Hili limesemwa na wengine na limesemwa vizuri na Prof. Shivji kwamba Bunge la Katiba lina madaraka ya kuweza kufutilia mbali rasimu ya Katiba ya Tume ya Warioba ambayo kimsingi ni mahali pa kuanzia tu siyo mwisho. Kuna watu wanasema ati Bunge liko kwa ajili ya Kuboresha sijui wamepata wapi mawazo hayo; hayako kwenye sheria ya Katiba Mpya! Sheria ile - ambayo wengine tuliikosoa toka mwanzo - imelipa Bunge uwezo wa kufutia, kuongeza na hata kubadili rasimu ya Katiba ambayo ililetwa kwao na TUme ya Katiba chini ya Jaji Warioba.
Kwa vile madaraka ya Tume hiyo yamekoma, chombo pekee chenye madaraka ya kuandaa rasimu ya Katiba ambayo italetwa kwa wananchi kuulizwa ni Bunge la Katiba. Bunge la Katiba halitaleta rasimu ya Jaji Warioba bali rasimu yao ambayo wameiandaa kutokana na rasimu ya Warioba. Kama wajumbe wengi wanakubaliana na rasimu ya Warioba basi kitakacholetwa kwa wananchi kitafanana sana na ile; lakini kinyume chake ni kuwa Watanzania wanaweza kupigia kura rasimu ya Katiba tofauti.
Well.. habari ndiyo hiyo...
Mzee Mwanakijiji, kwanza asante kwa hii!. Naomba nikiri sasa nimeanza tena kumuona Mzee Mwakijiji yulee niliyemfahamu wakati nilipojiunga JF!, yule Mzee Mwanakijiji wa KLH News!, Mzee Mwakijiji wa "Cheche za Fikra!", ndio huyu Mwanakijiji wa leo!, ambaye amekuja na ukweli halisi as it is, not as it ought to be!, no matter ni mchungu kiasi gani kumeza, kilichopakuliwa ndicho hiki, watu wameze, wateme ni shauri yao ukweli huu ndio utasimama!.
Nilipo waambia , [h=3]
Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele![/h]ulinibeza sana humu! sasa unaelekea kuukubali ukweli huu mchungu!, na maandalizi ya kuukubali ule ukweli wangu mwingine mchungu kabisa kuwa 2015 ni CCM tena!, utafuatia!. Uzuri wa ukweli, huwa unasimama no matter what!.
Namalizia kwa ule ule msisitizo wangu kwenye ile mada tuliyobishana sana na Mkuu Mzee Mwanakijiji, kuwa "Japo Watanzania walitaka "Katiba Bora!", lakini kitakachopatikana kwa mchakato huu ni "Bora Katiba!" nikasema "maji ukiisha yavulia nguo!", kwa misingi ya "if you can't get what you want (Katiba Bora", then take what you get "Bora Katiba" kwa msingi wa na "moja shika sii kumi nenda rudi!", kuliko kukosa yote tukarudia katiba ya zamani, nikawasisitiza watu humu, tukubali matokeo na kwenye kura ya maoni, tuipigie kura ya ndio hii "Katiba Mpya!".
Pasco.