Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

HTML:
i)     Kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa Serikali na wanaofanya kazi kwenye Taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya Serikali..
Huu ni uhuni mwingine. Hizi posho za wafanyakazi wa serikali ni zile housing allowances labda na medical. kwa wale wafanyakazi basic. Lakini wao wanalipana posho saana kwahiyo wanajiondolea kodi. Hili hapana kwa kweli.
 
HTML:
i)         Kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 50 badala ya asilimia 120 kwenye mifuko ya plastiki za microns 30 na zaidi yaani Polymers of ethylene na nyinginezo za (HS. Code 3923.2900).
Sera ya mazingira imefikia ukomo?
 
HTML:
i)     Ili kutatua tatizo la ucheleweshaji wa marejesho ya kodi (tax refunds) kwenye mafuta yanayonunuliwa na Kampuni za madini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itaanzisha utaratibu wa kuweka kiasi cha fedha kwenye Akaunti maalum (escrow account) ambacho kinawiana na kiwango cha mahitaji ya mafuta kwa mwezi. Aidha Kampuni itaruhusiwa kununua mafuta kwenye matanki ya Kampuni za waagizaji wa mafuta bila ya kulipia kodi kwa kiwango cha fedha ilichoweka kwenye akaunti. Endapo mahitaji ya mafuta kwa mwezi yatakuwa makubwa zaidi ya kiwango  ilichoweka kwenye akaunti, Kampuni hiyo itawajibika kuongeza fedha za ziada zenye kukidhi mahitaji yake. Hatua hii inatarajiwa kutatua tatizo la ucheleweshaji wa marejesho ya kodi iliyolipwa kwenye mafuta.
Kwenye hili nchi nyingine wanafanyaje? Tunasamehe kodi assume billion 300 halafu mapato billion 250. Ngoja tuone kwenye madini na hiyo kodi huwa wanasamehe kiasi gani
 
source;mwananchi
Neville Meena, Dodoma
KATIKA hali isiyotarajiwa, baadhi ya mawaziri na wabunge hawakuhudhuria Kikao cha Bunge cha jana jioni, wakati wa kusomwa kwa mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2011/12 yaliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo.

Hotuba hiyo ilisomwa kuazia saa 10.00 jioni na kuchukua muda wa saa 2:15. Hii ni bajeti ya kwanza ya Serikali tangu Rais Jakaya Kikwete alipochaguliwa kwa mara ya pili kuongozi nchi, kama ilivyo kwa Bunge la 10 ambalo linapokea na kujadili kwa mara ya kwanza bajeti hiyo chini ya uongozi wa Spika Anne Makinda.

Hata hivyo, kulikuwa na idadi kubwa ya
viti vilivyokuwa wazi wakati Waziri Mkulo alipokuwa akisoma bajeti hiyo na haikufahamika mara moja sababu za baadhi ya mawaziri na wabunge wengi kutohudhuria tukio hilo muhimu la kitaifa.

Jana ilikuwa ni siku ya tatu au kikao cha tatu cha Mkutano wa Nne wa Bunge la 10, ambao ulianza juzi, lakini tofauti na vikao vilivyowahi kufanyika ambavyo huwa na idadi kubwa ya wabunge wakati Serikali ikiwasilisha bajeti yake, kikao hicho kilikuwa na wabunge wachache.

Akizungumza mara baada ya kusomwa kwa bajeti hiyo jana, Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed alisema hali hiyo inaweza kusababishwa na baadhi ya wabunge kukata tamaa.

“Inawezekana wanaona bajeti ni yaleyale ya kila siku na wakifikiria Bunge hili ni refu wakadhani hakuna umuhimu wa kuja, jambo ambalo siyo sahihi,” alisema Hamad.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR -Mageuzi), David Kafulila ambaye alisema: “Tatizo ni kwamba wabunge walikata tamaa kabla ya bajeti haijasomwa, wanaona kama hakutakuwa na jipya.”

Hata hivyo, hali ilikuwa ni tofauti kwa wageni ambao walikuwa wengi kiasi cha wahudumu wa Ofisi ya Bunge kulazimika kuongeza idadi ya viti katika baadhi ya sehemu za wageni ambao wengi walikuwa kutoka katika taasisi mbalimbali vikiwamo vyama vya siasa, viongozi wa dini, mabalozi, wakuu wa mashirika ya kimataifa, viongozi wastaafu na wakuu wa vyombo vya dola.

Miongoni mwa waliohudhuria walikuwa ni Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, Makatibu
Wakuu wa Wizara, Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Wakuu wa Mikoa, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Ulaya, vyama vya wafanyakazi, vyombo vya habari
pamoja na taasisi mbalimbali.

Kuwasili eneo la Bunge
Waziri Mkulo aliwasili katika Viwanja vya Bunge saa 9.46 akiwa na mkoba (brifcase) uliokuwa umebadikwa stika yenye nembo ya Serikali katika pande zake mbili na maandishi yaliyosomeka "BAJETI YA SERIKALI 2011/2012."

Mara baada ya kushuka kwenye gari lake, waziri huyo aliunyanyua mkoba juu wake na kuugeuza kila upande, hivyo kutoa fursa kwa wapigapicha wa vyombo
mbalimbali vya habari waliokuwapo kunasa tukio hilo la kihistoria.

Saa 09.48, Mkulo aliingia katika lango kuu la Bunge, lakini hakwenda moja kwa moja ukumbini na badala yake alipumzika katika sehemu ya maalumu
akisubiri kuitwa na Spika.

Spika wa Bunge, Makinda aliingia ukumbini saa 09.58 akiongozwa na mpambe wa Bunge pamoja na makatibu wasaidizi watatu, ambao walikuwa ni wanaume wawili na mwanamke, na baada ya Siwa kuwekwa mahala pake wote walichukua nafasi zao kisha Spika kutoa ruhusa kwa wabunge kuketi.

Wabunge hao walikuwa wamesimama kutii mbiu iliyopigwa saa 09.57 na mpambe wa Bunge, ikiashiria kwamba Spika alikuwa tayari kuingia ukumbini.

Baada ya hatua hiyo, Spika alitoa fursa kwa Katibu kusoma ratiba ya tukio lililokuwa likifuata. Katibu huyo alisema: "Hoja za Serikali, hoja ya Waziri wa Fedha na
Uchumi," baada ya hapo Spika alimwita Waziri Mkulo kufika mbele ya Bunge na kuwasilisha Bajeti ya Serikali.

Mara milango miwili ya lango kuu la kuingia katika ukumbi wa Bunge ilifunguliwa na Waziri Mkulo aliingia ukumbini hapo akiongozwa na mmoja wa askari wa Bunge na kwenda moja kwa moja katika kizimba. Wakati wote huo alikuwa akisindikizwa na makofi ya wabunge.

Wakati Mkulo akitamka neno la kwanza katika hotuba hiyo ambalo ni "Mheshimiwa Spika...." Ilikuwa imetimu saa 10.00 jioni.

Wabunge wakunwa
Wakati Waziri Mkulo akisoma bajeti hiyo, wabunge walikuwa wakipiga makofi mara kwa mara ikiwa ni ishara ya kupongeza vipengele mbalimbali vilivyokuwamo na makofi yaliyochukua muda mrefu zaidi ni wakati Waziri Mkulo alipotangaza hatua za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

Miongoni matumizi hayo ni kudhibiti mishahara hewa, kupunguza idadi ya kaunti katika mamlaka za miji na mitaa nchini, kupunguza posho zisizo na tija, kupunguza safari za nje na ukubwa wa misafara ya viongozi na kupunguza semina na warsha ambazo kufanyika kwake kutaendelea kuhitaji kibali cha Waziri Mkuu.

Ilipotimu saa 11.51 Spika Makinda alilazimika kuwatuliza wabunge ambao walionekana kuanzisha mijadala midogo midogo isiyo rasmi baada ya Waziri Mkulo kutangaza ongezeko la faini kwa madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani, kutoka Sh20,000 za sasa hadi Sh50,000. Awali, katika hotuba yake, faini hiyo ilikuwa imependekezwa hadi kufikia Sh300,000.
 
SERIKALI imefanya maboresho katika mfumo kodi 11 tofauti, ikiwamo ile ya usalama barabarani baada ya kupandisha faini kwa mtu anayepatikana na kosa kutoka Sh20,00 hadi Sh50,000.
Hatua hiyo ya serikali inadaiwa itapunguza makosa ya barabarani na ajali zinazotokana na uzembe.

Akiwasilisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012 bungeni Dodoma jana, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, alisema mabadiliko hayo ya faini yametokana na kufanyiwa marekebisho sheria namba ya usalama barabarani.

“Napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Usalama Barabarani, Sura 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati wa uendeshaji gari barabarani kutoka Sh20, 000 hadi Sh50,000” alisema.

Sheria zingine ambazo zimefanyiwa marekebisho, ni ile ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Sheria ya Kodi ya Mapato, Ushuru wa bidhaa, Sheria ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi Stadi.

Mkulo alitaja sheria zingine kuwa, ni ushuru wa stempu, ushuru wa mafuta na ile ya petroli, leseni za biashara na marekebisho ya ada na tozo mbalimbali za wizara, mikoa na idara zinazojitegemea.

Waziri Mkullo alisema serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za sera na utawala, ili kuongeza mapato ya kodi na yasiyo ya kodi, kupanua wigo wa mapato maeneo mengine.

Pia, serikali imesamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa serikali na wanaofanya kazi kwenye taasisi zinazopata ruzuku kutoka serikalini.

Alisema serikali itaendelea kupitia sheria mbalimbali zinazotoa misamaha ya kodi kwa lengo la kuidhibiti, kusimamia mpango wa tatu wa Miaka mitano ya maboresho ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuendelea kuingiza sekta isiyo rasmi kwenye mfumo wa kodi.

Pia, serikali inapitia upya mfumo wa ukusanyaji kodi ya majengo kwenye majiji, miji, manispaa, wilaya na miji midogo; kufanya mapitio ya vyanzo vya mapato na mfumo wa ukusanyaji katika serikali za mitaa, ili kuongeza mapato.

Kuhusu marekebisho kodi zingine ikiwamo VAT, Mkullo alisema yamefanyika ili kuhamasisha uwekezaji na kuboresha uzalishaji sekta za kilimo, mifugo, viwanda, biashara na utalii.

Alisema kulingana na maboresho hayo, serikali imesamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye vipuri vya zana za kilimo; fyekeo, mashine za kukausha na kukoboa mpunga, mashine za kupandia mbegu na matrekta ya kukokota kwa mkono (power tillers).

“Lengo ni kuhamasisha matumizi ya zana bora za kilimo na kuvutia uwekezaji kwenye sekta ya kilimo, hatua ya kusamehe VAT kwenye chakula cha kuku inalengo la kuhamasisha uwekezaji nchini,” alisema.
Kodi zingine zimeondolewa katika nyuzi zinazotumika kutengenezea nyavu za kuvulia samaki, vipuri vya mashine za kunyunyizia na kutifua udongo na mashine za kupanda nafaka.

Pia, imeanzisha utaratibu wa marejesho ya kodi kwenye mauzo rejareja kwa bidhaa za ndani zinazouzwa kwa abiria, ambao siyo raia wa Tanzania wanaosafiri nje ya nchi.
 
CHAMA cha Walimu Tanzania CWT, kimesema hakijaridhishwana bajeti iliyosomwa jana na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo na elimu kutengewa Sh2,283.0 bilioni sawa na ongezeko la asilimia 12.Rais wa wa CWT, Gratian Mukoba alisema ongezeko hilo ni ‘changa la macho’ ikilinganishwa na ya mwaka jana ambayo licha ya kutengewa Sh2,045.4 bilioni, bado matatizo yamekuwa palepale.

Alisema serikali kama ina nia nzuri na maendeleo ya elimu, haina budi kutenga asilimia sita ya pato la taifa kwa ajili ya elimu akisema sekta hiyo inakabiliwa na matatizo mengi ikilinganishwa na nyingine.

“Hiyo asilimia 12 wanayoisema ukifanya mahesabu vizuri hata asilimia tatu hatujafika, sasa unategemea maendeleo ya elimu yatapatikana wapi wakati wenzetu wanakimbilia asilimia sita hadi saba bado hajaisaidia sekta ya elimu,” alisema Mukoba.

Alisema Kenya inatumia asilimia sita ya pato la taifa katika elimu, Uganda asilimia 5.8,Rwanda asilimia 3.8 wakati Tanzania bado iko asilimia 1.2 ambayo alisema ni sawa na bure ikilinganishwa na matatizo yanayoikabili sekta hiyo.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk Evance Rweikiza alisema bajeti hiyo ni nzuri kwa kuwa imegusa maeneo mengi yaliyokuwa yakilalamikiwa na sekta binafsi.

"Nilivyoiona ni nzuri, imegusa maeneo tuliyokuwa tukiyalalamikia watu wa sekta binafsi, imegusa miundombinu, umeme, uwezeshaji na kuboresha vyuo hasa vya ufundi stadi," alisema Dk Rweikiza.Lakini Dk Rweikiza alisema bajeti hiyo haikuitendea haki sekta ya kilimo kwa kuitengea bajeti ndogo huku serikali ikisisiza utekelezaji wa mkakati wake wa Kilimo Kwanza, ambao alisema haiwezekani ukafanikiwa kwa bajeti hiyo.

Kasoro nyingine aliyoibaini katika bajeti hiyo ni serikali kuamua kurudisha leseni za biashara jambo alilodai kuwa litajenga mazingira mabaya kwa wawekezaji hata kuwaogopesha, akifafanua kuwa inaweza kuwafukuza wale wa kigeni na kuona serikali kama haina msimamo kwa sera zake kwa kuwa awali ilifuta leseni hizo.

Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Humphrey Moshi pamoja na kuisifia bajeti hiyo kuwa inakwenda na wakati, lakini naye alisema ina changamoto kadhaa ikiwemo kilimo kutengewa bajeti ndogo isiyolingana na mkakati wa Kilimo Kwanza.

"Ni bajeti inayokwenda na wakati, imegusa maeneo mengi kwa kutazama hali ya sasa, lakini ina changamoto zake ya kwanza ni utekelezaji. Je, itatekelezwa?" Alisema Profesa MoshiAlisema changamoto nyingine ni bajeti ya maendeleo kutegemea wahisani na kusema kwamba jambo hilo ni hatari kwa taifa na kuishauri serikali itafute vyanzo vingine vya mapato kwa ajili ya maendeleo.

Pia alisema bajeti hiyo inakabiliwa na changamoto ya udhibiti wa kodi za wawekezaji katika serikali za mitaa unaoweza kuzalisha ulaji mpya kwa watendaji.Kuhusu adhabu za makosa ya barabarani iliyoongezwa kutoka Sh20,000 hadi Sh50,000, alishauri iongezwe kwa madereva wa mabasi na malori kwa kuwa husababisha madhara zaidi katika ajali.

Profesa huyo alishauri serikali idhibiti mfumuko wa bei na kuangalia jinsi ya kupunguza uagizaji wa bidhaa zisizo na umuhimu kutoka nje ya nchi.
 
Itakuwa poa sana ila kama hawatakuwa waangalifu watawanufaisha polisi na mahakimu uchwara
 
Nimesikia serikali itapunguza matumizi ikiwa ni pamoja na kupunguza safari za nje, sherehe, semina (elekezi?), maonesho, n.k. Mimi niko kwenye hili la sherehe; Mimi naona sherehe za kutimiza miaka 50 ya uhuru zimeishaanza yaani miezi sita kabla. Kuna kupunguza gharama kweli hapa?
 
Mi nataka niskie bajeti ivuli inasema inataka kuona malio na posho za watumishi wa umma zinaendana na uzito wa majukumu yao.

Jamni tutasemaje
Kilimo kwanza waati Afisa kilimo wa Mkoa anazidiwa mapato na meya wa jiji.?
Utapataje Elimu bora primary na sekondary wakti Afisa Elimu wa Mkoa na wilaya anazidiwa kipato na mbunge
Utakuwaje na ulinzi mzuri kama RPC anazidiwa kimapato na mwanasiasa.

Wanasiasa kamwe hawateleta mabadiliko. Wo ni chachu tu. Ni watendaji wanaotakiwa kuwa frontline ndo wataleta mabadiliko ya kweli. Wabunge piganieni watu sahihi wapate maslahi sahihi ikiwezekana hata kuwazidi.

Mkuu nadhani ni budget kivuli. Kama ni hivyo hivi budget kivuli ina maana gani? Mtu si anaweza akasema chochote ama kupendekeza chochote kwa kuwa hana pahala pa kuitekelezea hiyo budget ambapo ateweza kuulizwa kwamba ulisema hivi lakini mambo halisi ni haya? Nisaidie ili nijue umuhimu wa budget kivuli
 
ccm waje kusikiliza nini wakati posho zinaingia kama kawaida? na bajeti ishapita kwani wako wengi bungeni very simple
 
ccm waje kusikiliza nini wakati posho zinaingia kama kawaida? na bajeti ishapita kwani wako wengi bungeni very simple

Maswali mepesi-:

1.Wamelazimishwa kuomba kazi ya ubunge au kuteuliwa uwaziri?
2.Ukumbi wa Bunge hauwatoshi?
3.Hawajui majukumu yao?
4.Wana ajenda ya siri?
5.Wana udhuru?
 
Ndugu wadau! Niandikapo mada hii machozi yananitoka mtoto wa kiume. Jana Mh. Mkullo alitanga kiama kwa madereva wazembe na matajiri ambao hawatengenezi magari yao .
Hapa Mwanga leo saa 12.00 asubuhi polisi ambapo ni siku ya gulio la Mwanga Mjini Polisi wote wametoka wapo barabarani . zamani kila siku ya gulio ambapo hata yale magari yalio kuwa hayaingii mjini siku hiyo yanaingia kutokana na wananchi kufuata mahitaji muhimu ya wiki nzima. walikuwa wakitozwa Tsh 3000/= kama kinga ya kuendesha magari mabovu na kwa uzembe. Leo kulingana na Bajeti ya mkulo ambayo polisi hao wameanza kuitekeleza hata kama haijapitishwa na Bunge hesabu ni TSh 10,000 ukiwa mjeuri ni Tsh 50,000 bila risiti ya serikali.
Tutafika wadau PH02759J.JPG
 
Ndugu wadau! Niandikapo mada hii machozi yananitoka mtoto wa kiume. Jana Mh. Mkullo alitangaza kiama kwa madereva wazembe na matajiri ambao hawatengenezi magari yao .
Hapa Mwanga leo saa 12.00 asubuhi polisi ambapo ni siku ya gulio la Mwanga Mjini Polisi wote wametoka wapo barabarani . zamani kila siku ya gulio ambapo hata yale magari yalio kuwa hayaingii mjini siku hiyo yanaingia kutokana na wananchi kufuata mahitaji muhimu ya wiki nzima. walikuwa wakitozwa Tsh 3000/= kama kinga ya kuendesha magari mabovu na kwa uzembe. Leo kulingana na Bajeti ya mkulo ambayo polisi hao wameanza kuitekeleza hata kabla haijapitishwa na Bunge hesabu ni TSh 10,000 ukiwa mjeuri ni Tsh 50,000 bila risiti ya serikali.
Tutafika wadauView attachment 31692
pencil.png
 
Waliowengi ni wabunge wa chama cha magamba,ni vilaza wanachojua ni kupiga madawati na kushangilia kila linalosemwa na mbunge mwenzao,hawaoni umuhimu wa uwepo wao bungeni zaidi ni posho tu.:madgrin:
 
Simmekaba penati sasa iyo elimu bure itakujaje..? matumizi ya serikali tril 8 maendeleo tril 4 kuna maendeleo hapo kweli
Tehe teh teh......Kwani bajeti yenu lazima iwe trilion 12? inaweza kuwa trilion 18 si mnasema kuna vyanzo mbadala na matumizi yasiyo ya lazima? na mliahidi elimu bure mwaka wa kwanza wa utawala?
Huu ndiyo wakati muafaka mngetumwagia shule jinsi hii nchi inavyotakiwa iende,ningerudisha kadi yangu ya CCM.
 
b) Upungufu wa Nishati ya umeme:

Nchi yetu inakabiliwa na upungufu wa nishati ya umeme kutokana na kiwango kidogo cha uzalishaji usioendana na mahitaji. Kwa kuzingatia kuwa umeme una umuhimu wa kipekee katika kukuza uchumi wa nchi, Serikali itachukua hatua kadhaa za kukabiliana na upungufu huu, ikiwemo kukamilisha mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 100 Dar es Salaam na ule wa megawati 60 Mwanza;

Kuiwezesha TANESCO kupata mikopo kutoka taasisi za fedha za kimataifa kwa ajili ya kununulia mitambo ya uzalishaji na kuangalia upya namna ya kugawanya shughuli za Uzalishaji.

Usafirishaji na Usambazaji; kwa lengo la kuiachia TANESCO kujikita kwenye eneo ambalo ina uwezo nalo kiushindani na hivyo kuleta ufanisi katika sekta nzima ya umeme. Aidha, kutokana na kukamilishwa kwa sera, sheria na kanuni za ubia kati ya Serikali na sekta binafsi (PPP), Serikali itaandaa utaratibu wa kuhusisha sekta binafsi katika sekta ya umeme na inatarajiwa kwamba baadhi ya miradi ya uzalishaji umeme itatekelezwa kwa njia ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi.

Serikali imeshaanza majadiliano na wawekezaji katika uzalishaji wa umeme kwa ubia katika miradi ifuatayo; Mtwara MW 300, Mpanga MW 144, na miradi ya usafirishaji umeme wa kV 400 ya Morogoro-Tanga-Kilimanjaro-Arusha km 682 na upanuzi wa Gridi ya Kaskazini Magharibi kwa mikoa ya Kagera, Kigoma na Rukwa - km 1000. Serikali inawashauri wananchi kuanza kutumia vyanzo mbadala vya umeme wa jua, upepo na nishati inayotokana na biogesi pamoja na kutumia kwa uangalifu nishati ya umeme iliyopo.

WAKITEKELEZA HAYA WALAU KWA 0.75 TUNAWEZA ZUNGUMZA CHOCHOTE ILA SIASA ZIKIINGIA NDANI TUMEUMIA
.MPANGO WA MUDA MREFU WA UWEKEZAJI KWENYE NISHATI YA UMEME NDIO SULUHISHO LA KUDUMU REJEA POST YANGU NILIYO ITOA WIKI CHACHE JUU YA KIPAUMBELE KWENYE NISHATI YA UMEME

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...pewa-dhamana-na-wananchi-2015-iliangalie.html

KWA KWELI IMEFIKA KIPINDI SERIKALI ITILIE MKAZO HILI SUALA. PIA NAOMBA SASA WANASIASA KAENI KANDO KUBALINI KUSIKILIZA MAONI NA USHAURI WA WATALAAMU (TECHNICAL EXPERTS).

PIA IPENI UHURU TANESCO WA KIMAAMUZI ,MADENI YA SERIKALI NA TAASISI ZAKE ZOTE MNAYODAIWA NA TANESCO LIPENI .
 
"Kuhusu deni la taifa, Mkullo alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana, lilifikia dola 11,380.2 milioni za Marekani na kwamba, liliongezeka kwa dola 654.28 milioni ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2009. Mkullo alisema ongezeko hilo lilitokana na mikopo mipya ya ndani na nje yenye masharti nafuu kugharimia miradi mbalimbali ya maendeleo." Source Mwananchi la leo.

Deni la Taifa limekuwa likiongezeka kila kukicha na kwa sasa limefikia kiasi cha Tshs. Trilion 17.8, na hivyo kupelekea kila mtanzania kudaiwa kiasi cha Tshs. 445,000/= kwa wastani wa watanzania milioni alobain (40,000,000).

Serikali haionyeshi kushitushwa na hali hiyo na inazidi kutwisha mzigo mkubwa kizazi kijacho, cha watoto wetu na wajukuu zetu.

Safari za Mhe za Nje ya Nchi ziko pale pale kila kukicha, Mashangigi yananunuliwa tu na kuendelea kutumika, Mawazili na watendaji wengine kuendelea kukaa Mahotelini kila kukicha, Posho za Waheshimiwa zinazidi tu kuboreshwa kila kukicha, na yote ya haya, TRA nao wanaendelea tu kuandamwa na MADENI yaliyotokana na kesi mbalimbali ambazo zinawagalimu mabilioni ya Shilingi za Kitanzania na Mianya ya kodi inazidi kubuniwa kila kukicha, kila mtanzania anaona ni bora awe shujaa wa kutokulipa kodi kwani haoni faida yake hasa Mfanyabiashara, anaebaki kulipa kodi ni mtumishi mwema (Loyal employee) pekee ambae hana namna ya kukwepa.

Mkulo anasema Bajeti hii ni ya Matumaini, tuendelea kuwa na utulivu wetu na tuwe na matumain siku zote.

Hii ndio Bajeti ya Mkolo, Waziri wa Fedha!!
 
Ndugu wadau!
niandikapo habari hii machozi yananitoka mtoto wa kiume. Jana Waziri wa fedha katangaza bajeti mpya ambayo imeongeza faini kwa madereva wazembe na wale matajiri wasiotengeneza magari yao (magari mabovu). Kwa siku za Nyuma Polisi walijiundia kanuni yao hapa Mwanga kuwa siku ya Alhamisi ambapo kuna gulio kubwa la wiki huwa wanajikusanyia Tsh 3000 kwa kila gari na kwa Wazururaji wastaafu (waendesha Boda boda) Tsh 2000.
Leo mnamo saa 12.00 asubuhi hata kabla bunge halijaanza kuijadili bajeti hiyo mapai wetu hawa wakiongozwa na viongozi wao wote hapa mwanga (kasoro OCD ) wapo kwenye barabara zote zinazoingia mwanga wakikusanya pesa haramu za Rushwa zikiwa katika viwango vipya vya Tsh 5000 bodaboda na 10,000 kwa magari yote! Ukiwa jeuri kidogo 50,000 inakuhusu tena bila risiti ya serikali ukikomaa zaidi faini ya zamani lakini itajumuisha makosa 4 yaani Tsh 80,000/= Binafsi nimewapandishia na kuwakimbia kwa hiyo nipo mafichoni sasa. TUTAFIKA! Tanzania yenye neema tele inawezekana kila m2 atimize wajibu wake!:A S 100:
 
Back
Top Bottom