Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa leo, Juni 26, 2025, kuwasilisha hoja ya kufunga shughuli za Bunge ikiwa ni hitimisho la Mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika Mkutano huo umejadili mambo mbalimbali ikiwemo Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2024, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2025/2026 na bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Kesho, Juni 27, 2025, Rais atahitimisha rasmi Bunge la 12, hatua itakayofungua rasmi dirisha la maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akihitimisha Mkutano wa 19 wa Bunge, Juni 26, 2025.
"Ninawashukuru sana wana Ruangwa kwa kuniunga mkono na kunipatia ushirikiano katika kipindi chote nilipokuwa nikitekeleza majukumu ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezi Mungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena."
"Mhe. Spika, niruhusu kwa unyenyekevu mkubwa nigusie jambo la kihistoria, lenye hisia na lenye uzito mkubwa kwa Taifa letu. Kama Taifa, tunakumbukumbu ya majonzi na maumivu makubwa tuliyoyapitia kwa tukio la tarehe 17 Machi 2021, pale ambapo tulimpoteza Kiongozi wetu kipenzi, Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Ukweli usiopingika ni kwamba, tukio hili lilituacha sote tukiwa na majonzi, taharuki na giza nene."
"Mhe. Spika, katika giza hilo la huzuni iliyogubika taifa letu, Mwenyezi Mungu alimpa ushupavu, ujasiri na utulivu wa kipekee Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na akawa faraja kubwa kwa Watanzania. Kiongozi huyu alisimama imara katika upepo mkali wa historia ya nchi yetu, alichukua hatamu ya uongozi kwa utulivu, kwa busara na kwa ujasiri usioyumba. Katika kipindi hiki alitufundisha kuwa utulivu si udhaifu, bali ni nguvu ya ndani inayotoka kwa Mungu katika kushughulika na masuala makubwa ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ndani na nje ya mipaka ya Nchi."
"Mhe Spika, katika kipindi hicho kigumu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alinionesha imani kubwa na hatimaye aliamua niendelee kumsaidia kwa nafasi ya Waziri Mkuu. Hili si jambo dogo. Ninayakumbuka maneno yake kwangu: “Kassim Tuendelee kushirikiana kulitumikia Taifa letu, simamia shughuli za Serikali”. Ninamshukuru kwa moyo wa dhati Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa imani aliyoionesha kwangu.”Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania, Akihitimisha Mkutano wa 19, wa Bunge la 12 la Tanzania."
"Mhe. Spika, niruhusu nimnukuu Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, aliyewahi kusema: ‘Hapa Tanzania leo hakuna mwanasiasa maarufu kama Rais Samia, iwe ndani ya Chama ama nje ya Chama Cha Mapinduzi.’ Maneno haya yana uzito mkubwa na yanabeba ukweli wa hali halisi."
"Ninawapongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 na kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya watani wao wa jadi Simba SC. Hii ni ishara ya ushindani wa hali ya juu katika ligi yetu. Kadhalika, nawapongeza kwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika – ni hatua muhimu kwa ustawi na ubora wa soka letu. Nawapongeza pia Simba SC kwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mafanikio haya ya vilabu vyetu ni heshima kwa taifa letu."
"Nitumie fursa hii kuwakumbusha wadau mbalimbali kila mmoja kwa nafasi yake, ikiwemo wananchi ambao ni wapiga kura, kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo. Serikali itahakikisha kila raia mwenye sifa anapata haki ya kupiga kura au kugombea bila vikwazo. Pia, tunapaswa kuilinda na kuitunza tunu ya amani na utulivu wa nchi yetu kabla, wakati na baada ya uchaguzi."