Bunge la Ubelgiji lapitisha azimio la kuiwekea Rwanda vikwazo

Mateso chakubanga

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2021
Posts
587
Reaction score
800
Bunge la Ubelgiji limepitisha muswaada wa kuiwekea Rwanda vikwazo vya kiuchumi na kijeshi kutokana na mchango wake wa machafuko mashariki mwa DRC.

Azimio hilo lenye kurasa 11 liliwasilishwa na mbunge wa ubelgiji mwenye asili ya DRC mutyebere Ngoi kutoka chama cha kishoshalisti limeungwa mkono na wabunge wote wa bunge la Ubelgiji.

Katika azimio hilo lililojulikana kama 76 limetoa wito kwa serikali ya Ubelgiji kusitishwa kwa misaada yote ya kijeshi, kiuchumi na ushirikiano, pia limeadhimia kufutwa kwa mkataba wa ushirikiano kati ya Rwanda na Ubelgiji uliosainiwa tarehe 19.2.2024 limetoa wito pia kusitisha uuzaji wa bidhaa zote za mafuta kutoka Ubelgiji na kusitishwa kabisa kwa mashirikiano ya kijeshi na kufuta misaada yote kwa serikali ya Rwanda.

Soma: Umoja wa Ulaya (EU) waitaka Rwanda kutoa vikosi vyake Mashariki mwa Congo huku ikipanga kupitia upya makubaliano ya malighafi na nchi hiyo
 
Binadamu wana roho za ajabu sana, Rwanda ina utulivu, uchumi una stawi lakini Kiongozi wa Nchi anahangaika na wanao mkosoa na kuwamaliza, ana sababisha nchi majirani wakose Amani.
Yaani ni kama kila analofanya bado halimpi utulivu wa nafsi.
Hivi Kiongozi aoni maisha ya watu yanavyo haribika kwasababu yake!!
 
Kagame apelekwe mahakama ya kimataifa huyo muuaji mkuu
 
Kagame apelekwe mahakama ya kimataifa huyo muuaji mkuu
Huyu hana muda watamnyakua yeye na watoto wake wanafanya mambo ya hivyo mnoo hasa dogo Ian hawampendi kwa udhalilishaji wake na kuhusika kwake kutekwa watu Gisenyi na Kigali kazi anayo bwana mkubwa au mkulungwa aje ajifiche kimanzichana au hata Msangangongele huku kwa wandengereko na wazaramo
 
Ni jambo jema sana
 
Safi, huyo dikteta inatakiwa akamatwe afungwe cheni aburuzwe kwenye gari hadi afe
 
Yaani waAfrica wenyewe tumemshindwa PK mpaka wazungu watusaidie, Tishekedi naye ameshindwa kulinda mipaka ya nchi yake sasa anaziweka rehani rasirimali za Taifa lake.
 
Kaka,,,ukiona JIRANI YAKO anaanzisha migogoro ya mipaka,ardhi inamwiita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…