Bunge la Kenya kuanza mijadala kwa Kiswahili

Waterloo

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Posts
25,356
Reaction score
38,922
Nimeona kwenye azam TV habari usiku huu wabunge wakenya wakipelekeshana kwenye mijadala ya bunge kwa lugha ya kiswahili imekuwa kama comedy ni vituko hakuna mfano.lakini msipate hofu mtazoea tuu. Naona nguvu ya Rais magufuli kulazimisha matumizi ya kiswahili inavuka mipaka ya nchi sasa.

Hongereni wakenya tukienzi kiswahili.
 
Tuwekee video tucheke
 
Mijadala kwenye bunge la Kenya imekuwa ikifanywa kwa lugha ya kiswahili na kiingereza pia, kwa pamoja, tangu tupate Uhuru. Lugha zote mbili ni lugha rasmi bungeni. Hii ilikuwa 2017. Naona wanakwaya wamesahau asili ya kiswahili ni wapi. Sijui bunge la Tz likilazimishwa kutumia kiingereza hata kwa lisaa limoja itakuwaje. Kuelewa lugha zaidi ya moja au mbili ni 'advantage' moja kubwa mno. Alafu hata kiswahili cha baadhi ya wabunge Tz ni kibovu kupindukia. 'r'/'l', 'dhi'/zi huwa zinawakanganya sana.
 

Watanzania wengi wana matatizo ya kimatamshi huku Wakenya wengi wana matatizo ya kisarufi. Huenda Kiswahili ndiyo lugha inayoongewa ovyo kabisa na wazungumzaji wake. Wazanzibari ndiyo wanaongea Kiswahili kizuri, wengine wababaishaji.
 

Kuwa Serious bro[emoji2][emoji2]
Toka uhuru ndio wanaongea Kiswahili kibovu namna hii? Halafu Kingereza Cha Wakenya ni Kibovu pia,
Infact Wakenya hawajui Kingereza wala Kiswahili, Confused people
 
Wakenya hawajui kiswahili wala English vyote hivyo ni mzigo kwao, wanaweza kujitutumua kama wapo vizuri kwenye English ila akiongea hata mzungu mwenye lugha yake hatafurahi sababu anaongea na accent ya kilugha
 
Wakenya hawajui kiswahili wala English vyote hivyo ni mzigo kwao, wanaweza kujitutumua kama wapo vizuri kwenye English ila akiongea hata mzungu mwenye lugha yake hatafurahi sababu anaongea na accent ya kilugha
Heheee,Lia bas
 
Watanzania wengi wana matatizo ya kimatamshi huku Wakenya wengi wana matatizo ya kisarufi. Huenda Kiswahili ndiyo lugha inayoongewa ovyo kabisa na wazungumzaji wake. Wazanzibari ndiyo wanaongea Kiswahili kizuri, wengine wababaishaji.
Kuna demu wa kikenya nachati nae hapa aisee ni kichefu chefu maandishi yake utafikiri ni bata anaharisha, sio kingereza sio kiswahili ngoja nitascreenshot mida mida 😬😬😬
Kwenye sa anaweka za πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hajui kuruka space full kubananisha maneno.
 
Mimi siamini hebu nipe mawasiliano yake nithibitishe.
 
Hahaha aisee
We hujawahi elewa wakenya ni watu wa aina gani hao wabunge sio eti hawajui Kiswahili lakini nikujifanya tu ,tangu nianze kumsikiliza Duale sijawahi kusikia amezungumza Kiswahili kisomali lakini juzi amezungumza Kiswahili cha kwao bahali yake,sio eti hajui alichokua anafanya ,sasa mbunge atasema vipi kua walete sheng bungeni eti hajui Kiswahili ilihali lugha aliokutana nayo baada ya kuzaliwa ni Kiswahili ,Kwa shule amesoma Kiswahili halafu ajue shengi ambayo umeanza tu juzi na asijue Kiswahili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…