Bunge la Mei 26, 2025: Wizara ya Mambo ya Ndani yaomba zaidi ya Trilioni 2/- kwa Bajeti ya Mwaka 2025/26

Bunge la Mei 26, 2025: Wizara ya Mambo ya Ndani yaomba zaidi ya Trilioni 2/- kwa Bajeti ya Mwaka 2025/26

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

View: https://www.youtube.com/watch?v=cRKUyHuLjzA


WhatsApp Image 2025-05-26 at 09.27.36_ab96adbe.jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent L. Bashungwa (Mb) akiwasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma, ambapo atawasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, leo tarehe 26 Mei 2025.

Hali ya Usalama Nchini

"Kwa kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025 Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limewezesha kudumisha usalama, amani na utulivu, na hivyo kuifanya nchi yetu kuendelea kuwa kivutio kwa wawekezaji, wageni na watalii."

"Katika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025 makosa makubwa ya jinai yalitolewa taarifa katika vituo vya Polisi yalikuwa makosa 40,022 ikilinganishwa na makosa 43, 147 yaliyotolewa taarifa katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2023/24. Hivyo, makosa 3,125 yamepungua sawa na asilimia 7.2"

"Magari ya kisasa ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya doria na misako."

"Julai 2024 hadi Aprili, 2025, matukio ya ajali 1,322 yameripotiwa ikilinganishwa na matukio 1,463 yaliyoripotiwa mwaka"

"Shilingi bilioni 30 zimetengwa kwa ajili ya mafunzo kwa watendaji ikiwemo kutoa elimu kuhusu namna ya kushughulikia ukatili wa kijinsia na unyanyasaji kwa wanawake na watoto."

"Shilingi bilioni 30 zimetengwa kwa ajili ya mafunzo kwa watendaji ikiwemo kutoa elimu kuhusu namna ya kushughulikia ukatili wa kijinsia na unyanyasaji kwa wanawake na watoto."

"Serikali imewezesha Jeshi la Magereza kutumia nishati safi katika magereza yote 129, kwa ajili ya kupikia chakula cha wafungwa na mahabusu magerezani. Utekelezaji huu ni sawa na asilimia 100 ya lengo ya kupeleka nishati safi kwa magereza yote nchini."

"Shirika linatekeleza majukumu yake ya msingi ya uzalishaji ikiwemo shughuli za viwanda vidogo, ujenzi na uchimbaji madini. Uzalishaji huo umewezesha ukusanyaji wa mapato ghafi ya jumla ya Shilingi bilioni 16.22"

"Serikali imewezesha Jeshi la Magereza kutumia nishati safi katika magereza yote 129, kwa ajili ya kupikia chakula cha wafungwa na mahabusu magerezani. Utekelezaji huu ni sawa na asilimia 100 ya lengo."

"Julai 2024 hadi Aprili 2025 jumla ya wageni 1,839,342 waliingia ikilinganishwa na wageni 1,695,350 waliongia katika kipindi kama hicho mwaka 2023/24. Aidha, jumla ya wageni 1,698,420 walitoka nchini ikilinganishwa na wageni 1,579,925 waliotoka mwaka 2023/24."

"Julai 2024 hadi Aprili 2025, jumla ya Pasipoti 114,448 zimetolewa ikilinganishwa na Pasipoti 141,762 zilizotolewa kipindi kama hicho mwaka 2023/24."

"Katika mwaka 2025/26 Shilingi bilioni 3.24 zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na usajili na utambuzi wa watu 2,389,290 wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea."

"Elimu kwa umma imetolewa kuhusu taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili kuwezesha wananchi kufanya marekebisho ya taarifa binafsi katika mfumo wa NIDA na kuwezesha jumla ya wananchi 12,121 kurekebisha taarifa zao"

"NIDA pia imesajili na kutambua Watanzania 1,300 wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) katika nchi za Comoro, Marekani, Ubelgiji, Uingereza, Uholanzi na Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu (UAE)."

"Makadirio ya Ukusanyaji wa Maduhuli kwa Mwaka 2025/26, Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2025/26 Wizara imepanga kukusanya jumla ya Shilingi 428,000,000,000, ikiwa ni ongezeko la Shilingi 24,700,000,000 kutoka Shilingi 403,300,000,000 mwaka 2024/25, sawa na asilimia 6.12. Miongoni mwa mikakati iliyowekwa na Wizara kufikia lengo hilo ni kuimarisha huduma za Uhamiaji Mtandao (e-immigration); kuimarisha matumizi..."

"Maombi ya Fedha kwa Mwaka 2025/26, Mheshimiwa Spika, bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeongezeka kutoka Shilingi trilioni 1.71 mwaka 2024/25 hadi kufikia Shilingi trilioni 2.06 mwaka 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 21. Kwa niaba ya Viongozi na Watumishi wote wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, namshukuru kwa dhati Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa kuiongezea bajeti Wizara ambayo itaboresha utekelezaji wa majukumu ya Wizara."

"Mheshimiwa Spika, naomba Bunge lako liidhinishe Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka 2025/26 ya jumla ya Shilingi 2,067,161,717,000. Kati ya fedha hizo, Shilingi 701,703,184,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo, Shilingi 950,318,192,000 ni Mishahara na Shilingi 415,140,341,000 ni fedha za Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha za maendeleo, Shilingi 388,610,747,000 ni fedha za ndani na Shilingi 26,529,594,000 ni fedha za nje."
 

Attachments

Asisahau hela ya kuwalipa watekaji (poliz) maana wanatupiga mwingi
 
Back
Top Bottom