Jaluo_Nyeupe
JF-Expert Member
- Dec 21, 2010
- 2,824
- 2,264
nilidhani umeiweka hapa ili tuichangie.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chadema ni kama mwanamke mjamzito akifanyiwa zuri kwake karaha akifanyiwa baya ndio tabu! Sasa mnataka Serikali ipuuze kila linalosemwa na Upinzani!
Hii imekaaje wadau?
Mbona kama nilimsikia akisema sh 50,000?...na wabunge wakaipigia kelele/zomea! Kwa vyovyote vile kutakuwa na 'ulaji' zaidi kwa 'wazee wa fedha'!
Hata mimi nilisikia 50,000. Au hii siyo final version ya hotuba?
Yaani humu katika hiyo bajeti ni full usanii, yaani naona leo Mkulo atapata usingizi anasubiri kuona jinsi itavyopokewa na wananchi.Duuh... nakaza mkanda.
[HTML]Mheshimiwa Spika, mapato halisi ya ushuru wa forodha yalikuwa shilingi bilioni 343.2, sawa na asilimia 70 ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi bilioni 493.1. Mapato kutokana na ushuru wa bidhaa kutoka nje yalifikia shilingi bilioni 455.0, sawa na asilimia 73 ya bajeti ya shilingi bilioni 622.8, wakati shilingi bilioni 258.7, zilikusanywa kutokana na ushuru wa bidhaa zilizozalishwa nchini, ikilinganishwa na bajeti ya shilingi bilioni 404.2, sawa na asilimia 64. Aidha, mapato kutokana na Kodi ya Ongezeko la Thamani kutoka nje yalifikia shilingi bilioni 664.6, ikilinganishwa na bajeti ya shilingi bilioni 999.3, sawa na asilimia 67, wakati shilingi bilioni 611.2 zilikusanywa kutokana na Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa mauzo ya ndani, ikilinganishwa na bajeti ya shilingi bilioni 992.3 sawa na asilimia 62. Makusanyo halisi yanayotokana na Kodi ya Mapato yalikuwa shilingi bilioni 1,255.8, ikiwa ni asilimia 74 ya bajeti ya shilingi bilioni 1,702.3. Aidha, mapato halisi yatokanayo na vyanzo vingine vya kodi yalikuwa shilingi bilioni 449.7, ikiwa ni asilimia 72 ya bajeti ya shilingi bilioni 620.9
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010/11, Serikali ilipanga kukopa shilingi bilioni 1,397.6, kutoka vyanzo vya ndani ili kugharamia bajeti yake. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 600.0 ni kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo na shilingi bilioni 797.6 ni kwa ajili ya kulipia hatifungani zitakazoiva. Hadi Machi 2011, kiasi cha shilingi bilioni 1,107.5 kilikopwa kwa ajili hiyo. Kiasi hiki kinajumuisha dhamana za Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 607.6 zilizouzwa katika soko ili kulipia zilizoiva na shilingi bilioni 499.9 zilitumika kugharamia miradi ya maendeleo.
kuwataka wafanyabiashara wenye namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN), kuzuia asilimia 2 kila wanapofanya malipo kwa wasiokuwa na namba hizo, kutokana na bidhaa au huduma walizopata kutoka kwao, ili kuwahamasisha wasiokuwa na namba kwenda kusajiliwa.
30. Mheshimiwa Spika, kufuatia kuanza kutengemaa kwa uchumi wa dunia baada msukosuko wa kiuchumi duniani na nia ya Serikali ya kuboresha upatikanaji wa taarifa zilizohakikiwa kuhusu mwenendo mzuri wa Taifa kiuchumi, kisiasa, na utawala bora. Serikali inaendelea kumtafuta Mshauri Mwelekezi wa Kimataifa kwa ajili ya kusimamia zoezi la kutathmini uwezo wa Nchi wa kukopa na kulipa madeni (Sovereign Credit Rating). Mambo muhimu yanayozingatiwa katika tathmini hii ni pamoja na; hali ya utulivu wa kisiasa; kasi ya kukua kwa uchumi; udhibiti wa usimamizi wa bajeti ya Serikali; udhibiti wa masoko ya fedha na hali ya mfumuko wa bei; na urari wa malipo ya nje ya nchi. Hatua hii itasaidia kuwavutia wawekezaji na wakopeshaji kutokana na kuwepo kwa taarifa ya hali ya uchumi, siasa na utawala wa nchi na hivyo kurahisisha upatikanaji wa mikopo nafuu kutoka nje ya nchi kwa Serikali na kwa sekta binafsi.
31. Mheshimiwa Spika, mwaka 2000/01, Deni la Taifa, lilikuwa Dola za Kimarekani bilioni 8.55 ikilinganishwa na Dola bilioni 10.01 mwaka 2005/06 na kupungua mwaka 2006/07 hadi kufikia Dola bilioni 7.53. Kupungua kwa deni hilo kulitokana na misamaha mbalimbali ya madeni kutoka nchi wahisani na mashirika ya fedha ya kimataifa chini ya utaratibu wa (HIPC na MDRI). Aidha, Deni la Taifa liliongezeka hadi kufikia Dola bilioni 10.54 mwaka 2009/10, kutoka Dola bilioni 9.36 mwaka 2008/09. Kati ya Deni la mwaka 2009/10, Dola bilioni 5.99 ni deni la nje na Dola bilioni 4.55 ni deni la ndani, ikijumuisha Dola bilioni 1.63 za dhamana za Serikali kwa miradi ya Wizara, Idara na Taasisi za Serikali.
[FONT=Tahoma]i) Kilimo na umwagiliaji kimetengewa shilingi bilioni 926.2 ikilinganishwa na shilingi bilioni 903.8 mwaka 2010/11, sawa na ongezeko la asilimia 2.5;[/FONT]
[FONT=Tahoma][/FONT]
i) Elimu imetengewa shilingi bilioni 2,283.0 ikilinganishwa na shilingi bilioni 2,045.4 mwaka 2010/11, sawa na ongezeko la asilimia 12; na
ii) Afya imetengewa shilingi bilioni 1,209.1 ikilinganishwa na shilingi bilioni 1,205.9 mwaka 2010/11, sawa na ongezeko la asilimia 0.3.
MASUALA YANAYOHUSU SERIKALI ZA MITAA:
70. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuboresha utendaji na uwajibikaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia Programu ya Maboresho ya Serikali za Mitaa (LGRP II) ili kuwawezesha Wakurugenzi kusimamia majukumu yao kikamilifu. Serikali pia itawajengea uwezo Waheshimiwa Madiwani ili wasimamie utendaji wa Halmashauri zao na kuhakikisha nidhamu ya kazi inaimarishwa kulingana na sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma. Aidha, kamati za kupambana na rushwa pamoja na kamati za maadili za Halmashauri zitaimarishwa ili kusimamia nidhamu ya watumishi wa kada zote na kuhakikisha utendaji wao unazingatia maslahi ya taifa.
i) Kuanzisha utaratibu wa marejesho ya Kodi kwenye mauzo ya rejareja kwa bidhaa za ndani zinazouzwa kwa abiria ambao sio raia wa Tanzania wanaosafiri nje ya nchi. Utaratibu huu utaanza kutekelezwa kwa kuanzia na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa mauzo ya thamani ya shilingi 400,000 na zaidi. Utekelezaji wa utaratibu huu mpya utaanza rasmi tarehe 1 Januari 2012.
i) Kuondoa unafuu wa Kodi ya Ongezeko la Thamani uliokuwa unatolewa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (Non Governmental Organizations). Hatua hii haitazihusu Taasisi za Kidini (Religious Organizations); na
ii) Kutoa unafuu wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa Mashirika yasiyo ya kiserikali (Non Governmental Organizations) kwa vifaa vya matumizi binafsi ya kawaida (household consumables) kama vile vyakula, mavazi, na vifaa kama sabuni ambavyo vinatolewa msaada kwenye vituo mahsusi vya kulelea watoto yatima na shule.