Bunge la Katiba Haliko Kwa Ajili ya Kuboresha Rasimu ya Kina Warioba!

right on! right on!

Ufafanuzi: Kwanza si kweli kuwa muda wote Bunge la Katiba ni juu ya Bunge la siku zote. Huwa hivyo hasa kama nchi inajisikia kuwa haijawahi kuwa na Bunge wala Katiba, kama wakati wa kuzaliwa nchi mpya. Mahali pengine Bunge la siku zote huwa juu ya Bunge la Katiba, hasa kama la siku zote limechaguliwa na wananchi wakati la Katiba limeteuliwa. Na ikiwa hivi, basi hata uamuzi wa mwisho huwa si wa lile la Katiba bali wa Bunge la siku zote, kabla ya Kura ya Maoni kama ipo. Wakati mwingine yana nguvu sawa ya kutunga sheria; yakitofautiana kwa majukumu tu. Lililo muhimu ni kuwa Baraza lolote la kutunga sheria, liwe na jina lolote lile, ndilo linaamua sheria iweje, ikiwemo sheria inayoitwa Katiba. Kwa hili Shivji yuko sahihi. Na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba vilevile ni sahihi kwa kuonyesha ukuu wa Bunge dhidi ya Tume ya Katiba. Warioba hayuko sahihi na anajua hivyo, ila anafanya siasa ili tusipojua tuyapitishe mapendekezo ya Tume kiulaini.
 
Pole sana. Serikali moja imefungwa na sheria. Huwezi kuijadili. Na ni kwa sababu moja tu. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lazima iwepo kwenye picha!

Kama imefungwa kwa hiyo mjadala ni mbili au tatu! Sheria hiyo imefunga pia kwamba kura za wananchi nazo ni kuchagua serikali mbili ama tatu? Kama mmefungwa hivyo na sheria rudini tushiriki kwenye kilimo, mvua zinanyesha sasa.

Kumbe tunatakiwa kuanza upya kwa wananchi wenyewe kuamua muundo wa muungano kupitia kura ya maoni kisha ndio tume ifanye kazi yake huku ikijua aina ya muungano tunaoutaka. Hii ya tume na bunge kutaka kutuletea aina ya muungano naiona batili. kumbe tunaweza kuanza upya!
 
Ufafanuzi: Kwanza si kweli kuwa muda wote Bunge la Katiba ni juu ya Bunge la siku zote. Huwa hivyo hasa kama nchi inajisikia kuwa haijawahi kuwa na Bunge wala Katiba, kama wakati wa kuzaliwa nchi mpya. Mahali pengine Bunge la siku zote huwa juu ya Bunge la Katiba, hasa kama la siku zote limechaguliwa na wananchi wakati la Katiba limeteuliwa. Na ikiwa hivi, basi hata uamuzi wa mwisho huwa si wa lile la Katiba bali wa Bunge la siku zote, kabla ya Kura ya Maoni kama ipo. Wakati mwingine yana nguvu sawa ya kutunga sheria; yakitofautiana kwa majukumu tu. Lililo muhimu ni kuwa Baraza lolote la kutunga sheria, liwe na jina lolote lile, ndilo linaamua sheria iweje, ikiwemo sheria inayoitwa Katiba. Kwa hili Shivji yuko sahihi. Na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba vilevile ni sahihi kwa kuonyesha ukuu wa Bunge dhidi ya Tume ya Katiba. Warioba hayuko sahihi na anajua hivyo, ila anafanya siasa ili tusipojua tuyapitishe mapendekezo ya Tume kiulaini.

Mkuu sijakupata vyeka unaposema Bunge la Katiba na Bunge la siku zote yapo sawa kwa kuwa yanatunga sheria. Lakini pia unasema hili Maalum linatunga sheria ambayo inaitwa Katiba. Kama ndivyo na unaikubali dhana ya Constitutional supremacy na kwamba sheria yoyote itakayotungwa na chombo chochote itakuwa batili kama itakinzana na Katiba (ambayo imetungwa na bunge maalumu) basi ukuu huu wa katiba unaipa ukuu pia Bunge la Katiba dhidi ya Bunge pa kawaida.
 
Ufafanuzi: Kwanza si kweli kuwa muda wote Bunge la Katiba ni juu ya Bunge la siku zote. Huwa hivyo hasa kama nchi inajisikia kuwa haijawahi kuwa na Bunge wala Katiba, kama wakati wa kuzaliwa nchi mpya. Mahali pengine Bunge la siku zote huwa juu ya Bunge la Katiba, hasa kama la siku zote limechaguliwa na wananchi wakati la Katiba limeteuliwa. Na ikiwa hivi, basi hata uamuzi wa mwisho huwa si wa lile la Katiba bali wa Bunge la siku zote, kabla ya Kura ya Maoni kama ipo. Wakati mwingine yana nguvu sawa ya kutunga sheria; yakitofautiana kwa majukumu tu. Lililo muhimu ni kuwa Baraza lolote la kutunga sheria, liwe na jina lolote lile, ndilo linaamua sheria iweje, ikiwemo sheria inayoitwa Katiba. Kwa hili Shivji yuko sahihi. Na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba vilevile ni sahihi kwa kuonyesha ukuu wa Bunge dhidi ya Tume ya Katiba. Warioba hayuko sahihi na anajua hivyo, ila anafanya siasa ili tusipojua tuyapitishe mapendekezo ya Tume kiulaini.

I am trying to make sense of what you wrote, but I am not getting it. What exactly did you want to say?
 
Najisikia Uchungu sana kua Sehemu ya Watanzania ambako kunafanyika udhalimu wa nmana hii,Kama ningelikua na uwezo ningemwomba Mungu ili kila Mjumbe asiye na nia njema ya upatikanaji wa katiba yenye Maslahi ya Wananchi akisimama tu kuongea na Ikibidi akose nguvu za kuongea kisha akae chini au ashindwe kabisa kusimama na kuongea,Ee Mungu fanikisha Ombi hili.. Amein!
 
Hoja yako unaweza kuigeuza upande wa pili vile vile; kama Bunge la Katiba halina uwezo ambalo naamini linalo - kwa mujibu wa sheria na mantiki - basi mapendekezo ya TUme ya Warioba yangekuwa ya mwisho na watu wangeenda kwenye kura ya maoni moja kwa moja. Ndio maana kilichotolewa na Warioba ni mapendekezo tu na mambo mengine ambayo yamo kwenye rasimu hayakutoka kabisa kwa wananchi yametoka kwa tume yenyewe! Bunge ndilo sasa lina wajibu wa kupima mapendekezo hayo na kuona kama watanzania wengi wanakubaliana nalo - wao wakiwa ni wawakilishi wa Watanzania hao.

Angalau kinadharia.

you soun like the vice president Dr. Ghalib Bilaal ambayer hata hivyo hoja maelezo yake yanayooenekana kuwa ni pacha na ya kwako yalijibiwa vizuri na Jaji Warioba kuwa wao hawakutunga lolote isipokuwa ni mitizamo na mahitaji ya weananchi waliokutana nao kwa mahojiano na ushahidi wa picha na video upo na wameukabidhi.
Kufuta rasimu ni kufuta mawazo na mahitaji ya wananchi.
Kuhusu aliyoyaongea Professor Shivji, mimi nahisi umemuelewa utakavyo na si alivyokusudia.
 
Hivi kweli unaamini rasimu imetokana na mawazo ya wananchi? Really? Bahati mbaya msimamo wangu haujatokana na kumsikia Shivji; kwanza sijamsoma alichosema zaidi ya kuona headings tu.
 
Hoja yako unaweza kuigeuza upande wa pili vile vile; kama Bunge la Katiba halina uwezo ambalo naamini linalo - kwa mujibu wa sheria na mantiki - basi mapendekezo ya TUme ya Warioba yangekuwa ya mwisho na watu wangeenda kwenye kura ya maoni moja kwa moja. Ndio maana kilichotolewa na Warioba ni mapendekezo tu na mambo mengine ambayo yamo kwenye rasimu hayakutoka kabisa kwa wananchi yametoka kwa tume yenyewe! Bunge ndilo sasa lina wajibu wa kupima mapendekezo hayo na kuona kama watanzania wengi wanakubaliana nalo - wao wakiwa ni wawakilishi wa Watanzania hao.

Angalau kinadharia.

MM,
Hapo kwenye bold kuna uthibitisho wowote au ni hisia tu? Hata kama ndivyo mimi bado naamini tume inawakilisha mawazo ya watanzania kwa kiwango cha angalau 90%. Tukifanya makosa Bungeni kitakachofanyika ni Bunge litajigeuza lenyewe bila kujua na kuwa Bunge la kuandika Katiba.
 
Of course, uthibitisho upo. Soma rasimu ya Katiba halafu soma matokeo ya maoni yaliyokusanywa na TUme ya Warioba...
 
Kwa kawaida Katiba huwa inatengenezwa na Bunge la Katiba lililochaguliwa na wananchi directly.

Je, Katiba yetu ya sasa tuliyonayo ndiyo inasema hivyo?

Tume yenyewe was not the representative of the people.

Hapa unamaanisha nini? Ulitaka tume nayo iwe na wajumbe wengi kama Bunge? Nini maana ya tume?

Kwa kawaida wajumbe wa Bunge la Katiba hawateuliwi. Pia wabunge wa bunge la kawaida hawawezi kuwa converted automatically kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba.

Una uhakika lakini? Katiba yetu ya sasa inasemaje kuhusu hili pia? Inasema hivi kama unavyosema wewe? Tafadhali naomba ufafanuzi wako, it appears wewe ndiyo unataka kunichanganya zaidi maana kama uko sawa basi inaonyesha hakuna tulichofanya kwa kufuata Katiba yetu ya sasa tangu mwanzo mwanzo wa mchakato huu
 
Kitu kikubwa inakiona kuwa ni lazima kutakuwa na kubadilishwa kwa vipengele kibao hasa madaraka ya rais na muungano hivyo wengi watajiuliza mengi kwa CCm
 
Ndg. Mwanakijiji,

Mimi si Mwanasheria lakini ni msomaji mzuri na makini wa nyaraka mbalimbali. Mzee Shivji na wewe mko sahihi sana. Sitaki kuchangia huko, ila nataka kuweka sawa jambo moja kidogo hapo kwenye post yako, kwamba; Bunge la Katiba halitozalisha 'Rasimu ya Katiba' tena, bali kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za JMT ya Mwaka 2013, kifungu cha 25 (1), Bunge la Katiba litazalisha kitu kingine kabisa kinachoitwa 'Katiba inayopendekezwa'. Hii si lazima ifanane na ile ya Jaji Warioba na wenzake, hii ni zao la mijadala na maridhiano na hatimaye maazimio ya Bunge hili. Na hii ndiyo itapata uhalali wake kutoka kwa wananchi kupitia kura zao za ndiyo ama hapana. Kura zitapigwa kwa mujibu wa utaratibu unaopewa masharti na sheria ya kura za maoni ya mwaka 2013.

Wakatabahu,
HK.

Hii tafsiri ni potufu na hata wale wataalamu wa sheria waliokuwa wanajadili jambo hili pale ITV wamepinga na wamesema wazi kuwa bunge la katiba halina mamlaka ya kuweza kuja na rasimu mpya.

Hata katika hali ya kawaida tu ile rasimu ni maoni ya wananchi hivyo bunge la katiba linaweza kuyaboresha tu na si kuyabadilisha.

Katika hili Mzee MWANAKIjiji amepotoka sana na anachotetea ni kuchakachua maoni ya wananchi!
 
Last edited by a moderator:
Una uhakika lakini? Katiba yetu ya sasa inasemaje kuhusu hili pia? Inasema hivi kama unavyosema wewe? Tafadhali naomba ufafanuzi wako, it appears wewe ndiyo unataka kunichanganya zaidi maana kama uko sawa basi inaonyesha hakuna tulichofanya kwa kufuata Katiba yetu ya sasa tangu mwanzo mwanzo wa mchakato huu

Nikusaidie hapa kidogo; Katiba yetu ya sasa haina utaratibu wa kuandika Katiba Mpya. Ina utaratibu wa kufanyia marekebisho Katiba ya sasa chini ya Ibara ya 98. Ndio maana wengine tulisema kuwa ukiondoa matatizo mengine yote ya mchakato huu kimsingi mchakato huu ni haramu kutoka ulipofikiriwa! Unaisigida Katiba ya sasa na kuifanya haina maana. Huwezi kupata uhalali wa Kikwete kuanzisha hili dubwasha chini ya Katiba ya sasa; hana madaraka hayo na Wabunge waliopitisha sheria ya kusimamia mchakato huu huku wakiwa ni watu waliokula kiapo kulinda Katiba sasa ingekuwa tuna namna ya kuwafunga kamba na kuwakokota huku tunawacharaza viboko kuwarudishia senses zao ingetupasa kufanya hivyo.
 
Hata katika hali ya kawaida tu ile rasimu ni maoni ya wananchi hivyo bunge la katiba linaweza kuyaboresha tu na si kuyabadilisha.

Hii si kweli; hakuna mahali popote ambapo Bunge la Katiba linatakiwa "kuboresha"! Ingekuwa hivyo lingeitwa Bunge la Kuboresha Katiba! Kazi ya Bunge la Katiba ni kutunga Katiba na wanaanzia kwenye rasimu ya Tume ya Katiba. Kwa makosa watu wanafikiria TUme ya Warioba iko juu ya Bunge la Katiba na hivyo rasimu yake ni Lazima ifuatwe. La hasha, Bunge la Katiba chini ya Kifungu cha Sheria ya Katiba Mpya 25(1) ndilo lenye mamlaka ya hatimaye kuandika Katiba Itakayopendekezwa kwa wananchi. Ili wafanye hivyo wamepewa pa kuanzia - rasimu ya Tume ya Warioba.
 
Kitu kikubwa inakiona kuwa ni lazima kutakuwa na kubadilishwa kwa vipengele kibao hasa madaraka ya rais na muungano hivyo wengi watajiuliza mengi kwa CCm

Hili si tatizo kwani ndivyo sheria inavyotaka na ndivyo utaratibu uliokubaliwa. Kama walio wengi Bungeni wataamua kufanyia marekebisho vipengele vyovyote vya rasimu na ikaitwa kura na wakashinda basi vipengele hivyo vitakuwa katika Katiba Inayopendekezwa. Kama wananchi hawatakubaliana nayo basi wataikataa kwenye kura ya maoni.
 
Na ikiwa itatokea watafanya kubadili maoni ya rasimu ya katiba kutoka kwenye tume ya Warioba ambayo yametokana na wananchi halafu wakaweka madudu yasiyo na chembe ya utaifa bali vyama vyao kwenye kura ya maoni lazima tuiteme, NI HERI KUWA NA PENGO KULIKO KUWA NA JINO BOVU LITAKALOKUSUMBUA USIKU NA MCHANA KWA MAUMIVU

Ndg unatoa wapi UJACRI huo? waTZ ni walex2! Wenye uelewa hawaendi kupiga KURA wanabaki hom kutoa POVU,,! mpaka hapo sahau kuipiga chini kwenye KURA ya Maon
 
Na ukweli bado unabaki kuwa aliyeteua alikuwa na maslahi yake na ni lazima yapitishwe kwenye bunge hili kwa kura. Hamshangai tu kuona uteuzi una maswali mengi juu ya makundi watu waliyoteuliwa? Mengi zaidi yataonekana hivi karibuni na posho lazima itaongezwa ili kuwaridhisha wajumbe wasije wakapiga kura kinyume na mteuaji

Jambo hili limemgombanisha sana T,LISU na JK wa2 tukamuona LISU hana ADABU kupingana na RAIS matokeo yake ndo haya na bado tutayaona mengi2!
 
Pole sana. Serikali moja imefungwa na sheria. Huwezi kuijadili. Na ni kwa sababu moja tu. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lazima iwepo kwenye picha!

Km nilazima Serikali ya Mapinduzi iwepo Nikwanini pia TANGANYIKA icwepo! kwanini nyie watu wa CCM mnatufanya km Watt wadogo,,!
 
Back
Top Bottom