right on! right on!
Ufafanuzi: Kwanza si kweli kuwa muda wote Bunge la Katiba ni juu ya Bunge la siku zote. Huwa hivyo hasa kama nchi inajisikia kuwa haijawahi kuwa na Bunge wala Katiba, kama wakati wa kuzaliwa nchi mpya. Mahali pengine Bunge la siku zote huwa juu ya Bunge la Katiba, hasa kama la siku zote limechaguliwa na wananchi wakati la Katiba limeteuliwa. Na ikiwa hivi, basi hata uamuzi wa mwisho huwa si wa lile la Katiba bali wa Bunge la siku zote, kabla ya Kura ya Maoni kama ipo. Wakati mwingine yana nguvu sawa ya kutunga sheria; yakitofautiana kwa majukumu tu. Lililo muhimu ni kuwa Baraza lolote la kutunga sheria, liwe na jina lolote lile, ndilo linaamua sheria iweje, ikiwemo sheria inayoitwa Katiba. Kwa hili Shivji yuko sahihi. Na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba vilevile ni sahihi kwa kuonyesha ukuu wa Bunge dhidi ya Tume ya Katiba. Warioba hayuko sahihi na anajua hivyo, ila anafanya siasa ili tusipojua tuyapitishe mapendekezo ya Tume kiulaini.