Bunge laazimia Serikali ianze ujenzi wa Bandari Bagamoyo je haya waliyazingatia wabunge?

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
BUNGE limepitisha azimio la kuitaka Serikali iharakishe utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Bandarii ya Bagamoyo.

Azimio la Bunge hili la Bunge kuhusu Mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo limeazimia na Bunge lakini mradi haujawahi kuwepo.

Azimio la Bunge kuagiza mradi huu utekelezwe haraka lilikuwa linatoka wapi wakati mradi huo haupo kwenye mipango ya Serikali na haujawahi kutengewa fedha na Bunge ndio maana hata ukisoma vitabu vya Serikali haumo.

Sasa Bunge linawezaje kuiagiza Serikali katika jambo ambalo halina uchambuzi wa kina lakini azimio hili linatolewa huku Bunge halijui za gharama ya mradi, uwezo wa nchi kugharamia mradi huo, hatua ya utekelezaji wa miradi mingine ya kimkakati, uwezo wa kukopesheka na vigezo na sababu zingine za kiuchumi.

Hivi wabunge wakati mnalipitisha azimio hili kuhusu Bandari ya Bagamoyo mliyazingatia hayo au mliazimia nini.

 
BUNGE limepitisha azimio la kuitaka Serikali iharakishe utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Bandarii ya Bagamoyo...
Kina Babu Tale waliyazingatia kweli haya kabla hawajasema NDIOOO mbona huu mradi kama una mashaka makubwa ila wabunge Mungu anawaona mnavyokuwa mnapitisha viti.

Serikali ilishindwa kuendelea na huu mradi baada ya kelele kuwa nyingi kwa wananchi leo Bunge limeingia mtego wa Serikali ili ionekane ni maagizo ya Bunge
 
Miradi mingine bado inasua sua, na huo tena wanaanza kuhangaika nao? Mmm haya !
 
Tujiandae kisaikolojia kuwa koloni la China, Hadi watakapozaliwa kina nyerere wengine, kwa sasa kina mangungo hatuna namna
 
Mnapiga kelele wakati wataalaam wapi Tatari bagamoyo zaidi ya miezi 3 sasa
 
Bribery is NO longer a question of WHY, but how MUCH, tuendelee kunywa mchuzi mifupa tutakutana nayo chini ya bakuli
 
Bune? Au kikao Cha CCM?
 
Hao hao wabunge wanaopiga makofi na kucheka hata wanapoongea ya msingi au ya kuhuzunisha?

Mbunge anasema itengwe siku ya viboko nao wanacheka
Huwa unajiuliza hivi hawa kweli wanajielewa au wanaowaongoza ndio mazuzu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…