Leo Juni 12, 2025 Waziri wa Fedha
Dr. Mwigulu Nchemba atawasilisha Bajeti Kuu ya Serikali 2025/2026, nini vitakuwa vipaombele vya serikari? Matarajio ya Wanachi, Taasisi na Asasi za Kiraia yatafikiwa?
Kabla ya kuwasilisha hotuba hiyo, Bunge linapitisha hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo kuhusu mapitio ya hali ya Uchumi kwea Taifa.
"Mheshimiwa Spika mwaka 2024 pato halisi la Taifa lilifikia Shilingi
Trilioni 156.6 kutoka Shilingi
Trilioni 148.5 kwa mwaka 2023 sawa na ukuaji
asilimia 5.5 na kuifanya nchi yetu kuwa miongoni mwa nchi zilizokuwa na ukuaji mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki"
"Ukuaji huo ulichangiwa na jitihada mbalimbali za Serikali, Sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo ikiwa ni pamoja na kuanza uzalishaji wa Umeme katika Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP)"
"Mhe. Spika kwa mwaka 2024 Sekta Tano (5) zilizoongoza kwa ukuaji wa Uchumi ni pamoja na
Sanaa na Burudani iliyokuwa kwa
asilimia 17.1, Uzalishaji na Usambazaji wa Umeme iliyokuwa kwa
asilimia 14.4, Habari na Mawasiliano iliyokuwa kwa
asilimia 14.3, Fedha na Bima iliyokuwa kwa
asilimia 15.8 na Afya kwa
asilimia 10.1"
"Sekta Tatu (3) zilizochangia zaidi takribani nusu ya Pato la Taifa ni Kilimo iliyokuwa
asilimia 26.3, Ujenzi -
asilimia 12.8 na Uchimbaji wa Madini na Mawe - asilimia 10.1"
"Katika siku za mbeleni Serikali itaendelea kuongeza tija zaidi kwenye uzalishaji katika Kilimo ili kiendelee kuwainua Watanzania wengi zaidi kimapato"
Kuhusu mfumo wa Bei nchini
"Mhe. Spika mfumko wa bei nchini ulipungua na kufikia asilimia 3.1 kwa mwaka 2024 ikilinganishwa na asilimia 3.8 2 kwa mwaka 2023"
"Akiba ya Fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha, kukidhi mahitaji ya Uagizaji wa bidhaa na Huduma kutoka nje ya nchi ambapo mwaka 2024 akiba ya fedha za kigeni ilifikia
dola za Kimarekani Bilioni 5.546"
"Pato la Taifa linatarajiwa kuendelea kupanda hadi asilimia 6.0 mwaka 2025 na kufikia asilimia 6.1 mwaka 2026. Msingi wa mafanikio haya ni utekelezaji thabiti wa sera bora za uchumi na ushiriki wa sekta binafsi katika maendeleo ya Taifa."
"Serikali ya CCM ilitumia Shilingi
bilioni 961.5 kama Ruzuku iliyotolewa kwa kaya maskini, ili kuziwezesha kuongeza Kipato"
"Nihitimishe kwa kulihakikishia Bunge lako tukufu kuwa hali ya uchumi wa nchi yetu kwa sasa ni himilivu, ukiwa na mwelekeo chanya na ukuaji endelevu. Kuimarika kwa uchumi kunatokana na usimamizi makini wa sera za uchumi jumla pamoja na ushiriki wa wananchi wote katika ujenzi wa Taifa."