Bunge la Ulaya na Neo Colonialism-kiini cha kupinga bomba la mafuta toka Uganda hadi Tanzania

Bunge la Ulaya na Neo Colonialism-kiini cha kupinga bomba la mafuta toka Uganda hadi Tanzania

Naunga mkono hoja.
Hawa mabeberu na neo colonialism ni watu hatari sana!. Angalia walichomfanya Gadafi na Saddam, usikute hata yule Blaza wangu ni wao!.

Mimi niliwahi kuuliza humu US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali?
Mwisho wa siku do we know what really happened?. Ni sisi tuu kuletewa ile taarifa kuwa... just gone!.

Hata alipobadili sheria mpya ya madini ili yatufaidie zaidi, niliuliza humu Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts? leo migodi mingapi wame subscribers kwenye sheria mpya?, na madini ni deminishing resources!. Tutakuja kuachiwa mashimo!.

P

Mna mambo ya ajabu sana mnalaumu Mzungu kwa neo coloniliasm hapo hapo mnatangaza siku 5 za maombolezo kifo cha Mkuu wa Colonialism tena mnapeperusha bendera nusu mlingoti kwa heshima kubwa kama hiyo haitoshi mnafunga safari kwenda London kuzika, sasa Mzungu kosa lake ni lipi kama ninyi wenyewe hamjitambui wala kujielewa ?

Watu waliopinga hilo Bomba ndiyo hao hao Samia kapanda ndege kwa gharama yetu kwenda kuwazika na kutangaza siku za maombolezo hapa Tanzania.

Imefika wakati muwe matured people na kukubali kwamba Waafrika wenyewe ndio tatizo Afrika, Tanzania siyo masikini sababu ya colonialiasm, no Tanzania ni masikini sababu ya Low IQ ambayo ndiyo chanzo cha underperfomance, ineficiency na incompetence kila mahali, leo hii Polisi wanashoot to kill watoto wa miaka 14 ambao walipaswa kuwa shuleni, Mzungu anahusika vipi hapo? Kwanza anatoa hela kuwapa ili msomeshe watoto lkn bado mnashindwa, halafu mnalia
Colonialism?

Mpaka tutakapoanza kupractice meritocracy ndiyo tutatoka hapa vinginevyo ni vilio na kulaumu kila mtu kila siku!
 
jambo la msingi hapa ni kujibu hoja zilizo tolewa na Hilo Bunge la European Parliament, kuwa mradi huo utaleta uharibifu wa kimazingira haswa uchafuzi wa maji ya ziwa victoria.
hapa ndipo hoja ilipo, je kuna ukweli? je Wataalamu wetu walifanya utafiti? wanao wajibu wa kutoa ufafanuzi juu ya hoja hizo.

Tujibu hoja tusikimbilie kulalamika kuonewa au kuonewa wivu au vita ya kiuchumi.
inaweza ikawa chokochoko ya vita ya kiuchumi lakini twendeni kwa hoja.tusilipuke wala tusikubali kuhamaki, tujibu hoja kitaalamu na kwa uthibitisho wa kitaalamu ili tuwashinde kwa nguvu ya hoja za kitaalamu.
 
Bunge la Ulaya limeazimia kuufuta mradi wa bomba la mafuta toka Uganda hadi Tanga Tanzania.
Sababu za kitoto wanazotoa ati ni uharibifu wa mazingira na haki za binadamu!!

Huu ni uhujumumu wa moja kwa moja kwa uchumi wa nchi za kiafrika zinazotaka kujikomboa katika umasikini kwa kutumia malighafi zilizo katoka nchi zao.

Unafiki wa EU unaonekana wazi kabisa.
Tanzania enzi za Mwalimu Nyerere tulijenga bomba la mafuta la TANZAM, bomba hili linafanya kazi hadi leo hii.
Lakini kwa vile mafuta hayo yanatoka kampuni zao, huko ni kimya kabisa.
Vile vile leo hii EU inalilia bomba la gesi toka Urusi lisizimwe ili nchi zao ziendelee kupata gesi kuendesha uchumi wao.

Nchi hizi za Ulaya, EU, wnapendelea nchi za kiafrika ziwe tegemezi kwao daima dumu.
Tanzania lazima tulaani msimamo huu wa EU na bunge lao.

Labda nikuulize swali, hivi ni Afrika peke yake iliyotawaliwa kwa Ukoloni Dunia hii? Kwanza kwa taarifa kati ya sehemu ambapo haikutawaliwa kwa muda mrefu na Ukoloni ni Afrika, lkn kwingine kote walitawaliwa pia, mbona wao hawalii neo colonialism?

Acheni kuficha low intelligence inayopelekea under perfomance ya Afrika kwa kisingizio cha Coloniliasm.

Capitalism ina run Dunia, maana yake ni competition yule anayeshinda anasonga mbele, sasa sisi tunalea panya road tunashindwa hata kulea watoto wetu wenyewe bado unalaumu colonialism?

Nchi zote zilizotoboa siyo kwamba ziliwekewe red carpet no, ni hard work ndiyo iliyowatoa na siyo lele mama na kulia lia kuonewa kila siku, kwani Dunia hii waonewao ni Afrika peke yake?

Ondoa visingizio, Tanzania siyo masikini sababu ya Colonialism, Tanzania ni masikini sababu hatufwati meritocracy, kama tungefwata meritocracy 90% ya Viongozi waliopo sasa hivi hata ukarani wasingepita interview, mchawi yuko hapo na siyo sijui colonialism BS!
 
Kwa viongozi gani tulionao wa kupinga na kulaani? Labda waishie hapo tuu kwenye kupinga na kulaani na hiki ni kipimo Cha misimamo na maamuzi ya viongozi wetu

Time Will tell
 
Haya maneno mazito ; "Kufanya maamuzi magumu"

Sioni umuhimu wa kubandikwa "Uchumi wa Kati" na Kadhalika ili kradi tu....hailetiaana yeyote kama Hatuwezi kujiuzia hata Mafuta au Gesi??? Maana yaa masoko ya ndani ni nini, Kwanini tusiuziane? nasikia SADC peke yake kuna watu milioni zaidi ya 300 maana yake nini haswa??

Nimeona sehemu kuna watu Texas Marekani, nafikiri na Ohio wenye mashamba yao yenye kutoa mafuta, kwa kutumia teknoloji/ pampu za miaka ya 1800.. na mapampu yanafanya kazi mpaka leo. Na sio makampuni makubwa ni Watu binafsi, na wanaula Nini hasa tunacho shindwa? Nao wanachangia mafuta hayo kwa vipipa kadhaa kwa mwezi....haba kwa haba hujaza .... Hata hivyo tunashindwa? Kwani Capital wanaleta au tunawapa?

Vita vya Uchumi vipo, lakini sio vita zote hutoa mshindi, tufike sehemu tuseme wewe hujashindwa na sisi hatujashindwa..

Tufanye uamuzi, maamuzi ya Kungo'ka huko, COMMONWEALTH kwanza na kubatilisha treATies na EU - kwani wao wenyewe wa Ulaya wanasambaratika, in 10 to 25yrs na tuwaambie tuu 'Hatujui muendako' nasi tuna safari zetu.

Neo Coloniasm is Real.
 
Haya maneno mazito ; "Kufanya maamuzi magumu"

Sioni umuhimu wa kubandikwa "Uchumi wa Kati" na Kadhalika ili kradi tu....hailetiaana yeyote kama Hatuwezi kujiuzia hata Mafuta au Gesi??? Maana yaa masoko ya ndani ni nini, Kwanini tusiuziane? nasikia SADC peke yake kuna watu milioni zaidi ya 300 maana yake nini haswa??

Nimeona sehemu kuna watu Texas Marekani, nafikiri na Ohio wenye mashamba yao yenye kutoa mafuta, kwa kutumia teknoloji/ pampu za miaka ya 1800.. na mapampu yanafanya kazi mpaka leo. Na sio makampuni makubwa ni Watu binafsi, na wanaula Nini hasa tunacho shindwa? Nao wanachangia mafuta hayo k

Vita vya Uchumi vipo, lakini sio vita zote hutoa mshindi, tufike sehemu tuseme wewe hujashindwa na sisi hatujashindwa..

Tufanye uamuzi, maamuzi ya Kungo'ka huko, COMMONWEALTH kwanza na kubatilisha treATies na EU - kwani wao wenyewe wa Ulaya wanasambaratika, in 10 to 25yrs na tuwaambie tuu 'Hatujui muendako' nasi tuna safari zetu.

Neo Coloniasm is Real.
Well said mkuu, sijui tunakwama wapi wakizila tunajiuzia wenyewe, tatizo litakuja kwa technology! Lakini wataalaam tunao ila hatujui tunawatumia vp[emoji23][emoji23] ila Africa, hata Kama tukienda mbinguni lazima tutakua na taratibu za kula fimbo kwanza ndio tufike kwa Sir God.

Mungu katupa Kila kitu lakini wapiii, tupo wengi tunaweza kuamua kununua mafuta ya waafrica wenzetu na tukatoboa lakini sasa nyumbu ni wengi.

Africa my Africa,[emoji24]
 
Labda nikuulize swali, hivi ni Afrika peke yake iliyotawaliwa kwa Ukoloni Dunia hii? Kwanza kwa taarifa kati ya sehemu ambapo haikutawaliwa kwa muda mrefu na Ukoloni ni Afrika, lkn kwingine kote walitawaliwa pia, mbona wao hawalii neo colonialism?

Acheni kuficha low intelligence inayopelekea under perfomance ya Afrika kwa kisingizio cha Coloniliasm.

Capitalism ina run Dunia, maana yake ni competition yule anayeshinda anasonga mbele, sasa sisi tunalea panya road tunashindwa hata kulea watoto wetu wenyewe bado unalaumu colonialism?

Nchi zote zilizotoboa siyo kwamba ziliwekewe red carpet no, ni hard work ndiyo iliyowatoa na siyo lele mama na kulia lia kuonewa kila siku, kwani Dunia hii waonewao ni Afrika peke yake?

Ondoa visingizio, Tanzania siyo masikini sababu ya Colonialism, Tanzania ni masikini sababu hatufwati meritocracy, kama tungefwata meritocracy 90% ya Viongozi waliopo sasa hivi hata ukarani wasingepita interview, mchawi yuko hapo na siyo sijui colonialism BS!
Jaribu kuelewa argument yangu.
Tatizo kubwa hapa ni mindset na utegemezi, tungekuwa tunatekeleza miradi hii kwa hela yetu upuuzi wa EU haungekuwepo.
Tumefanya hivyo kwa Mradi wa Umeme wa JNHPP-Rufiji na hakuna aliyesema fyoko.
Mindset ya EU ni kututawala kiuchumi na unapotaka kujitoa kwenye hali ya utegemezi kwa kutumia mikopo toka Benki zao, tatizo liko hapo.
Haya ya kusema kuna Haki za Binadmu au uharibifu wa Mazingira , hayo yote ni ufedhuli tu wa kukuambia utaondokaje katika makucha yangu kwa hela yangu-na ndio Neo Colonialism.
I hope you get it!
 
Naunga mkono hoja.
Hawa mabeberu na neo colonialism ni watu hatari sana!. Angalia walichomfanya Gadafi na Saddam, usikute hata yule Blaza wangu ni wao!.

Mimi niliwahi kuuliza humu US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali?
Mwisho wa siku do we know what really happened?. Ni sisi tuu kuletewa ile taarifa kuwa... just gone!.

Hata alipobadili sheria mpya ya madini ili yatufaidie zaidi, niliuliza humu Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts? leo migodi mingapi wame subscribers kwenye sheria mpya?, na madini ni deminishing resources!. Tutakuja kuachiwa mashimo!.

P
Ni kweli kabisa, Economic Dominance ndio game lao.
 
Jpm aliposema kuna vita ya kiuchumi hamkukubali. Leo mnakula uturn kusema hii ni vita ya uchumi, kwani wazungu tuko nao katika ushindani hadi watupige vita vya kiuchumi? Mbona wanatupa arvs, corona vaccines na misaada kadhaa, ingekuwa ni neo colonialism si wasingetupa hata hiyo misaada. Itakuwa ni kweli studies zao zinaonesha mradi utaathiri ikolojia. tusikaze shingo tutaumia kupambana nao kikubwa tuachane na mradi huu na kuzingatia ushauri wao wa kitaalamu
Mkuu ujue , watakupa chakula , ARVs,Mabasi mazuri, kukuchimbia visima vya maji, hata kukujengea barabara.
Hivyo vyote vitakufanya uendelee kuwa tegemezi hadi ufe!

Lakini ukitaka kujenga viwanda vya msingi ili ujitegemee kiuchumi , kama kuanzisha viwanda vya chuma, miradi mikubwa ya nishati(kama JNHPP), basi hapo umewachokoza.
Wengi wenu hamjui kuwa hata TAZARA walikataa kabisa (World Bank na EU), kutukopesha kuijenga hadi ple Mwalimu alipowashirikisha wachina na ikajengwa.

Eu na wazungu ni sumu ya maendeleo.
 
Siyo bomba la mafuta tu wafungie hata bandari zote, mbuga , hivyo ni rasilimali zetu ila hazina faida kwetu,

Tozo zinatosha kuendesha nchi.
 
..hivi mna uhakika kwamba Tz itafaidika na bomba la mafuta toka Uganda?

..pia kwenye mradi huo ipo kampuni ya Total toka Ufaransa ambayo ni mwanachama wa EU. Je, kampuni Total imelalamika kuhusu Neo Colonialism?
Kwa uhakika Tanzania itafaidika , hata kama ni ajira za nchimi kwetu.
Kuhusu Total, kweli hiyo ni kampuni toka mwanachama wa EU, na wameshida hiyo tenda ya kujenga bomba, lakini wao si financiers wa mradi.
 
..miradi mingi huwa tunaahidiwa ahadi nzuri-nzuri baadae tunakuja kugundua kwamba ni dhuluma tupu.
 
Kujenga si lelemama, fedha nyingi na muda ni mrefu.

..watetezi wa huu mradi kwanini mnafikiri hautaharibu mazingira?

..Je, faida ambayo Tanzania itazipata inahalalisha uharibifu utakaosababishwa na mradi?
 
..watetezi wa huu mradi kwanini mnafikiri hautaharibu mazingira?

..Je, faida ambayo Tanzania itazipata inahalalisha uharibifu utakaosababishwa na mradi?
Mkuu pengine wewe bado ni kijana sana.
Kama umekuwapo nchini nikuulize tu, TAZAMA Pipeline ilijengwa 1968 na baba zetu Mwalimu Nyerere na Kaunda.
Mradi umekuwepo kwa miaka 54 sasa.
Je, umesikia uharibifu wowote unaotokana na mradi huo?
Tusipende kumeza propaganda za EU mazima mazima.
 
..Tazama pipeline imepita wapi?

..Na bomba la Hoima-Tanga litapita wapi?

..hoja ya mazingira iwekwe mezani na serikali ieleze kinagaubaga tutakabiliana vipi na changamoto hizo.

..sidhani kama ni sahihi kupuuza hoja hizo kwa madai kuwa ni ukoloni mamboleo.

..Pia uelewa wetu kuhusu mazingira umeongezeka toka 1968 wakati Tazama inajengwa.

..hata serikali zetu zina propaganda. Baadhi ya viongozi wetu ni madhalimu kuzidi hata wakoloni walivyokuwa.
 
kwenye mradi huo ipo kampuni ya Total toka Ufaransa ambayo ni mwanachama wa EU. Je, kampuni Total imelalamika kuhusu Neo Colonialism?
Hawa TotalEnergies ni moja ya makampuni mema sana kwa nchi yetu!. Imeleta neema kibao humu nchini mwetu Tanzania
Hizi ni baadhi ya neema hizo
  1. Uwekezaji: Sio Kila Uwekezaji na Kujenga Nchi, Mwingine ni Kuvuna tu, Uwekezaji wa Total Energies kujenga Nchi!
  2. Nishati Jadidifu: TotalEnergies yafanya tena kweli, yaongoza njia. Waziri Makamba aipongeza, awataka wengine wafuate
  3. Kumbe Watanzania Wana Uwezo Kuwa Mabilionea, Walikosa Mitaji na Mbinu!. TotalEnergy Mkombozi, Yamwaga Fursa za DODO Nchi Nzima!. Tuchangamkie Fursa?.
  4. Una Eneo Pembeni ya Barabara?, Ungependa Kuwa Millionaire au Bilionea?. Usiuze Eneo Lako!. Total Kutengeneza Ma Milionea na Ma Bilionea 100 wa DODO!.
  5. Total Tanzania yafanya makubwa, kuigeuza Tanzania kama Ulaya, yaanzia Temeke
  6. Licha ya kufanya makubwa Tanzania, kampuni ya mafuta ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, yaahidi kufanya zaidi na zaidi!
  7. Jee Kuna Ukweli Kuwa in Tanzania, Mafuta ya Vituo vya Total, " They are The Best?. If Yes, How Wakati Tunanunua Bulk?.
  8. Maendeleo ya Kweli Yataletwa na Watanzania: Kampuni ya Mafuta ya Total Yazindua Kituo cha Kwanza cha Watanzania, Total Tegeta Service Station
  9. Total yatoa fursa vituo vya COCO na CODO kuzigeuza DODO! Kuwa umiliki kituo cha mafuta cha total
  10. Mhe. Anthony Mavunde, One of the Few, Very Best Magufuli Has. Anafaa Kuwa Waziri Kamili, Nimeguswa kwa Hili
Haya ni mambo 10 tuu, tukitaka 100 pia hapo!. Hivyo TotalEnergies ni kampuni rafiki wa kweli kwa Tanzania!.

P
 
Back
Top Bottom