Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia Itifaki ya Biashara ya Huduma ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) ya Mwaka 2012.
Itifaki hiyo imeridhiwa Agosti 31, 2023 Bungeni jijini Dodoma na Wabunge wa Bunge hilo ambao walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali yaliyolenga kuhakikisha Tanzania inanufaika na fursa za kibiashara zinazotokana na utekelezaji wa Itifaki hiyo inayolenga kukuza ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi wananchama.
Akiwasilisha Azimio la Bunge, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuridhia kwa itifaki hiyo, kutaiwezesha Tanzania kunufaika na ushirikiano katika biashara ya huduma katika kukuza biashara ya bidhaa na kutekeleza malengo mapana ya SADC ya kukuza uchumi na kuondoa umaskini.
Aidha, aliongeza kuwa Itifaki hiyo itasaidia kuongezeka kwa uzalishaji kwa wakulima, ajira na thamani ya mazao ya kilimo kupitia kuimarika kwa huduma wezeshi za kifedha, usafirishaji na mawasiliano pamoja na uhawilishaji wa teknolojia kutoka nje ya nchi (technology transfer) kutokana na uwekezaji utakaofanyika nchini
Pia, amesema Itifaki hiyo itasaidia kupatikana kwa soko kubwa la bidhaa na huduma lenye idadi ya watu takribani milioni 360 waliopo SADC pamoja na kuongezeka kwa tija na ubora kwa bidhaa na huduma za Tanzania kutokana na kuongezeka kwa ushindani na hivyo kupelekea kupungua kwa gharama za kupata huduma.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda , Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Mariam Ditopile (Mb.) alisema Kamati inaishauri Serikali kuhakikisha changamoto mbalimbali za kibiashara zinaondolewa ikiwemo usafiri, ulinzi wa raia na mali zao pamoja na kutumia fursa mbalimbali kama ukuzaji wa sekta ya utalii kwa kujenga hoteli zenye viwango vinavyotakiwa na kufundisha kiswahili katika nchi hizo ili kukitangaza na kuongeza ajira kwa walimu nchini.