Bunge la Urusi lamruhusu Rais kupeleka majeshi mahala popote Duniani

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Bunge la Urusi limempa Rais wa n hi hiyo nguvu ya kupeleka majeshi yake mahala popote Duniani pale itakapo hitajika.

Bunge hilo limefikia uamuazi wake Leo 22.02.22 siku moja mara baada ya Urusi kuyatambua majimbo yaliyokua yanapigania kujitenga na Ukraine.

Kwa mtazamo wangu hii nayo ni moja ya mahesabu makali sana ya Urusi na rais wake.

Kwa mtazamo wangu hii maana yake ni kwamba jeshi la Urusi Sasa Lina ruhusa ya bunge kwenda kuishambulia nchi yoyote itakayoonekana kutishia usalama wa Urusi.

Mfano kama USA na NATO wataingia kijeshi kukabiliana na Urusi huko Ukraine,maana yeka nayo Urusi itajibu kwa kumfuata Adui yoyote katika NATO ambae itaona inastahili kumshambulia.

Mfano ni kama USA akiingia kijeshi dhidi ya Urusi naye Urusi ataifuta USA na kujibu mapigo hukohuko.

Hii si Hali njema hata kidogo.
 
Russia haina ubavu wa kupigana na NATO japo hata NATO hawatamani kuingia kijeshi kwny hilo
uzuri Rais kashapewa go ahead
ni kama kiduku alivyowaambia USA risasi moja tu ikitua PYONGYANG anavurumisha midude DC mfulululizo

Vivyo hvyo Urusi kwa go ahead alopewa putin na BUNGE nchi yoyote ya umoja wa NATO ikijitia kimbelembele midude ya HAJA inavurumishwa katika ARDHI yao habari ndio hiyo maana ya kuruhusiwa kwenda popote na JESHI
 
Nafikiri unaongea kitu usichokijua.

Ingekua vema ungesema Haijulikani nani ataibuka mshindi baina ya Russia na NATO.

Lakini ubavu TU wa kupigana nao Russia anao sana tu.

Hata NATO wenyewe wanalijua hilo.
 
Wewe unaijua Russia?anasilaha ya kuwapiga NATO wote Kwa Mara moja.
Ukiizungumzia nato unazungumzia USA , France, UK, na German. Hao wengine ni viherehere. Kuna vinchi vingine vilivyozaliwa baada ya kuanguka kwa ukomunisti navyo ni sehemu ya Nato japo vyenyewe havina mchango wowote.

German hawezi kukubali kushambuliwa na russia vile vile kwa france na uk. Hii ngoma itapiganwa kwenye meza ya mazungumzo. Ukraine kashapoteza majimbo mawili. Akiendelea na kelele ataporwa jingine. Kuna viongozi wanapenda kuwaletea wananvhi wao shida na tabu. Ref Saddam Hussein na Ghadaff. Walitakiwa waachie nchi maisha yaendelee. Wakashupaza shingo kilichofuta kila mtu alikiona.
 
Bunge la Urusi limempa Rais wa n hi hiyo nguvu ya kupeleka majeshi yake mahala popote Duniani pale itakapo hitajika.
Bunge hilo limefikia uamuazi wake Leo 22.02.22 siku moja mara baada ya Urusi kuyatambua majimbo yaliyokua yanapigania kujitenga na Ukraine.

Kwa mtazamo wangu hii nayo ni moja ya mahesabu makali sana ya Urusi na rais wake.

Kwa mtazamo wangu hii maana yake ni kwamba jeshi la Urusi Sasa Lina ruhusa ya bunge kwenda kuishambulia nchi yoyote itakayoonekana kutishia usalama wa Urusi.
Mfano kama USA na NATO wataingia kijeshi kukabiliana na Urusi huko Ukraine,maana yeka nayo Urusi itajibu kwa kumfuata Adui yoyote katika NATO ambae itaona inastahili kumshambulia.
Mfano ni kama USA akiingia kijeshi dhidi ya Urusi naye Urusi ataifuta USA na kujibu mapigo hukohuko.

Hii si Hali njema hata kidogo.
US atapigwa kutokea Cuba
 
Nafikiri unaongea kitu usichokijua.
Ingekua vema ungesema Haijulikani nani ataibuka mshindi baina ya Russia na NATO.
Lakini ubavu TU wa kupigana nao Russia anao sana tu.
Hata NATO wenyewe wanalijua hilo.
Wahenga walisema:
'Vita haina macho...' Na pia haina guarantee!
Ni busara kuweka akiba ya maneno!
 
Ufaransa imeomba kukutana kwa mara nyengine na Putin, sijui kama watakubaliwa[emoji16], hawa wamemchokoza Urusi moto wake kuuzima inakua tabu sana
wanaweka vikwazo ambavyo havina madhara mala wamekea vikwazo watu maarufu na bank wanamjua vizuri jamaa haongei sana ni action tuu bado uk kanajiona sana hakajwahi kuvamiwa pale kisiwan kameshikilia Mali za raia wa urusi.
 
Hii hatua ta urusi kuyatambua hayo majimbo na bunge kumpa rais green right ya kupeleka majeshi sehemu yoyote ile ni mahesabu makubwa sana na ktk huu mgogoro urusi ataibuka kidedea

Hii tabia ya malekani ya ku undermine wakubwa wenzake, itamgharimu sana na kuonyesha madhaifu yake. Haache kuishi kwa mazoea, dunia imebadilika sana
 
wanaweka vikwazo ambavyo havina madhara mala wamekea vikwazo watu maarufu na bank wanamjua vizuri jamaa haongei sana ni action tuu bado uk kanajiona sana hakajwahi kuvamiwa pale kisiwan kameshikilia Mali za raia wa urusi.
Vikwazo havinaga madhara ktkt nchi zinazojielewa. Kiduku amewekewa vikwazo miaka 50 iliyopita, lakini angalia moto wake mpaka wenyewe wanamwita kwenye table kutaka kuelewana
 
Ufaransa imeomba kukutana kwa mara nyengine na Putin, sijui kama watakubaliwa[emoji16], hawa wamemchokoza Urusi moto wake kuuzima inakua tabu sana
Wamemchokoza kivipi mkuu?
Naona km Putin ndio kaanza kuleta chokochoko.
 
uzuri Rais kashapewa go ahead
ni kama kiduku alivyowaambia USA risasi moja tu ikitua PYONGYANG anavurumisha midude DC mfulululizo

Vivyo hvyo Urusi kwa go ahead alopewa putin na BUNGE nchi yoyote ya umoja wa NATO ikijitia kimbelembele midude ya HAJA inavurumishwa katika ARDHI yao habari ndio hiyo maana ya kuruhusiwa kwenda popote na JESHI
Unawaza kizembe sana mkuu, unadhani hao uliowataja watakaposhambuliwa na urusi wao watakaa tu kwa kutulia et kwa sababu bunge la urusi limeruhusu majeshi kwenda pahali popote duniani.
 
Back
Top Bottom