Mkuu
Bongolander,
Hoja yangu kwamba serikali tatu zitatatua mgogoro wa muungano ipo based on the following background:
*Muungano wa 1964 ulilenga serikali ngapi? Jibu ni tatu;
*Je nini kilitokea? Uchakachauji kwa vile serikali ya TANU na baadae CCM gave priority to control "people" kuliko to control "territory", utamadanu ambao bado unaendelea leo.
*Je, iwapo serikali tatu zingetekelezwa from the get go, muungano ungekumbwa na migogoro? Jibu ni ndio lakini not absolute stability kwani hakuna muungano duniani (federal or unitary wenye absolute stability). Suala la msingi ni kwamba grievances za wazanzibari zisingekuwa kubwa kama zile zilizoanzia miaka 30 iliyopita chini ya Jumbe. Walichokuwa wanadai ni simply "serikali tatu".
*Je, kuirudisha Tanganyika baada ya matukio ya zanzibar ya kikatiba aliyojadili
Nguruvi3 hapo juu kutakuwa ni suluhisho la muungano? Jibu ni kwamba kwa vile tume ya warioba ilielekezwa kuja na mfumo wa kulinda na kuboresha muungano, hapakuwa na option zaidi ya serikali tatu kwani source ya grievances za wazanzibari ni lost of autonomy and right to self determination, vitu ambavyo viliheshimiwa ndani ya mkataba wa muungano kabla ya sarakasi za uchakachuaji kuanza.
Mengi yameshafanyika znz (rejea hoja za
Nguruvi3 hapo juu) na hii ni baada ya CCM kupuuza vilio vya wazanzibari for over 30 years kwamba tuheshimu mkataba wa muungano. Wazanzibari walifanikiwa kurudisha uzanzibari kupitia katiba yao ya kwanza tangia mapinduzi kuelekea 1980s (sikumbuki tarehe kamili) kwani bila ya kushtuka mapema, zanzibar ingefanywa kuwa Tanzania Visiwani for good kama vile Tanganyika ilivyofanywa kuwa Tanzania Bara kupitia sheria namba 22 ya serikali ya 1965.
Mkuu, hivyo ndivyo serikali moja ingewezekana kwa kulazimishwa na ccm, sio kwa matakwa ya wananchi; all in all, wa kulaumu kwa yote kuanzia mgogoro wa muungano hadi hatua za kikatiba zanzibar 2010 ni CCM (Dodoma), sio wazanzibari. Na kwa vile CCM imeshaharibu kwa kulazimisha mfumo kwa wananchi, na kwa vile zanzibar wamesha respond kupitia katiba yao ya 2010, inachotakiwa ni watanganyika pia kufanya hivyo kupitia katiba yao ya Tanganyika kama tume ya warioba inavyopendekeza. Baada ya hapo sasa tutarudi kwenye meza ya majadiliano as two sovereign entities ambapo umma utaamua iwapo tunautaka muungano na uwe wa aina gani. Ni dhahiri kwamba wananchi wengi toka pande zote watataka muungano uendelee lakini unaohusisha masuala kadhaa tu kuwa ni ya ushirikiano hence serikali tatu kama mkataba wa 1964 ulivyoweka wazi. Kwa maana nyingine, the contentious issues kwa pande zote za muungano hazitakuwa juu ya uwepo wa muungano bali muungano katika masuala gani.
Mkuu
Bongolander, pengine nikuulize, hizo sarakasi za serikali tatu zitarukwa na nani, wananchi au watawala?
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums