimarisha huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi pamoja na kuimarisha tiba utalii nchini.
- Kuendeleza na kusimamia afua za Tiba Asili na Tiba Mbadala.
- Kuimarisha upatikanaji wa huduma za tiba dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukiza na magonjwa ya milipuko.
- Kuimarisha huduma za afya ya akili, huduma za utengamao hususan kwa watoto, wazee na watu wenye ulemavu.