Bunge la bajeti 2024 limesusiwa na kudorora balaa!

Bunge la bajeti 2024 limesusiwa na kudorora balaa!

Sijui kama Watanzania wengi wanajua kuwepo kwa vikao vya bunge la bajeti vinavyoendelea Dodoma. Yaani kuanzia mitaani, mitandaoni, redioni, Kwenye Luninga na magazeti hakuna habari wala mijadala mizito inayoibuliwa kutokea bungeni, yaani kumepoa balaa.

Mahudhurio ya wabunge ni hafifu mno, michango ya wabunge ni duni mnoo, hotuba za bajeti zimepwaya kupitiliza, ni mwendo wa kucopy, kuCut na kuPaste bajeti zilizopita huku wakibadilisha tarakimu za pesa ya bajeti na kujazia blah blah fulani za kindezi, hakuna kipya au cha maana.

Na kuna taarifa nimesikia kuwa kuna wabunge kadhaa hawajui hata kama vikao vya bunge la bajeti vinaendelea Dodoma (japokuwa posho zote za vikao wanalipwa), na wabunge wengine wako Dodoma kupiga gambe na kuzagamuana tu mitaani, bungeni hawaingia ng'o
kinachoendelea dodoma ni vikao vya ccm,na wajumbe wenyewe pumzi ilishakata wamechoka kukalia kile kijiwe wako zao majimboni kujipitishapitisha kwa wadau na wapiga kura
 
Back
Top Bottom