Bunge la 12 Mkutano wa 19 Kikao cha 45 Juni 12, 2025 Dodoma

Bunge la 12 Mkutano wa 19 Kikao cha 45 Juni 12, 2025 Dodoma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Leo Juni 12, 2025 Waziri wa Fedha Dr. Mwigulu Nchemba atawasilisha Bajeti Kuu ya Serikali 2025/2026, nini vitakuwa vipaombele vya serikari? Matarajio ya Wanachi, Taasisi na Asasi za Kiraia yatafikiwa?

Kabla ya kuwasilisha hotuba hiyo, Bunge linapitisha hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo kuhusu mapitio ya hali ya Uchumi kwea Taifa.

"Mheshimiwa Spika mwaka 2024 pato halisi la Taifa lilifikia Shilingi Trilioni 156.6 kutoka Shilingi Trilioni 148.5 kwa mwaka 2023 sawa na ukuaji asilimia 5.5 na kuifanya nchi yetu kuwa miongoni mwa nchi zilizokuwa na ukuaji mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki"

"Ukuaji huo ulichangiwa na jitihada mbalimbali za Serikali, Sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo ikiwa ni pamoja na kuanza uzalishaji wa Umeme katika Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP)"

"Mhe. Spika kwa mwaka 2024 Sekta Tano (5) zilizoongoza kwa ukuaji wa Uchumi ni pamoja na Sanaa na Burudani iliyokuwa kwa asilimia 17.1, Uzalishaji na Usambazaji wa Umeme iliyokuwa kwa asilimia 14.4, Habari na Mawasiliano iliyokuwa kwa asilimia 14.3, Fedha na Bima iliyokuwa kwa asilimia 15.8 na Afya kwa asilimia 10.1"

"Sekta Tatu (3) zilizochangia zaidi takribani nusu ya Pato la Taifa ni Kilimo iliyokuwa asilimia 26.3, Ujenzi - asilimia 12.8 na Uchimbaji wa Madini na Mawe - asilimia 10.1"

"Katika siku za mbeleni Serikali itaendelea kuongeza tija zaidi kwenye uzalishaji katika Kilimo ili kiendelee kuwainua Watanzania wengi zaidi kimapato"

Kuhusu mfumo wa Bei nchini

"Mhe. Spika mfumko wa bei nchini ulipungua na kufikia asilimia 3.1 kwa mwaka 2024 ikilinganishwa na asilimia 3.8 2 kwa mwaka 2023"

"Akiba ya Fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha, kukidhi mahitaji ya Uagizaji wa bidhaa na Huduma kutoka nje ya nchi ambapo mwaka 2024 akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Kimarekani Bilioni 5.546"

"Pato la Taifa linatarajiwa kuendelea kupanda hadi asilimia 6.0 mwaka 2025 na kufikia asilimia 6.1 mwaka 2026. Msingi wa mafanikio haya ni utekelezaji thabiti wa sera bora za uchumi na ushiriki wa sekta binafsi katika maendeleo ya Taifa."

"Serikali ya CCM ilitumia Shilingi bilioni 961.5 kama Ruzuku iliyotolewa kwa kaya maskini, ili kuziwezesha kuongeza Kipato"

"Nihitimishe kwa kulihakikishia Bunge lako tukufu kuwa hali ya uchumi wa nchi yetu kwa sasa ni himilivu, ukiwa na mwelekeo chanya na ukuaji endelevu. Kuimarika kwa uchumi kunatokana na usimamizi makini wa sera za uchumi jumla pamoja na ushiriki wa wananchi wote katika ujenzi wa Taifa."
 

Attachments

Back
Top Bottom