Bunge la 13, Mkutano wa Tatu, Kikao cha Tano, Tarehe 09 Aprili, 2026

Bunge la 13, Mkutano wa Tatu, Kikao cha Tano, Tarehe 09 Aprili, 2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Wakati mkutano wa tatu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania ukiendelea, leo Aprili 9, 2026 pamoja na mambo mengine Wabunge wateule wawili wataapa kiapo cha uaminifu na ahadi ya Uzalendo, wakiwa ni Wabunge wapya walioteuliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan.

Wabunge hao ni Angela Kizigha na Dkt. Evaline Munisi.

Sambamba na hilo Wabunge watapata nafasi ya kuuliza maswali kwa Waziri Mkuu na kupata majibu ya papo kwa papo.

Mara baada ya kipindi hicho, Wabunge watapata nafasi nyingine ya kuuliza maswali ya kawaida kwa Mawaziri na kupatiwa majibu.

Wakati huo huo, Wabunge wataendelea kuchangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/2027 iliyowasilishwa bungeni Aprili 1, 2026 na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba.


Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, ameweka wazi mpango mpya wa Serikali unaolenga kutatua changamoto ya mitaji kwa vijana wanaohitimu masomo yao nchini. Akizungumzia hali ya upatikanaji wa mikopo, Nchemba amebainisha kuwa Serikali imeanza mchakato wa kuangalia uwezekano wa kijana kutumia cheti chake cha kuhitimu kama dhamana ya kukopa fedha za kuanzia maisha au biashara.

"Tumeanza kuwaza kwamba kijana aweze kutumia cheti chake alichohitimu kuweza kukopa baada ya kuhitimu, ili kuondoa kikwazo cha kukosa dhamana ambacho kimekuwa kikiwakwamisha wahitimu wengi"
 
Back
Top Bottom