Bunge la Marekani laidhinisha kitita cha $ billion 60 kwa Ukraine

Bunge la Marekani laidhinisha kitita cha $ billion 60 kwa Ukraine

Baada ya mkwamo wa muda mrefu uliochangiwa na baadhi ya wabunge wa Marekani wenye mahaba na Putin hatimaye bunge la Marekani limepitisha kifurushi kipya cha $billion 60 kwa vita vya Ukraine.

Msaada huu mpya kwa Ukraine unajiri baada ya mwaka mmoja na nusu tangu bunge lililokuwa likiongozwa na Democrats kupitisha msaada kwa vita vya Ukraine.

Ushindi wa Republicans mwaka jana katika bunge la Marekani uliweka mkwamo wa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kwa Ukraine kupata msaada kutoka Marekani.

Hata hivyo spika mpya wa bunge la Marekani ameamua kuwapuuza wabunge wachache wa MAGA lakini wenye sauti kubwa ndani ya chama cha Republicans waliosababisha mkwamo huo na kuamua kupeleka miswada mitatu ya usalama katika bunge iliyopewa jina la "21st Century Peace through Strength Act" ambayo imepitishwa kwa wingi wa kura.
Tangu vita ianze Ukrain keshatafuna USD Bil 300 za msaada? sasa hiyo USD 60 cha mtoto. TABULELE@
 
Huo mswaada wa kuipa Ukraine msaada ungeanzaje kujadiliwa iwapo usingependekezwa na serikali ya Baden?
Wabunge wa Congress na Senate ndio wenye mamlaka ya kuwasilisha miswaada katika mabunge yao. Hiyo miswaada inaweza kuwa ni kutokana na mapendekezo ya Rais, lobbyists au makundi mbalimbali. Hata bajeti ya serikali huwa inaanza kuandaliwa na bunge kisha anapelekewa Rais kutoa maoni yake.
 
Fanya research kidogo kabla ya kujibu....

Plus hao Pentagon hawako kwenye biashara ya kuisaidia Ukraine, wako kwenye biashara ya kuuza silaha za kampuni zao.

View attachment 2969856
Nifanye research ya nini? Research ya kwamba Ukraine wanatumia Patriot missiles kutungulia drones??

Halafu Pentagon haina makampuni yake, makampuni yote ya silaha Marekani ni kampuni binafsi, pia hakuna shida makampuni ya silaha kunufaika kwa mauzo ya silaha zake pale panapokuwa na vita, hasa wanapopeleka silaha upande ambao unahesabika ni washirika wao na values sawa kama Ukraine.
 
Hawatashinda hiyo vita
Wanaweza wasishinde lakini wakapata amani ya muda mrefu baada ya vita kwa sababu gharama itakayoingia Urusi katika hii vita itapunguza sana kama sio kuacha kabisa michezo yake ya kulazimisha serikali vibaraka nchi jirani na kudokoa maeneo ya majirani zake kidogo kidogo.

Pia ni mkakati mpana wa Ukraine kuingia kwenye mazungumzo ya amani ikiwa katika "strong position" ambapo Russia haitaipuuza.
 
Values ni mambo ya midomoni, war is about making money, pengine hujawahi kusikia Pentagon revolving door
 
I guess Nyerere made a lot of money when he fought Iddi Amin.
Now you are comparing a communist Nyerere with the Capitalists of the West.... From next week angalia stock prices za Raytheon na wengine. It's about the Benjamins.
 
Wanaweza wasishinde lakini wakapata amani ya muda mrefu baada ya vita kwa sababu gharama itakayoingia Urusi katika hii vita itapunguza sana kama sio kuacha kabisa michezo yake ya kulazimisha serikali vibaraka nchi jirani na kudokoa maeneo ya majirani zake kidogo kidogo.

Pia ni mkakati mpana wa Ukraine kuingia kwenye mazungumzo ya amani ikiwa katika "strong position" ambapo Russia haitaipuuza.

Kumbe kurazimisha ukibaraka kwenye nchi zingine ni vibaya?
Sasa mbona hiyo ndo sera kuu ya hao wamagharibi ambao upo hapa unawashadidia maana hata misaada hiyo yote kwa Ukraine ni kumlinda kibaraka wao asianguke na kuingia kibaraka wa Urusi.
Hayo yote uliyo yasema yangekuwa na mantiki mpaka sasa Urusi angetakiwa awe ameshindwa vita.

Kadri vita inavyo dumu muda mrefu inaiathiri vibaya Ukraine ,Urusi ina athirika lakini sio kwa kiwango kikubwa sana kama Ukraine.
 
Back
Top Bottom