Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Wabunge wamepitisha makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2025/2026, jijini Dodoma leo Juni 3, 2025.
Katika mjadala wa kupitisha bajeti hiyo wajumbe wametoa ushauri mbalimbali ikiwemo Serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama za matibabu ya baadhi ya magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo usafishaji wa figo.
Kuhusu baje ya Wizara ya Afya: Bunge la 12, Mkutano wa 19, Kikao cha 37, Juni 02, 2025
📊 Takwimu Muhimu za Bajeti na Mafanikio:
1. Mafanikio ya Sekta ya Afya (2021–2025):
Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali: Vimeongezeka kutoka 8,549 mwaka 2021 hadi 12,846 Machi 2025 – ongezeko la vituo 4,297.
Vitanda vya Wagonjwa: Vimeongezeka kutoka 86,131 hadi 153,683, ICU kutoka 258 hadi 1,362.
Vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi: Vimepungua kutoka 556 hadi 104 kwa kila vizazi hai 100,000.
Watoto wachanga waliohudumiwa: 1,517,219 (88.9%) walipata huduma ndani ya siku tatu za kwanza baada ya kuzaliwa.
2. Uwekezaji katika Huduma za Afya:
Tiba utalii: Wagonjwa kutoka nje ya nchi wameongezeka kutoka 5,705 mwaka 2021 hadi 12,180 Machi 2025.
Samia Health Super Specialization: Wataalam 2,779 wamepatiwa mafunzo ya ubingwa.
Viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba: Viwanda 10 vipya vimeanzishwa nchini.
Mashine za PET CT Scan: 1 ya kisasa yenye thamani ya Tsh Bilioni 18.5 imefungwa.
3. Fedha na Bajeti:
Makusanyo ya maduhuli hadi Machi 2025: Tsh 603.7 bilioni (asilimia 80 ya lengo).
Jumla ya bajeti ya mwaka 2024/25: Tsh 1.31 trilioni.
Fedha zilizopokelewa hadi Machi 2025: Tsh 1.23 trilioni (asilimia 94).
4. Huduma Rafiki kwa Vijana:
Vituo vya kutoa huduma za afya ya uzazi kwa vijana: Vimeongezeka hadi kufikia 1,561 kutoka 1,111 mwaka 2024.
5. Chanjo:
Utoaji wa chanjo za kawaida umeongezeka kutoka asilimia 81 hadi asilimia 97.