Bunge la Chama kimoja tutegemee tena G55 mpya ikitokea?

Bunge la Chama kimoja tutegemee tena G55 mpya ikitokea?

Tanzania ina uzoefu wa kuwa na Bunge la chama kimoja, lkn pamoja na kuwa na bunge la chama kimoja kulikuwa na mijadala mikali na hoja nzito zilizojadiliwa ukiwamo ule wa kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika uliotokea kwenye miaka ya 1990 al maarufu kama G55.

Wabunge wa CCM wa wakati huo kina, Njelu Kasaka, Jenerali Ulimwengu, Philip Marmo na wengine, walikuwa ni watu waliojiamini waliojengwa kwenye chama na ambao walikuwa tayari hata kufukuzwa ndani ya chama.

Tofauti ya mabunge hayo ya nyuma na linalotarajiwa kuwa Bunge la sasa ni historia ya watakaounda kundi hilo.

Kwenye bunge la awamu iliyopita ukiwaondoa wabunge wa upinzani, kazi kubwa ya wabunge wa CCM ilikuwa ni kuitetea serikali, matusi ya akina Lusinde yalielekezwa kwa wapinzani, Spika alimalizia hasira zake kwa kuwafukuza wapinzani.

Kwenye bunge la awamu hii Serikali itakuwa inajitetea yenyewe, spika atakuwa anawafokea wanaCCM wenzake wabunge wa CCM watakuwa wanaihoji Serikali na kwa kufanya hivyo lazima kutatokea kupishana kati ya utawala na wabunge na kati ya serikali na baadhi ya wabunge wa CCM, baadhi yao wataonekana kama wasaliti wanaofanya kazi ya upinzani, na hapo ndipo tunaweza kupata kundi lingine kama la G55 ndani ya bunge la chama kimoja.

Wakati wa G55 zisingekuwa busara za Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kukemea CCM ingepasuka vipande viwili, safari hii bahati mbaya hatuna kiongozi wa kalba ya Nyerere, ukitokea mgawanyiko ndani ya Bunge la chama kimoja sioni mtu sahihi au kiongozi anayeweza kuwaunganisha pasipo kuwaumiza.
Hiyo haitakaa itokee bunge zimejaza malaya wa kisiasa yani ndio mzee,hawana lolote hao ubunge wamepata kwa nguvu ya meko.
Wathubutu kwa lipi labda
 
Nyerere alikuwa ana akili, sio kwamba hakuwajua kabla hao G55. Sasa hivi kabla hata hamjajulikana ni G55 mwingine atatekwa, mwingine kesi uhujumu uchumi, mwingine TRA watatua kwenye biashara yake n.k
 
Upinzani wa kweli upo ndani ya CCM kamanda
Tanzania ina uzoefu wa kuwa na Bunge la chama kimoja, lkn pamoja na kuwa na bunge la chama kimoja kulikuwa na mijadala mikali na hoja nzito zilizojadiliwa ukiwamo ule wa kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika uliotokea kwenye miaka ya 1990 al maarufu kama G55.

Wabunge wa CCM wa wakati huo kina, Njelu Kasaka, Jenerali Ulimwengu, Philip Marmo na wengine, walikuwa ni watu waliojiamini waliojengwa kwenye chama na ambao walikuwa tayari hata kufukuzwa ndani ya chama.

Tofauti ya mabunge hayo ya nyuma na linalotarajiwa kuwa Bunge la sasa ni historia ya watakaounda kundi hilo.

Kwenye bunge la awamu iliyopita ukiwaondoa wabunge wa upinzani, kazi kubwa ya wabunge wa CCM ilikuwa ni kuitetea serikali, matusi ya akina Lusinde yalielekezwa kwa wapinzani, Spika alimalizia hasira zake kwa kuwafukuza wapinzani.

Kwenye bunge la awamu hii Serikali itakuwa inajitetea yenyewe, spika atakuwa anawafokea wanaCCM wenzake wabunge wa CCM watakuwa wanaihoji Serikali na kwa kufanya hivyo lazima kutatokea kupishana kati ya utawala na wabunge na kati ya serikali na baadhi ya wabunge wa CCM, baadhi yao wataonekana kama wasaliti wanaofanya kazi ya upinzani, na hapo ndipo tunaweza kupata kundi lingine kama la G55 ndani ya bunge la chama kimoja.

Wakati wa G55 zisingekuwa busara za Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kukemea CCM ingepasuka vipande viwili, safari hii bahati mbaya hatuna kiongozi wa kalba ya Nyerere, ukitokea mgawanyiko ndani ya Bunge la chama kimoja sioni mtu sahihi au kiongozi anayeweza kuwaunganisha pasipo kuwaumiza.
 
Tanzania ina uzoefu wa kuwa na Bunge la chama kimoja, lkn pamoja na kuwa na bunge la chama kimoja kulikuwa na mijadala mikali na hoja nzito zilizojadiliwa ukiwamo ule wa kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika uliotokea kwenye miaka ya 1990 al maarufu kama G55.

Wabunge wa CCM wa wakati huo kina, Njelu Kasaka, Jenerali Ulimwengu, Philip Marmo na wengine, walikuwa ni watu waliojiamini waliojengwa kwenye chama na ambao walikuwa tayari hata kufukuzwa ndani ya chama.

Tofauti ya mabunge hayo ya nyuma na linalotarajiwa kuwa Bunge la sasa ni historia ya watakaounda kundi hilo.

Kwenye bunge la awamu iliyopita ukiwaondoa wabunge wa upinzani, kazi kubwa ya wabunge wa CCM ilikuwa ni kuitetea serikali, matusi ya akina Lusinde yalielekezwa kwa wapinzani, Spika alimalizia hasira zake kwa kuwafukuza wapinzani.

Kwenye bunge la awamu hii Serikali itakuwa inajitetea yenyewe, spika atakuwa anawafokea wanaCCM wenzake wabunge wa CCM watakuwa wanaihoji Serikali na kwa kufanya hivyo lazima kutatokea kupishana kati ya utawala na wabunge na kati ya serikali na baadhi ya wabunge wa CCM, baadhi yao wataonekana kama wasaliti wanaofanya kazi ya upinzani, na hapo ndipo tunaweza kupata kundi lingine kama la G55 ndani ya bunge la chama kimoja.

Wakati wa G55 zisingekuwa busara za Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kukemea CCM ingepasuka vipande viwili, safari hii bahati mbaya hatuna kiongozi wa kalba ya Nyerere, ukitokea mgawanyiko ndani ya Bunge la chama kimoja sioni mtu sahihi au kiongozi anayeweza kuwaunganisha pasipo kuwaumiza.
G55 kwa wabunge hawa wa sasa kina Kibajaji? Like seriously?

Hawa hawa ambao tumbo ndilo "central nervous system" yao?👇👇👇

20201109_160950.jpg
 
Hahaha haiwezi kutokea kwasababu wale wabunge wa wakati ule walichaguliwa.

Hawa wamepewa ubunge kwa HISANI ya Magufuli.

Hivyo ondoa fikra hizo kabisa, hawa hata kuuliza maswali watakuwa wanasubiria kupewa na kufundishwa namna ya kuuliza.

Wakikosea hata ubunge wana nyang'anywa na kufukuzwa uanachama.
 
Tanzania ina uzoefu wa kuwa na Bunge la chama kimoja, lkn pamoja na kuwa na bunge la chama kimoja kulikuwa na mijadala mikali na hoja nzito zilizojadiliwa ukiwamo ule wa kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika uliotokea kwenye miaka ya 1990 al maarufu kama G55.

Wabunge wa CCM wa wakati huo kina, Njelu Kasaka, Jenerali Ulimwengu, Philip Marmo na wengine, walikuwa ni watu waliojiamini waliojengwa kwenye chama na ambao walikuwa tayari hata kufukuzwa ndani ya chama.

Tofauti ya mabunge hayo ya nyuma na linalotarajiwa kuwa Bunge la sasa ni historia ya watakaounda kundi hilo.

Kwenye bunge la awamu iliyopita ukiwaondoa wabunge wa upinzani, kazi kubwa ya wabunge wa CCM ilikuwa ni kuitetea serikali, matusi ya akina Lusinde yalielekezwa kwa wapinzani, Spika alimalizia hasira zake kwa kuwafukuza wapinzani.

Kwenye bunge la awamu hii Serikali itakuwa inajitetea yenyewe, spika atakuwa anawafokea wanaCCM wenzake wabunge wa CCM watakuwa wanaihoji Serikali na kwa kufanya hivyo lazima kutatokea kupishana kati ya utawala na wabunge na kati ya serikali na baadhi ya wabunge wa CCM, baadhi yao wataonekana kama wasaliti wanaofanya kazi ya upinzani, na hapo ndipo tunaweza kupata kundi lingine kama la G55 ndani ya bunge la chama kimoja.

Wakati wa G55 zisingekuwa busara za Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kukemea CCM ingepasuka vipande viwili, safari hii bahati mbaya hatuna kiongozi wa kalba ya Nyerere, ukitokea mgawanyiko ndani ya Bunge la chama kimoja sioni mtu sahihi au kiongozi anayeweza kuwaunganisha pasipo kuwaumiza.
Rais Mwinyi ni mcha Mungu na khofu ya Mungu ndio maana kipindi chake alitowa ruksa.

Lakini kwa sasa wote tumenyooshwa kwa rula na Ndugai ndio yuko pale hakuna gunzi tena.

Spika iko bungeni lakini mic ipo Chamwino.

Tumekwisha
 
Sawa, nahitaji mifuko 100 ya cement huko kwenye duka la wanaCCM bei iko Je.
"Nashangaa napokea vimeseji vingine, Mhe rais nimejitahidi katika kipindi changu, kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa, niliona hili nilizungumze wakuu wa mikoa wakuu wa wilaya msiwe na wasiwasi, na inawezekana wala yasitokee mabadiliko."JPM

#DodomaKiapo
 
hakuna mwenye akili atakuwa na muda wa kufuatilia upuuzi wa bunge, tunawatakia maccm ngonjera njema, no one will be watching you, tutakuwa bize kupambana na kutafuta mkate wa kila siku
 
Nasikitika Jana ilikuwa bahati mbaya kwangu nikaangalia UTV walikuwa na kipindi wanamuhoji mjinga mmoja sijui anaitwa nani ukweli moyo wangu uliumia sana...kuona mtu anaedhaniwa ameelika anaongea ujinga
Niliona,wageni wote wawili walikuwa wanaongea vitu vya ajabu kabisa!
 
Bila mama kuwa Mwenyekiti wa ccm na kuvunja bunge Ili aanze fresh kuna Kazi maana kuna watu hawako tayari kuona Mzanzibar anakuwa Rais

Pili sharti mama atumie vyombo vya dola kuwazima baadhi au kuwafukuza uanachama wa ccm kabisa Ili wasimyumbishe
 
Tatizo hili bunge sio tu chama kimoja bali ni bunge la mtu moja ambae analicontrol kwa remote toka cha mwino
Kwahiyo ni vigumu kupata G55
Ulikuwa sahihi

Njelu Kasaka aanika alivyoongoza G-55 kudai Tanganyika​

Dar es Salaam. Mwaka 1993, Njelu Kasaka akiwa mbunge wa Chunya aliwasilisha bungeni hoja binafsi ya kutaka kuundwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano.
Miaka 26 baadaye, mwanasiasa huyo ameandika kitabu kueleza sababu za kufikia uamuzi huo.

“Mara nyingi nilipokutana na watu mbalimbali waliniuliza kutaka kujua mazingira yaliyokuwepo wakati wa mchakato na kabla ya mchakato wa Hoja ya Tanganyika maarufu kama G-55 kufika bungeni,” anaandika Kasaka katika shukrani zake mwanzoni mwa kitabu hicho kinachoitwa “Maisha, Siasa na Hoja ya Tanganyika”.

“Mimi ndiye niliyewasilisha hoja bungeni Agosti 23,1993. Na kila mara nilipotoa maelezo kwa watu walinishauri niandike kitabu.”

Katika kitabu hicho, Kasaka anaeleza jinsi alivyoitwa sehemu tofauti na viongozi wa juu wa Serikali kama Waziri Mkuu John Malecela, “viongozi wakubwa wa serikali ambao hawakutaka kujulikana” hadi Mwalimu Julius Nyerere alipoingilia kwa kumtuma Joseph Warioba kuwaambia kuwa anataka kukutana nao.

“Kusema kweli kilichokuwa kinamtesa Malecela si hoja ya Tanganyika, bali ni uamuzi wa Serikali yake kuiruhusu Zanzibar kujiunga na (Jumuiya ya Nchi za Kiislamu) OIC kinyume cha Katiba,” anasema Kasaka baada ya kueleza jinsi alivyomkatalia waziri huyo mkuu kuondoa hoja yake bungeni.

Pia anaeleza jinsi Samuel Sitta, ambaye alikuwa waziri wa sheria na katiba wa wakati huo, alivyoishauri serikali mbinu tatu za kuua hoja ya Tanganyika.
Chimbuko la hoja

Kasaka, ambaye Februari 2 alifikisha miaka 77, anaeleza kuwa mpango huo ulikuwa na wakati mgumu kuutekeleza wakati huo kutokana na nguvu ya Mwalimu Nyerere, ambaye licha ya kuachia urais aliendelea kuwa mwenyekiti wa CCM kwa miaka kadhaa.
“Mtu yeyote aliyejaribu kukosoa Muungano alioasisi yeye (Mwalimu) na Sheikh Abeid Amani Karume mwaka 1964 alihesabiwa kama ni mpinga Muungano na ni mtu anayetumiwa na maadui ili kuuvunja au kuusambaratisha,” anasema.

Anasema cha kushangaza alipothubutu kufanya hivyo, wabunge walimshangilia sana na mwisho wa mchango wake alipokea vikaratasi 112 vya pongezi za maandishi na kugundua kuwa wabunge walimshangilia si kwa sababu aliongea jambo walilolijua, bali kwa sababu ya ujasiri tu wa kuyasema matatizo ya Muungano huo hadharani na kwa ufasaha.

Mpango ulivyosukwa

Baada ya mchango huo, kundi la kwanza la wabunge wanane lilikutana naye nyumbani kwa mbunge wa Babati, Mateo Qaresi eneo la Upanga jijini Dar es Salaam Juni 13, 1993.
Anawataja baadhi ya wabunge hao kuwa ni William Mpiluka (Mufindi), Abdallah Nakuwa (Lindi Mjini), Arcado Ntagazwa (Kibondo), Lumuli Kasyupa (Kyela) na Jared Ghachocha (Ngara).

Anaeleza kuwa madhumuni ya mkutano huo ilikuwa kutengeneza mkakati wa namna ya kutekeleza wazo la kuunda Serikali ya Tanganyika na walikubaliana waunde kamati ya kusukuma mbele ajenda ya kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika.

“Mimi nilipewa jukumu la kuwa katibu na mratibu wa mchakato huo na Qaresi akawa mwenyekiti wa kamati,” anasema.

Kamati hiyo ilikuwa hatua ya kwanza ya utekelezaji wa hoja yao na hatua ya pili ilikuwa ni kuwashawishi wabunge waunge mkono pendekezo hilo, na tatu ilikuwa ni kulifikisha kwa Naibu Spika Pius Msekwa.

Bunge wakati huo lilikuwa linaongozwa na Spika Adam Sapi Mkwawa, lakini kutokana na matatizo ya kiafya, hakuwapo na uongozi ulikuwa chini ya Msekwa.
Kundi la G-55

Kasaka anasema baadaye kazi ya kushawishi wabunge ilianza na yeye alichapisha karatasi ambayo ilizungushwa kwa wabunge kuwataka wanaounga mkono hoja wajiandikishe na kusaini.

“Haikuchukua muda, wabunge 44 walijiorodhesha na kutia saini. Idadi hii ya wabunge ilichukuliwa ni ya kutosha kuruhusu kumjulisha naibu spika kuhusu kusudio letu, baada ya kutueleza kuwa ilikuwa inawezekana ilimradi tu tuzingatie matakwa ya Kanuni za Kudumu za Bunge,” anasema.

Msekwa aliitangaza hoja kwa waandishi wa habari na kuijulisha Serikali.
“Vyombo vya habari vilipotangaza, umma ukapata habari. Shauku ya wananchi kwa hoja ya wabunge ikawa kubwa sana ingawa Redio Tanzania haikutangaza, ilichapishwa katika vyombo binafsi na gazeti la Mfanyakazi,” anasema.

“Mahudhurio ya wananchi katika viwanja vya Karimjee yaliongezeka sana. Hatukujua kwamba suala la Muungano na hasa kurudishwa kwa Serikali ya Tanganyika lilikuwa na mvuto kiasi hicho.”

Baadaye idadi ikafikia 57, lakini kabla hajaiwasilisha wawili kati yao wakajitoa na kubaki 55.

Aliyeomba kujiondoa ni Donald Ksenha (Dodoma Mjini) na Dk C.C Magoti (Mbunge wa Taifa).

Anasema wakati hamasa ikiendelea, Serikali iliunda timu ya kujadiliana na wabunge iliyoongozwa na Sitta. Wajumbe wengine ni mawaziri Edward Lowassa, Anne Makinda na Mohamed Seif Khatib.

Anasema hatua ya awali ya Serikali ilikuwa kuwataka waachane na hoja hiyo na kuiondoa bungeni, pendekezo ambalo walilikataa licha ya kufanya vikao sita.

Alisema baada ya majadiliano walikubaliana G-55 irekebishe hoja yake kwa kutaka wananchi washirikishwe katika kubadili sera ya CCM ya Muungano wa serikali mbili, jambo walilolikubali.

Lakini jitihada za kutaka hoja ifutwe zikaendelea, huku serikali ikiimarisha timu yake kwa kumuongeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Damian Lubuva.

Ndipo baadaye walipobaini kuwa Sitta aliiandikia serikali mapendekezo matatu ya kuua hoja hiyo.

“Kwa kuwa hoja binafsi inahitaji kibali cha Spika kujadiliwa, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais ambane Spika asitoe kibali na hoja itakufa,” anasema Kasaka.
Mbinu ya pili ilikuwa ni hoja hiyo kupelekwa kwenye mkutano wa wabunge wa CCM ambako serikali itapata muda wa kueleza hatua ambazo itachukua kutatua matatizo ya Muungano, na wabunge wengi wataelewa “hivyo kutokuwa na haja ya kuendelea na hoja”.

Na mbinu ya mwisho ni kuruhusu hoja iwasilishwe bungeni na baadaye Serikali kwa kutumia kanuni za Bunge itafanya mabadiliko kwenye hoja ambayo yatataka hoja nzima iondolewe.

Hata hivyo, Kasaka na wenzake wakaendelea na msimamo wao na baadaye wakaitwa na Malecela kabla ya Mwalimu Nyerere kuwaita na kujadiliana nao.

Anasema Mwalimu Nyerere aliwasikiliza na kuelewa hoja zao kuwa zinatokana na Serikali ya Muungano kutotekeleza wajibu wake na kuwataka waibane ili ifanye kazi yake ipasavyo.

Lakini akawatahadharisha kuwa hoja yao itaua Muungano, akisema hata kama ameambiwa mama yake ni mchawi na dawa yake ni kumuua, hangekubali na kuwashauri wakatafakari.

Kasaka anaeleza jinsi walivyosimama imara hadi hoja yao iliposomwa bungeni na baadaye kupitishwa.

“Niliwasilisha hoja yangu kwa niaba ya kundi maarufu la wabunge la G-55 lililokuwa likiwakilisha wabunge zaidi ya 100, waliokuwa wamejipanga kuunga mkono,” anaandika Kasaka.

Kasaka anaeleza alianzisha hoja hiyo baada ya kuona mfumo wa serikali mbili haufai na kutaka Serikali iondokane nao mapema iwezekanavyo.

Anaeleza kuwa mfumo huo ulikuwa hautoi haki sawa kwa nchi shiriki.
Kasaka anawanukuu wananchi wa Zanzibar wakiushangaa mfumo huo kuwa ni wa ajabu ulimwenguni kwa kuwa “nchi moja haijapewa haki inayostahili na moja imependelewa zaidi kuliko nyingine”.

Anasema baadaye ndipo harakati za kukwamisha utekelezaji wa hoja hiyo ulipoanza.
Anasema Mwalimu Nyerere hakuridhishwa na hatua ya Bunge na katika mkutano wa wabunge wa CCM uliofanyika ukumbi wa Kilimani aliwashutumu Malecela na Horace Kolimba kwa kuruhusu suala hilo lifike bungeni, huku akimkingia kifua Rais Ali Hassan Mwinyi.
 
Back
Top Bottom