Bunge La Kumi Na Tatu, Mkutano Wa Pili, Kikao Cha Nne, Tarehe 30 Januari, 2026

Bunge La Kumi Na Tatu, Mkutano Wa Pili, Kikao Cha Nne, Tarehe 30 Januari, 2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Baadhi ya wabunge wakiwasili bungeni jijini Dodoma leo Januari 30, 2026 kushiriki kikao cha nne cha mkutano wa pili wa Bunge la 13.

Katika shughuli za leo, kama ilivyo kawaida, kutakuwa na kipindi cha maswali na majibu ambapo wabunge watauliza maswali na kujibiwa na serikali.

Aidha, Bunge litaendelea kujadili hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 13, iliyobainisha mwelekeo wa serikali yake.


Serikali imesema inaendelea na hatua mbalimbali za uundwaji wa Baraza la Taifa la Vijana.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka ametoa kauli hiyo bungeni leo Januari 30,2026 alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ndanda, Faraji Nandala aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuanzisha Baraza la Taifa la Vijana.

“Baraza la Vijana la Taifa linaundwa kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Taifa la Vijana Sura ya 441. Sheria inaunda Baraza hilo kuanzia ngazi ya Kata hadi ngazi ya Taifa.

“Kwa mujibu wa sheria hii Waziri mwenye dhamana ya Maendeleo ya Vijana nchini amepewa mamlaka ya kutunga Kanuni chini ya kifungu cha 27(1) kwa lengo la kurahisisha utekelezaji wa sheria husika.

"Kanuni hizi pia tayari zimeshatungwa na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali Na. 348 la tarehe 15 Septemba, 2017.

“Zoezi la uundwaji wa baraza lilisitishwa ili kutoa nafasi ya kukamilishwa kwa mapitio ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ambayo imekamilika na kuzinduliwa mwezi Agosti, 2024.

“Baada ya kukamilika kwa mapitio ya sera hiyo, serikali inaendelea na hatua mbalimbali za uundwaji wa baraza ikiwa ni pamoja na kuomba ushauri na mwongozo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuanza kutekeleza sheria hiyo kwa mafanikio,” amesema Waziri Nanauka.
 
Screenshot_20260130-103758~2.png
 
Hatuna Bunge wala Serikali halali! Wahuni wameua wananchi kisha wakajitangaza Rais na wabunge. Unapokuwa na waovu kwenye uongozi, ni laana kubwa!!
 
Back
Top Bottom