Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imetoa taarifa kuhusu uendeshaji wa mradi wa mabasi yaendayo Haraka (BRT) jijini Dar es Salaam na kubaini tija ndogo katika utekelezaji wake licha ya uwekezaji mkubwa wa serikali.
Hayo yamebainishwa bungeni jijini Dodoma leo Jumatatu Februari 10, 2025 na Mwenyekiti wa PIC, Augustine Holle ambapo amesema kuwa Serikali imewekeza Sh1.3 trilioni katika awamu mbili za mradi na Dola za Marekani 148.2 milioni kwa awamu ya tatu.
“Hata hivyo, Kamati imegundua kuwa Awamu ya Kwanza (Kimara - Kivukoni) inatumika kwa kiwango kidogo, Awamu ya Pili (Mbagala Rangitatu - Katikati ya Jiji) imekamilika lakini haijapata mwendeshaji kwa zaidi ya mwaka mmoja, na Awamu ya Tatu (Azikiwe - Gongo la Mboto) imekamilika kwa asilimia 55 bila mchakato wa kumpata mwendeshaji,” amesema Holle.
Kamati imeitaka DART kuharakisha upatikanaji wa watoa huduma kwa awamu zote ili kuhakikisha mradi huu unatumika kikamilifu na kuleta tija kwa wananchi na taifa.