Mateso chakubanga
JF-Expert Member
- May 10, 2021
- 587
- 800
Bunge la Ubelgiji limepitisha muswaada wa kuiwekea Rwanda vikwazo vya kiuchumi na kijeshi kutokana na mchango wake wa machafuko mashariki mwa DRC.
Azimio hilo lenye kurasa 11 liliwasilishwa na mbunge wa ubelgiji mwenye asili ya DRC mutyebere Ngoi kutoka chama cha kishoshalisti limeungwa mkono na wabunge wote wa bunge la Ubelgiji.
Katika azimio hilo lililojulikana kama 76 limetoa wito kwa serikali ya Ubelgiji kusitishwa kwa misaada yote ya kijeshi, kiuchumi na ushirikiano, pia limeadhimia kufutwa kwa mkataba wa ushirikiano kati ya Rwanda na Ubelgiji uliosainiwa tarehe 19.2.2024 limetoa wito pia kusitisha uuzaji wa bidhaa zote za mafuta kutoka Ubelgiji na kusitishwa kabisa kwa mashirikiano ya kijeshi na kufuta misaada yote kwa serikali ya Rwanda.
Soma: Umoja wa Ulaya (EU) waitaka Rwanda kutoa vikosi vyake Mashariki mwa Congo huku ikipanga kupitia upya makubaliano ya malighafi na nchi hiyo