Bunge la Ulaya kutuamulia Tanzania na Uganda nini Cha kufanya ni kutudharau?

Bunge la Ulaya kutuamulia Tanzania na Uganda nini Cha kufanya ni kutudharau?

Bunge la Ulaya limesema kuwa ni marufuku Tanzania na Uganda kujenga bomba la mafuta na gesi kutoka Uganda kwenda Tanga Tanzania kwakuwa mradi unachafua mazingira na unadhulumu watu linakopita ni sawa? Maswali hapa ni:

1. Wazungu wanapata wapi nguvu hii ya kutuamulia sisi nini kizuri na nini kibaya? Je , ni hii tabia yetu ya ombaomba na utegemezi kwao ndio inayotuponza? Je, historia ya utumwa inatuponza, wanatudharau kutuona kama wajinga, watumwa wao?

2. Ni kweli mradi huu unaharibu mazingira kwa kiasi hicho kuliko wao wanavyochafua? Viwanda vyao havichafui mazingira?

3. Ni kweli watu wetu wanaopitiwa na mradi hawakupata stahiki zao sawasawa na thamani ya mradi wenyewe (value for money)? Wamedhulumiwa na wajanja? Nchi zao hazikujengwa na watumwa na Mali za kupora wengine?

4. Nini hatima ya uhusiano wetu na nchi za Magharibi, wakoloni wetu wa zamani? Ndio ukoloni unarudi tena? Wanawaza kurudi tena?
Mungu wabariki Wazungu
 
Kwanza tujiulize lile la TAZAMA limetuletea athari gani tokea lijengwe na limetuletea faida ipi mpaka sasa..
Za kuambiwa changanya na zako, huu mradi watu tumewekeza humo kwa muda mrefu mpaka tumefilisika kwa sasa kisa danadana hizo za hao mabeberu, nawasihi viongozi wasirudi nyuma wafanye kama ilivyokuwa kwa bwawa la Nyerere.

Tusipangiane vya kufanya wao huko wanasapoti vita Ukraine je wamepima madhara wanayopata Ukraine na Russia?..

Wakati ni huu wakuwa na msimamo thabiti hakuna haja ya kuwasikiliza kama wao wanavyotaka, walianzia kwenye mabenki yasitoe pesa za kuendesha huu mradi bado watu wakafanya mipango mingine wanaona mradi unaanza wanaibuka na hoja zile zile za mwanzo tena, shenzi zao hao.
mradi huu kuna nchi jirani zinatuchongea ili ukwame.
 
Sio kila katazo linaubaya wake, viongozi wa kiafrika pia sio wa kuamini saana hasa katika mikataba mikubwa, wazungu wanajaribu kutustua kiustaraabu ipo shida na wao wameiona sasa sisi kazi yetu ni kuitafuta hiyo shida na kuifanyia kazi. Wao wanao uzoefu wa kutosha katika hili na ni jukumu letu kusikiliza na kuchukua taadhari.

Wazungu wanajua kabisa shida zako wewe ni mzigo kwao, lazima wazuie hizo shida, mfano nyie wenyewe toka mwaka 2015 mligoma kuajiri na vijana wenu wakakosa ajira na mliambiwa hilo ni boom litakuja kubutuka tu, sasa leo mmezalisha panya road mnajidai kabisa hamjui wametoka wapi???

Pasi na shaka bomba likipita linaharibu mazingira na wewe unajua, sema ni kawaida kupima athari na kulinganisha na faida mara nyingi tunafunika kombe kwa faida kiduchu, babu zenu walikuwa wanabadilisha almasi kwa shanga na walikuwa na majibu kama haya ya kwako matokeo yake unayaona.

Stahiki manake nini kama mtu akilipwa fidia anapaswa kuwa bora zaidi ya walipomkuta sababu mradi unaopita ni biashara ya kudumu, kwa nini wasiwape hisa wakawa sehemu ya umiliki???? unaambiwa umekaa vibaya unakasirika nini sasa kaa vizuri basi.
Well Noted....
 
Unahamisha goli hapa kwa kusema mavitu mengi mno, bomba linafanyika leo dunia umebadilika sana, Elizabeth sio malkia tena na hayupo. angalia leo kwanza. Nani kakuzuia usiharibu watu wamekustua kuweka records sawa mbeleni usije sema hukuambiwa
too late, tunayo miradi mingi mno ya hivi; TAZAMA, SGR, Bwawa, Songas, Buzwagi, Merelani, daraja la wami, kigamboni, nk. Hawa ni wapuuzi tu, tulipokuwa tunawahamisha watu wetu kutoka ngorongoro kwenda msomera ili kulinda hifadhi na wanyama walipiga kelele pia, sijui wanawashwa na kitu gani. Mabomu wanayotengeneza ndiyo yanayochafua mazingira.
 
Mtamuuzia nani?
Mtatoa wapi hela?
Technolojia?
Hee, swali hilo tuwaulize waganda wenye mafuta yao lakini hata sisi mafuta haya tutayahitaji maana yatakuwa rahisi, tutaifufua tipper yetu na kuanza kuyasafisha.
 
We have to take EU concern very seriously and maybe invite them in the future proceedings regarding the project.

But so far we remind EU of our knowledge of where they started to develop their economies. For instance when England became the workshop of the world they used steam engines and burned million calories of coal!

We also take this opportunity to let them know that we are aware of similar projects conducted in India and the conflict between India and USA regarding burning of fossil fuels for power generation!

Tanzania as among sovereign countries of the world has the mandate and authority to operate projects that will bring fast economic growth without interference from international community

We are very sorry to European Union but we must continue with our projects for benefit of the people of Tanzania!
well narrated
 
too late, tunayo miradi mingi mno ya hivi; TAZAMA, SGR, Bwawa, Songas, Buzwagi, Merelani, daraja la wami, kigamboni, nk. Hawa ni wapuuzi tu, tulipokuwa tunawahamisha watu wetu kutoka ngorongoro kwenda msomera ili kulinda hifadhi na wanyama walipiga kelele pia, sijui wanawashwa na kitu gani. Mabomu wanayotengeneza ndiyo yanayochafua mazingira.
Dogo hapa unachanganya changanya mambo, sote lengo letu moja ila mtu akikuambia uzaifu wako fanyia kazi kwanza sio kwa ubaya. Inawezekana hujui mengi lakini hata wanaokulipa uwasifie wakijua ukweli mie nakwambia watakulipa mara mia zaidi na value yako kwako ndio itapanda.

Tunajua humu JF mmeiteka kwa propaganda lakini huu mtumbwi mnaolipwa kuutoboa na nyinyi mmepanda, hao wanaowalipa ni wakishua hawatazama na nyinyi. ongezeni uzalendo kwa Tanzania na watanzania wenzenu nyie kizazi kipya tunawategemea mnaakili tatizo lenu moja tu hamuwezi vumilia njaa tu.
 
Vita ya kiuchumi hii sasa,wapambane
Nayo

Ova
 
Hawa jamaa mambo yao ya kujadili yameisha?
Bunge la Ulaya limesema kuwa ni marufuku Tanzania na Uganda kujenga bomba la mafuta na gesi kutoka Uganda kwenda Tanga Tanzania kwakuwa mradi unachafua mazingira na unadhulumu watu linakopita ni sawa? Maswali hapa ni:

1. Wazungu wanapata wapi nguvu hii ya kutuamulia sisi nini kizuri na nini kibaya? Je , ni hii tabia yetu ya ombaomba na utegemezi kwao ndio inayotuponza? Je, historia ya utumwa inatuponza, wanatudharau kutuona kama wajinga, watumwa wao?

2. Ni kweli mradi huu unaharibu mazingira kwa kiasi hicho kuliko wao wanavyochafua? Viwanda vyao havichafui mazingira?

3. Ni kweli watu wetu wanaopitiwa na mradi hawakupata stahiki zao sawasawa na thamani ya mradi wenyewe (value for money)? Wamedhulumiwa na wajanja? Nchi zao hazikujengwa na watumwa na Mali za kupora wengine?

4. Nini hatima ya uhusiano wetu na nchi za Magharibi, wakoloni wetu wa zamani? Ndio ukoloni unarudi tena? Wanawaza kurudi tena?
Sasa si waje watawale tena kama ndo wanalotala
 
Dogo hapa unachanganya changanya mambo, sote lengo letu moja ila mtu akikuambia uzaifu wako fanyia kazi kwanza sio kwa ubaya. Inawezekana hujui mengi lakini hata wanaokulipa uwasifie wakijua ukweli mie nakwambia watakulipa mara mia zaidi na value yako kwako ndio itapanda.

Tunajua humu JF mmeiteka kwa propaganda lakini huu mtumbwi mnaolipwa kuutoboa na nyinyi mmepanda, hao wanaowalipa ni wakishua hawatazama na nyinyi. ongezeni uzalendo kwa Tanzania na watanzania wenzenu nyie kizazi kipya tunawategemea mnaakili tatizo lenu moja tu hamuwezi vumilia njaa tu.piga
wacha hizo, wakati wazungu wanaipiga dunia kwa makombora mazito ya moto na kuifukisha moshi mzito wa viwanda vizito (mama) na midege mikubwamikubwa angani wacha na sisi tuipekeche kidogo kupitisha mabomba ya gesi, mafuta, maji, mkongo, reli na barabara, Wacha tushirikiane kuiharibu dunia ili tusije kulaumiana huko mbele ya safari mambo yakiharibika. Ulaya ina hofu na global warming zaidi kuliko nchi nyingine, vinchi vyao muda sio mrefu vitamezwa na maji.
 
Back
Top Bottom