Bunge la 12, Mkutano wa 19 Kikao cha Kwanza, Aprili 8, 2025

Bunge la 12, Mkutano wa 19 Kikao cha Kwanza, Aprili 8, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 umeanza leo Aprili 8, 2025 Jijini Dodoma, ukiwa ni mahususi kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2025/2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma, Ofisi ya Bunge, miongoni mwa shughuli zitakazofanyika leo kutolewa kwa taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, na uwasilishwaji wa randama za makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha wa 2025/2026.

Pia, kutakuwa na maswali kutoka kwa wabunge kwenda wizara mbalimbali ambapo wizara zikazoulizwa maswali leo ni pamoja na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali (TAMISEMI), Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Nishati, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Maji, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.


Rais Samia Suluhu Hassan amesaini Muswada wa Sheria ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wa mwaka 2024, na hivyo kuwa sheria kamili. Tangazo hilo limetolewa Bungeni Aprili 8, 2025 na Naibu Spika Mussa Zungu. Sheria hiyo inalipa TBC msingi wa kisheria wa kuboresha utendaji, kukabiliana na changamoto za kifedha na kiteknolojia, na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Muswada huo ulijadiliwa na kupitishwa katika kikao cha tatu cha mkutano wa 18 wa Bunge.

Serikali kupunguza gharama za usafishaji figo kwa kuongeza vituo

"Serikali imepanga kupunguza gharama za huduma za usafishaji figo (dialysis) kwa kuongeza vituo vya huduma hiyo katika hospitali 15 za rufaa za mikoa na za kanda nchini," amesema Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel, wakati akijibu swali la mbunge wa Mbulu Mjini, Isaay Zacharia.

Ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuondoa mzigo wa gharama kubwa kwa wagonjwa wa figo na kuwawezesha kupata huduma kwa urahisi zaidi katika maeneo yao ya karibu.
 
waambiwe kabisa hoja ya bajeti ya uchaguzi 2025, isijadiliwe kabisa kwa sababu uchaguzi hautakuwepo!!👿
 
Bunge limepoteza mvuto siyk km lile la Mh Sita Bunge la viwango na kasi.
 
Back
Top Bottom