Bunge la Katiba Haliko Kwa Ajili ya Kuboresha Rasimu ya Kina Warioba!

Bunge la Katiba Haliko Kwa Ajili ya Kuboresha Rasimu ya Kina Warioba!

Nakubaliana na wewe .Nakumbuka mwezi April mwaka 2012 nilipinga composition ya Bunge la Katiba.Nadhani nilikua nikichangia kwenye mjadala ulioanzisha na tulikua wachache sana tuliopinga huu mchakato tangu Mwanzo.Miaka 2 baadae tuko hapa

Historia ya Kenya ipo njia kujirudia hapa Tanzania

Historia ya alliance ya chama tawala cha MMD na chama cha UPND dhidi ya hoja za Patriotic Front na wanaharakati pamoja na wananchi wa Zambia kwenye katiba inajirudia na chama tawala wakajichimbia shimo kwenye uchaguzi mkuu uliofuata Upinzani ukashinda

Hofu ya chama tawala ilikua kuogopa reforms za tume ya uchaguzi na pendekezo la mshindi wa urais kupata 50%+1 ya kura zote.

Sasa uchaguzi mkuu uliofuata 2011 upinzani ukashinda ingawa hawakufikisha 50% + 1 .Wangekua na katiba mpya wasingetangazwa washindi

Wananchi waliungana na upinzani kwa kuwa walijua chama tawala hakina nia thabiti ya kushiriki mchakato wa katiba mpya kwa maslahi ya wazambia wote.

CCM hapa hawajifunzi.Nasi tuendelee kuwakumbusha wananchi historia na upinzani tujipange kuonyesha misimamo hata kama tumeshafanya makosa

Nilisema hatuwezi kufanya mazungumzo na watu wasio na nia njema.Wengine wakanikemia kuwa katiba mpya eti haipatikani barabarani

Msimamo wangu ni kuwa wasiotaka kukaa mezani kwa nia njema tukutane nao barabarani kisha turudishane mezani tukiwa na maumivu sasa tujadiliane kwa nidhamu.

Mchakatoo wetu wa kupata KATIBA MPYA umekwendaa kilainii sana!!!
Hii ni kuonyesha kuwa WATANZANIA ni wastaarabu, wasiopenda malumbano, wenye upendo na uvumilivu mkubwaa wa KISIASA NA KIJAMIII.
 
Tumemtafasiri vibaya Prof Shivji maana ndiye aliyekuwa msitari wa mbele juu ya katiba inayotokana na maoni ya wananchi hata tukapata mchakato uliotumika. Sasa tatizo ni wapi, katika mchakato au ni katika matokeo? Ukweli ni huu, kama Bunge la Katiba litakuja na katiba yenye mabadiliko ya msingi au kwa kutupilia mbali Rasimu ya Kamati ya Katiba kama wengine wanavyosema, basi hela ya kodi ya wananchi itakuwa imetumika isivyo maana kitakachotokea katika uhalali wake ni kile kile sawa na katiba tuliyonayo sasa ambayo imekosolewa. Sababu kuu ya kuaandaa katiba mpya ni kwa sababu tuliyo nayo hikutoka kwa wananchi wenyewe, si kwa sababu tu ilikuwa mbaya bali tusiwe na katiba kwa matakwa ya kundi fulani au vyongozi fulani. Kama ni kwa sababu ya ubaya wa katiba ya sasa basi tungetumia njia ile ile kuiboresha. Cha msingi hapa ni kupata katiba halali na ili kupata katiba halali tukakubaliana mchakato ambao serikali iliridhika utakuja na katiba halali.
 
Hakuna tofauti kubwa ya mfumo uliotumiwa na tume ya walioba na huu wa bunge la sasa kupata maoni.tume ya walioba ilitumia sampling kupata maoni kwa maana haikuweza kuwafikia watanzania wote na baadaye kufanikisha kuwa na document ya kuanzia.

Bunge maalumu la katiba ni wawakilishi wa wananchi,taasisi na asasi zenye malengo yanayofanana,hivyo waliopo bungeni nao ni wawakilishi wa wananchi kupitia kura ama kwa nafasi mbalimbali walizokuwa nazo.Kwa ujumla tunasema ni wawakilishi wanaosimama kwa niaba ya wananchi bila kujali wana itikadi gani za siasa.

Inawezekana kabisa katika maeneo mengine tume ya Jaji Walioba haikuwa sahihi,ama sehemu nyingine kampeni za ushawishi zilikuwa kubwa na watu kuchangia bila utashi wao kwa maana ya kushawishiwa na makundi ya kisiasa,lakini pia inawezekana katika maeneo mengine tume ya jaji walioba ilikuwa sahihi kwa asilimia mia moja.Jaji walioba anastahili kupewa pongezi,kama kuna mapungufu ni ya kibinadamu kama binadamu yeyote yule.Sasa mjadala upo mezani,muda upo wa kutosha na hapo kikubwa ni kutofautisha kati ya hoja ya nguvu na nguvu ya hoja.

Tofauti za mitazamo zinazotengeneza magenge tofauti,lazima tukubali,lakini kikubwa zaidi ni kwa waheshimiwa wetu wabunge kujitaidi kujenga hoja ambazo hata mwenzako hakiwa na kichwa kigumu ama msimamo usiobadilika ambaye ameingia bungeni kwa kuapa kwamba piga huo msimamo wangu huu lazima upite itafikia hatua ataona aibu tu.

Hivyo unataka kutuambia bunge la katiba,muhimu kwa ni maoni yao eti kwa sababu ni wawakilishi wa wananchi,
hivyo mawzo yao ni sahihi kuliko maoni na mawzo yaliyotoka moja kwa moja kwa wananchi???
 
Katika hili la Katiba Mpya, wale wote tuliopinga Mchakato wa CCM/JK tutabaki kuwa sahihi. Napenda kutambua umakini na msimamo wa MMM kupitia makala kadhaa hapa JF na kwingineko.

Ukweli wa wazi ni kuwa haiwezekani papatikane katiba ya Taifa/Wananchi toka kwa hao mafisadi. IMPOSSIBLE.

Kosa kubwa la watu wengi ni "kuamini kwa nia njema" kuwa "the end would justify the means". Kwamba licha ya ubovu wa sheria na muundo mzima wa ule mchakato lakini somehow mwishoni tungepata Katiba NZURI (ya Wananchi).

Tunalazimisha kuona tunachoamini badala ya kuamini tukionacho.
 
Mchakatoo wetu wa kupata KATIBA MPYA umekwendaa kilainii sana!!!
Hii ni kuonyesha kuwa WATANZANIA ni wastaarabu, wasiopenda malumbano, wenye upendo na uvumilivu mkubwaa wa KISIASA NA KIJAMIII.

kiulaini kulinganisha na ugumu upi muliotegemea? hivi kumkuta mtu anajisaisia mlangoni kwako na wewe ukachekelea ndiyo ustaarabu huo? naamua kuwa upande wa wasio wastaarabu ili tupate mustakabali bora kwa taifa letu.
 
CHADEMA lazima wafahamu kuwa political monopoly ya upande wa pili wa Bunge kwa sasa imekuwa automatically dissolved baada ya Rais Kikwete kuteua wawakilishi 201 kutoka asasi ambazo siyo za kiserikali, makundi yenye mahitaji maalum nchini, Vyama vya siasa vyote vyenye usajiri wa kudumu, asasi za kidini na bila kusahamu wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuwa pia ni wajumbe wa Bunge la Katiba.

Kama CHADEMA wanataka kusimamia hoja zao kama CCM walivyojiandaa lazima wakubali kuwa karibu kabisa na haya makundi ya wajumbe niliowataja otherwise, hii hoja ya kusema 'tutakutana' kwenye majukwaa ya siasa nje ya Bunge la Katiba baada ya kujitoa haitakuwa na mashiko kwa wananchi kama makundi mengine yatakuwa upande wa hoja za CCM na hasa ikichukuliwa kuwa kuna wanaJf tayari wamebainisha kuwa asilimia 70 ni wajumbe waliokunywa maji ya bendera ya CCM.

Kuna hatari ya CHADEMA kuonekana ndiyo 'vichwa maji' kama watajiondoa kwenye mchakato huku makundi mengine yakibakia kuendelea na mchakato, kwa maana nyingine hoja zao zitakuwa zinapambana na hoja za wengi ambalo kwa nje wanaonekana wametoka nje ya vyama (CCM).

Hata hoja ya kusema wananchi wengi wametaka hiki au kile itakuwa ni kaput kama makundi mengine yataamua kukaa upande wa CCM kihoja ndani ya Bunge la Katiba.

CHADEMA must tread delicate path on the remaining process towards getting the new constitution.
 
Hili limesemwa na wengine na limesemwa vizuri na Prof. Shivji kwamba Bunge la Katiba lina madaraka ya kuweza kufutilia mbali rasimu ya Katiba ya Tume ya Warioba ambayo kimsingi ni mahali pa kuanzia tu siyo mwisho. Kuna watu wanasema ati Bunge liko kwa ajili ya Kuboresha sijui wamepata wapi mawazo hayo; hayako kwenye sheria ya Katiba Mpya! Sheria ile - ambayo wengine tuliikosoa toka mwanzo - imelipa Bunge uwezo wa kufutia, kuongeza na hata kubadili rasimu ya Katiba ambayo ililetwa kwao na TUme ya Katiba chini ya Jaji Warioba.

Kwa vile madaraka ya Tume hiyo yamekoma, chombo pekee chenye madaraka ya kuandaa rasimu ya Katiba ambayo italetwa kwa wananchi kuulizwa ni Bunge la Katiba. Bunge la Katiba halitaleta rasimu ya Jaji Warioba bali rasimu yao ambayo wameiandaa kutokana na rasimu ya Warioba. Kama wajumbe wengi wanakubaliana na rasimu ya Warioba basi kitakacholetwa kwa wananchi kitafanana sana na ile; lakini kinyume chake ni kuwa Watanzania wanaweza kupigia kura rasimu ya Katiba tofauti.

Well.. habari ndiyo hiyo...
na hasa kipengele cha muungano,muungano unaotakiwa ni serikali moja tu, yaani serikali moja na katiba moja.kusiwe na katiba ya Zanzibar wala Tanganyika kama kweli tunautaka muungano vinginevyo ni kuuvunja muungano,nawaomba wajumbe wote wa katibu wazigatie hayo
 
CHADEMA lazima wafahamu kuwa political monopoly ya upande wa pili wa Bunge kwa sasa imekuwa automatically dissolved baada ya Rais Kikwete kuteua wawakilishi 201 kutoka asasi ambazo siyo za kiserikali, makundi yenye mahitaji maalum nchini, Vyama vya siasa vyote vyenye usajiri wa kudumu, asasi za kidini na bila kusahamu wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuwa pia ni wajumbe wa Bunge la Katiba.

Kama CHADEMA wanataka kusimamia hoja zao kama CCM walivyojiandaa lazima wakubali kuwa karibu kabisa na haya makundi ya wajumbe niliowataja otherwise, hii hoja ya kusema 'tutakutana' kwenye majukwaa ya siasa nje ya Bunge la Katiba baada ya kujitoa haitakuwa na mashiko kwa wananchi kama makundi mengine yatakuwa upande wa hoja za CCM na hasa ikichukuliwa kuwa kuna wanaJf tayari wamebainisha kuwa asilimia 70 ni wajumbe waliokunywa maji ya bendera ya CCM.

Kuna hatari ya CHADEMA kuonekana ndiyo 'vichwa maji' kama watajiondoa kwenye mchakato huku makundi mengine yakibakia kuendelea na mchakato, kwa maana nyingine hoja zao zitakuwa zinapambana na hoja za wengi ambalo kwa nje wanaonekana wametoka nje ya vyama (CCM).

Hata hoja ya kusema wananchi wengi wametaka hiki au kile itakuwa ni kaput kama makundi mengine yataamua kukaa upande wa CCM kihoja ndani ya Bunge la Katiba.

CHADEMA must tread delicate path on the remaining process towards getting the new constitution.
nawaomba wabunge wa katibu hasa kutoka bara kwamba muungano uwe wa serikali moja na katiba moja,na kama akitokea mtu wa kusema serikali mbili au tatu huyo hatakuwa hakubaliani kwamba, sisi ni ndungu na ikishindikana ni bora kuuvunja muungano wenyewe kuliko kuvaa ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu
 
right on; nadhani mwanzoni watu walidandia wazo la "Katiba Mpya" bila kufikiria sana kwani wengi waliamini kile kilichoitwa "nia njema" ya Rais Kikwete.
Ikumbukwe kuwa mchakato huu haukuanzishwa na chama chochote cha siasa na hata kwenye CCM haukuanzia katika utaratibu wa vikao vya chama; ni kama Kikwete aliamka tu usiku mmoja na kuamua kuwapatia wananchi Katiba Mpya!
Wapinzani ambao ndio walikuwa na hoja hii walikumbatia pendekezo hilo wa furaha wakiamini wameshinda.. sasa miaka mitatu baadaye watu wanaanza kuona machungu.

Mwisho wa siku nadhani ama wataamua kujitoa when it is too late au watalazimika kushindwa kwa nguvu ya kura na kujikuta kuwa hawana uwezo wa kuleta mabadiliko mengine wao wenyewe.
Ni bora tungechelewa ili tuwe na mchakato mzuri na wenye kuzaa Katiba Bora kuliko kuwahi na kujikuta tunaburuzana na kubambikiziana Katiba mpya

Hapo ndipo watanzania wengi walipokosea kwa kutokujua genesis ya mabadiliko haya ya Katiba ya Tanzania, Ni kwamba Tanganyika Laws Society, Legal and Human Rights Centre kwa kushirikiana na Mchungaji Christopher Mtikila walifungua mashtaka dhidi ya Serikali ya Tanzania katika Mahakama ya haki za Binadamu ya Umoja wa Nchi za Afrika iliyoko mjini Arusha Tanzania.

Waziri Kombani na Jaji Werema kwa kutokujua nini hatma ya mashtaka hayo ndipo walipokurupuka kutoa majibu waliyotoa mara tu utawala wa Kikwete ulipoingia madarakani kwa awamu ya pili 2010. Kwa kuwa Serikali ya Tanzania ilijua kuwa hamna yoyote ya kupata ushindi dhidi ya mashtaka hayo ndipo ilipoanisha mchakato wa mabadiliko ya katiba kwa shingo upande. KAMA MTAKUMBUKA KWA MSHANGAO WA WENGI ETI CCM IKAJITIA PIA KUUNGA MKONO PENDEKEZO LA MGOMBE BINAFSI, ILE ILIKUWA NI DANGANYA TOTO WALIKIWSHA PIGWA BAO MAHAKAMA YA HAKI ZA BINADAMU YA AFRIKA.

Ni bora tungechelewa ili tuwe na mchakato mzuri na wenye kuzaa Katiba Bora kuliko kuwahi na kujikuta tunaburuzana na kubambikiziana Katiba mpya
[/QUOTE]
ALL IN ALL TUKIACHA MAMBO YA KISIASA, RASIMU YA KATIBA IMEJAA MAMBO MBALI MBALI YA MSINGI SANA KWA MWANANCHI MMOJA MMOJA, JAMII NA TAIFA HIVYO NI MAONI YANGU KUWA IT IS AN OVER STATEMENT KWA MWANAKIJIJI KUUPUUZA MCHAKATO HUU MOJA KWA MOJA.

HISTORIA YA MABADILIKO YA KIKATIBA YA TANZANIA INAONYESHA KUWA HAKI ZA BINADAMU ZILIINGIZWA KATIKA KATIBA KWA MARA YA KWANZA MWAKA 1984, MABADILIKO YA SASA HATA KAMA HAYATAACHIEVE MUCH KISIASA LAKINI YAPO MABADILIKO MAKUBWA YATAYOFANYIKA KWA MAISHA YA INDIVIDUL CITIZENS.

UTANGULIZI WA HUKUMU YA MTIKIILA. TLS NA LHRC "IN THE CONSOLIDATED MATTER OF
1.
TANGANYIKA LAW SOCIETY
2. THE LEGAL AND HUMA
N RIGHTS
CENTRE
V.
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
REVEREND CHRISTOPHER R. MTIKILA
V.
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
AFRICAN UNION
UNION AFRICAINE
UNIÃO AFRICANA
AFRICAN COURT ON HUMAN AND PEOPLES' RIGHTS
COUR AFRICAINE DES DROITS DE L'HOMME ET DES PEUPLES
APPLICATION
No. 00
9/2011
APPLICATION No.
011/2011

following judgment:
The Parties
1. The Tanganyika Law Society and The Legal and Human Rights
Centre ("the 1st Applicants) describe themselves as Non-Governmental
Organizations ("NGO's) with Observer Status before the African
Commission on Human and Peoples' Rights ("the Commission"). They
are both based in the United Republic of Tanzania. They state their
objectives as representing the interests of its members, the
4
administration of justice, and upholding and advising the Government
and the public on all legal matters, including human rights, rule of law
and good governance; and the promotion and protection of human and
peoples' rights, respectively.
2. Reverend Christopher R. Mtikila ("2nd Applicant"), is a national of
the United Republic of Tanzania. He brings his application in his
personal capacity, as a national of the Republic.
3. The Respondent is the United Republic of Tanzania and is cited
herein because the Applicants contend that it has ratified the African
Charter on Human and Peoples' Rights ("the Charter"), and also the
Protocol. Furthermore, the Respondent has made a declaration in terms
of Article 34(6) of the Protocol, accepting to be cited before this Court by
an individual or an NGO with Observer Status before the Commission.
On the prayers:
126. In Conclusion:

Having found the applications admissible and that the Court has
jurisdiction to consider the applications, the Court by majority finds:
1. In respect of the 1st Applicants the Court holds:
That the Respondent has violated Articles 2, 3, 10 and 13(1) of the
Charter .
2. In respect of the 2nd Applicant, the Court holds:
That the Respondent has violated Articles 2, 3, 10 and 13(1) of the
Charter.
3. The Respondent is directed to take constitutional, legislative and all
other necessary measures within a reasonable time to remedy the
violations found by the Court and to inform the Court of the measures
taken.
4. In accordance with Rule 63 of the Rules of Court, the Court grants
leave to the 2nd Applicant to file submissions on his request for
reparations within thirty (30) days hereof and the Respondent to reply
thereto within thirty (30) days of the receipt of the 2nd Applicant's
submissions.

Endelea kufuatilia hukumu hiyoi kupitia:
http://www.african-court.org/en/ima...-2011 Rev Christopher Mtikila v. Tanzania.pdf
 
WEll.. subirini mshangae.. si mlikubali mchakato... ndiyo hivyo... Bunge litafuta vipengele na uzuri ni kuwa watapiga kura na wengi watapewa!!!

Na ukweli bado unabaki kuwa aliyeteua alikuwa na maslahi yake na ni lazima yapitishwe kwenye bunge hili kwa kura. Hamshangai tu kuona uteuzi una maswali mengi juu ya makundi watu waliyoteuliwa? Mengi zaidi yataonekana hivi karibuni na posho lazima itaongezwa ili kuwaridhisha wajumbe wasije wakapiga kura kinyume na mteuaji
 
Ben, mchakato mzima toka mwanzo ulitengenezwa kuweza ukiangalia matakwa ya CCM. CCM watafanyia mabadiliko makubwa rasimu ya Warioba na watapiga kura na kura zitaamua nani anakubalika. Wakipitisha basi watakuja kwa wananchi ambako threshold ya kupitisha ni ndogo mno kuliko ya huko Bungeni...

Hayo ni mawazo yako na Ben, lakini sio lazima wabunge ''kama unavyowaita wabunge wa CCM'' wapinge maoni yote ya Jaji Warioba, tusipende sana kuongea na kutabiri na kufikiri kwamba mna akili za kugundua mawazo na hisia za watu wengine, Ngoja tusubiri tuone! tatizo lako MM,Ben nk ni wanaharakati na sio wanasiasa............naamini baada ya Bunge tutakutana JF!
 
Ni lini Chama tawala cha CCM kiliwahi kiliwahi kukubali kwa nia ya dhati utungwaji wa katiba mpya?
 
Ni lini Chama tawala cha CCM kiliwahi kiliwahi kukubali kwa nia ya dhati utungwaji wa katiba mpya?

Bwana mdogo kumbuka CCM ndio wako madarakani, sera na maoni yao kwa hakika ndio yanatawala nchi na hawalazimiki kwa namna yoyote ile kuchukuwa maoni ya upinzani? hivi wewe unaamini kwamba ni wananchi wote wanaamini sera za upinzani? Bunge la Katiba ni moja ya hatua muhimu kupata katiba mpya, Kumbuka mwaka jana Chadema walimuagiza Prof.Baregu ajitotoe kwenye Tume ya Katiba kwamba imejaa wanaCCM na hawakuamini ingeweza kuja na maoni wnayoyataka, Kwa uzalendo Prof.Baregu aliwakatalia kwa lugha nzuri tu kwamba ''Nchi ni bora kuliko chama'' baada ya rasimu kutoka Chadema wameiunga mkono kwa kiasi kikubwa na Kumsifia Jaji Warioba ambae waliamini anatekeleza mawazo ya CCM. Kwa ushahidi tu hata kwa sasa BAADHI YA WABUNGE WA CCM Mfano Kangi Lugora amejitokeza na kusema yeye anaunga mkono serikali 3, na wapo wengi tatizo hapa ni watu kuendekeza uchambuzi kanjanja kama wa Chadema kabla ya chaguzi mbalimbali kwamba wana 100% ya kushinda sababu wanakubalika, matokeo yakija kinyume watoa maelezo kwamba CCM ndio wameshindwa kwani wao wameongeza kura kulinganisha na 2010''.........NI BORA TUSUBIRI NINI KITATOKEA, TUWAACHIE WAJUMBE
 
Unaweza ukajiona uko sahihi lakini kinacholeta shida hapa ni kwamba CCM haiaminiki tena kutokana na historia yake ya wizi katika kura na mambo ya kifisadi. Na pia kutokana na viongozi wengi wa CCM kutokuwa tayari na mabadiliko ya katiba
 
Mimi nakubaliana na wewe maana ukiangalia uteuzi wa Rais uliegemea kupata watu watakaoongeza kura za kupitisha Katiba ya CCM. Mfano, sisi wana NGOs tulipendekeza majina ya wawakilishi wetu lakini tulishangaa kuona akina Kingunge na Kimiti wakiletwa Bungeni na Rais akitupilia mbali majina yetu labda Mama Magdalena pekee. Kwa kweli hii siyo haki hata kidogo.
 
Katika mambo ya amini usiamini hili ni moja wapo ,Bunge hili La Katiba ni janga la Taifa ,kama kunapotokea njaa ,mafuriko ,kimbunga ,tetemeko kubwa la ardhi basi ,mwaka huu Tanzania imekumbwa na balaa ambalo sio dogo.

Bunge hili la katiba ambalo wakuu walijisahau na kutaka kuionyesha dunia kuwa WaTANZANIA sasa wamekuwa na
wameamua kuzua Katiba mpya ambayo imewashirikisha wananchi ,wakaamua kurusha matangazo live ,aloo ni vioja mabishano yasio na kichwa wala miguu ,mara kura zimepigwa ,yote ni kuionyesha dunia kuwa Tz wamo katika kuitekeleza demokrasia kwa vitendo ,kufumba na kufumbua kura nyingi kuliko idadi wapigaji ,tayari ni aibu.

Haya usiku ule wakuu hawakulala wakilaumiana ilikuwaje ,kuna mmoja akahoji tv zilionyesha ? Akajibiwa kwa kizungu YES ? Akahoji nani katoa ruhusa ,hapo watu wakasita na kutazamana machoni ,mzee si unajua hatukutegemea kama kutatokea changamoto ,..mshavuruga kila kitu ,wekeni chungio halafu ndio muonyeshe sio mnakulupuka tu ,mmeona sasa ?

WaTanzania wenzangu ,haijulikani kama kutatolewa matangazo live ,ndio imetoka ,umebahatika kuona ulichoona,hii inatokana na kutojiamini kwa viongozi wetu ,hii inatokana na udhaifu wa viongozi wetu,wao kama viongozi wanaogopa nini kurusha matangazo haya ili wananchi wenye kufuatilia wawe na kihabarisho cha moja kwa moja toka kwenye ukumbi ,wananchi waone kinachoendelea ,waone kile walichokiwakilisha ,waone umahiri wa wajumbe. Mnafunga milango na hakuna muandishi ,hivi kundi fulani likiamua kutoka na kusema ya kusema ,pengine waseme mlichokitaka wananchi sicho kinachojadiliwa ,CCM wametoa rasimu ingine tofauti na ya Warioba iliyotokana na Tume ,mtasemaje ?

Hili ni janga ambalo lisiposhughulikiwa litazidi kuipeleka Tanzania pabaya na kuididimiza katika dimbwi la umasikini huku ni kurudishana nyuma ,kunahitajika kila kitu kuwa live ,mwenye hamu ya kutazama atatazama ,halafu hamuoni kuwa siku hizi kuna mitandano ,mawasiliano yamejaa kwenye nyanja nyingi ,kama mnaona mnaficha mtakuwa mnajidanganya ,tena mnajidanganya vibaya sana ,amueni kuonyesha mwenendo mzima wa vikao vya bunge hilo live,ili kupunguza uzushi.

Taifa la Tanzania linafaa kuombewa kutokana na janga hili ,tayari watu au wajumbe wameanza kudai hela za nyongeza ,hivi ndilo waliloliendea ,baada ya mwezi watadai zaidi maana watasema maisha yamepanda .

dalili za janga hili kuwa nene ni pale palipotokea hujuma za kura au tuseme tatizo la kuzidi kura ,mabishano yalikuwa ya ajabu kulikuwa ustaarabu unaanza kutoweka kila mmoja akijiona ni mkali wa kushauri.

Wananchi hatutaki kuhadithiwa tunahitaji matangazo live !Labda mtwambie gharama za kurusha matangazo ni kubwa ,hapo tutawaelewa.
 
Hili limesemwa na wengine na limesemwa vizuri na Prof. Shivji kwamba Bunge la Katiba lina madaraka ya kuweza kufutilia mbali rasimu ya Katiba ya Tume ya Warioba ambayo kimsingi ni mahali pa kuanzia tu siyo mwisho. Kuna watu wanasema ati Bunge liko kwa ajili ya Kuboresha sijui wamepata wapi mawazo hayo; hayako kwenye sheria ya Katiba Mpya! Sheria ile - ambayo wengine tuliikosoa toka mwanzo - imelipa Bunge uwezo wa kufutia, kuongeza na hata kubadili rasimu ya Katiba ambayo ililetwa kwao na TUme ya Katiba chini ya Jaji Warioba.

Kwa vile madaraka ya Tume hiyo yamekoma, chombo pekee chenye madaraka ya kuandaa rasimu ya Katiba ambayo italetwa kwa wananchi kuulizwa ni Bunge la Katiba. Bunge la Katiba halitaleta rasimu ya Jaji Warioba bali rasimu yao ambayo wameiandaa kutokana na rasimu ya Warioba. Kama wajumbe wengi wanakubaliana na rasimu ya Warioba basi kitakacholetwa kwa wananchi kitafanana sana na ile; lakini kinyume chake ni kuwa Watanzania wanaweza kupigia kura rasimu ya Katiba tofauti.

Well.. habari ndiyo hiyo...

Mwanakijiji, naomba tafsiri ya kifungu cha 25(2) cha sheria ya mabadiliko ya katiba.
 
nakubaliana na wewe .nakumbuka mwezi april mwaka 2012 nilipinga composition ya bunge la katiba.nadhani nilikua nikichangia kwenye mjadala ulioanzisha na tulikua wachache sana tuliopinga huu mchakato tangu mwanzo.miaka 2 baadae tuko hapa

historia ya kenya ipo njia kujirudia hapa tanzania

historia ya alliance ya chama tawala cha mmd na chama cha upnd dhidi ya hoja za patriotic front na wanaharakati pamoja na wananchi wa zambia kwenye katiba inajirudia na chama tawala wakajichimbia shimo kwenye uchaguzi mkuu uliofuata upinzani ukashinda

hofu ya chama tawala ilikua kuogopa reforms za tume ya uchaguzi na pendekezo la mshindi wa urais kupata 50%+1 ya kura zote.

Sasa uchaguzi mkuu uliofuata 2011 upinzani ukashinda ingawa hawakufikisha 50% + 1 .wangekua na katiba mpya wasingetangazwa washindi

wananchi waliungana na upinzani kwa kuwa walijua chama tawala hakina nia thabiti ya kushiriki mchakato wa katiba mpya kwa maslahi ya wazambia wote.

Ccm hapa hawajifunzi.nasi tuendelee kuwakumbusha wananchi historia na upinzani tujipange kuonyesha misimamo hata kama tumeshafanya makosa

nilisema hatuwezi kufanya mazungumzo na watu wasio na nia njema.wengine wakanikemia kuwa katiba mpya eti haipatikani barabarani

msimamo wangu ni kuwa wasiotaka kukaa mezani kwa nia njema tukutane nao barabarani kisha turudishane mezani tukiwa na maumivu sasa tujadiliane kwa nidhamu.

you are absolutely right - naona tunalekea huko huko kenya tusipoangalia vzuri. The reason is these people are not in our favor but rather their stomach na wealth. Wakivuruga hiyo katiba kweli atapokalika. Tunawasubiri.
 
Back
Top Bottom