Bunge la 12, Mkutano wa 19, Kikao cha 51, 23 Juni 2025

Bunge la 12, Mkutano wa 19, Kikao cha 51, 23 Juni 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Wakati mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiendelea jijini Dodoma, leo Juni 23, 2025 pamoja na mambo mengine Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atawasilisha taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2024.

Wabunge, wataendelea kuchangia bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/2026.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Rais Samia ameagiza kila wilaya ambayo haina VETA ya serikali ijengewe VETA ya serikali. Ujenzi unaendelea katika wilaya 64 Tanzania nzima.

Vile vile, wakati Rais Samia anakula kiapo, kulikuwa na mikoa mitano ambayo haikuwa na VETA za mikoa. Mikoa mingine ilikuwa tayari imeanza ujenzi lakini haujakamilika. Hata hivyo, alivyoingia madarakani, katika bajeti yake ya kwanza alihakikisha fedha zinaelekezwa kukamilisha VETA ya Geita, ambayo imepangwa kuwa maalum kwa masuala ya madini. Aidha, tumekamilisha VETA ya Simiyu, Ludewa na Rukwa, na kwa sasa ujenzi wa VETA ya Mkoa wa Songwe unaendelea.
 
Back
Top Bottom