Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 unaendelea leo Aprili 14, 2024 bungeni Jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine wabunge wataendelea kuijadili hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Kama kawaida kutakuwa na Kipindi cha Maswali na Majibu kwa wabunge kuiuliza maswali Serikali.
Akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge Joseph Michael Mkundi Bungeni leo Aprili 14, 2025 aliyehoji "Takwimu zinaonesha Wagonjwa wengi wa Saratani waliopo katika Taasisi ya Ocean Road wanatokea Kanda ya Ziwa, kwa nini Serikali isiboreshe Hospitali ya Rufaa ya Bugando Kitengo cha Saratani ili kusaidia uwepo mgawanyiko wa taasisi hizo kuhusumia watu?"
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema utafiti unaonesha Wagonjwa wengi waliopo kwenye Taasisi ya Ocean Road wanatokea Kanda ya Kaskazini na sio Kanda ya Ziwa kama ambavyo imekuwa ikiaminika hivyo.
"Tunaendelea na utafiti wa kina kubaini visababishi halisi vya saratani katika Kanda ya Ziwa, ambapo saratani za kibofu cha mkojo, mji wa uzazi kwa wanawake, damu, macho na figo zimebainika kuongoza,"
"Tumechukua sampuli za damu 9,600 kutoka kwa watu wasio na saratani kwa kulinganisha na wagonjwa, huku sababu zinazotajwa kwa sasa zikiwa bado ni nadharia. Serikali inaendelea kutoa elimu na kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kudhibiti Saratani katika maeneo saba ya kipaumbele."
Pia soma:
~ Dkt. Mollel: Utafiti unaonesha Wagonjwa wengi wa Ocean Road wanatokea Kanda ya Kaskazini si Kanda ya Ziwa