Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Serikali imesema itaendelea kuwalea na kuwapatia matunzo wazee wasiojiweza ambao hawana familia na ndugu wa kuwatunza kupitia makazi ya wazee na wasiojiweza 13 inayoyamiliki.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mwanaidi Ali Khamis wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi aliyetaka kujua ni lini Serikali itatunga sheria itakayojumuisha mtoto kuwatunza wazazi wake wakizeeka.
Pia amesema Serikali itaendelea kufanya tathmini wakati wa utekelezaji wa Sera ya Wazee iliyoboreshwa ambayo ina tamko la kuwataka watoto kuwajibika kuwatunza wazazi na endapo kutakuwa na umuhimu wa kuwepo na sheria maalumu kwa wazee wakati wa utekelezaji basi wizara itaanzisha mchakato huo.