Nani atakubaliana nawe katika hoja yako? Wewe unaona ni vyema kuliteka Bunge Maalum la Katiba kwa siku ya pili sasa kujadili jambo la kura tu? Kwamba iwe ya siri au ya wazi? Iko wazi kabisa kuwa kura zote zinazotoa hatma ya jambo fulani hupigwa kwa siri. Inategemewa kuwa kura inayozungumzwa sasa katika Bunge Maalum la Katiba itatumika hasa katika kupitisha Ibara za Rasimu huko Dodoma. Yafaa iwe ya siri.
Waonaji wameshaona.Kuwa kura iwe ya siri. Na ndivyo ilivyo. Uwazi uwepo lakini usiwe katika kura ya kutoa mustakabali wa jambo fulani muhimu kama hili la Katiba mpya. Prof. Tibaijuka,nakuheshimu sana. Lakikini kaika hili uliteleza. Ni muda wako kuomba nafasi ya kuchangia na kujirudi.