Bunge la 12, Mkutano wa 19, Kikao cha Nane, tarehe 17 Aprili 2025

Bunge la 12, Mkutano wa 19, Kikao cha Nane, tarehe 17 Aprili 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 unaendelea leo Aprili 17, 2025 bungeni Jijini Dodoma ambapo hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka wa fedha 2025/2026 itaendelea kujadiliwa.

Kama kawaida kutakuwa na Kipindi cha Maswali na Majibu kwa wabunge kuiuliza maswali Serikali.



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu, ametoa wito kwa madaktari na wauguzi kote nchini kuonesha utu wanapowahudumia wagonjwa, hasa wale wanaoshindwa kulipa gharama za matibabu kwa wakati. Wakati wa kipindi cha maswali na majibu, Zungu alitoa kauli hiyo kufuatia swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest, aliyehoji lini Serikali itapeleka watumishi wa afya katika wilaya za pembezoni kama Kyelwa.

"Mheshimiwa Naibu Waziri, waambie madaktari na watumishi wawe na utu. Mtu amelazwa kwa huduma ya dialysis, analipia kila siku, lakini siku moja tu akishindwa kulipa, wanampita bila kumpa huduma. Hii ni hatari sana,"

Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dk Festo Dugange, amekiri kuwepo kwa matukio hayo na kusema yanadhihirisha ukosefu wa utu, licha ya Serikali kugharamia mishahara, umeme, vifaa tiba na huduma nyingine kwa manufaa ya wananchi.
 
😃😃😃😃 wabunge kuuliza maswali serikaliiii 😃
 
Sipotezi muda wangu kuangalia bunge lisilo na tija
 
Back
Top Bottom