Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Hili limesemwa na wengine na limesemwa vizuri na Prof. Shivji kwamba Bunge la Katiba lina madaraka ya kuweza kufutilia mbali rasimu ya Katiba ya Tume ya Warioba ambayo kimsingi ni mahali pa kuanzia tu siyo mwisho. Kuna watu wanasema ati Bunge liko kwa ajili ya Kuboresha sijui wamepata wapi mawazo hayo; hayako kwenye sheria ya Katiba Mpya! Sheria ile - ambayo wengine tuliikosoa toka mwanzo - imelipa Bunge uwezo wa kufutia, kuongeza na hata kubadili rasimu ya Katiba ambayo ililetwa kwao na TUme ya Katiba chini ya Jaji Warioba.
Kwa vile madaraka ya Tume hiyo yamekoma, chombo pekee chenye madaraka ya kuandaa rasimu ya Katiba ambayo italetwa kwa wananchi kuulizwa ni Bunge la Katiba. Bunge la Katiba halitaleta rasimu ya Jaji Warioba bali rasimu yao ambayo wameiandaa kutokana na rasimu ya Warioba. Kama wajumbe wengi wanakubaliana na rasimu ya Warioba basi kitakacholetwa kwa wananchi kitafanana sana na ile; lakini kinyume chake ni kuwa Watanzania wanaweza kupigia kura rasimu ya Katiba tofauti.
Well.. habari ndiyo hiyo...