Bla bla nyingi kila siku Kafulila anatamba kwenye vyombo vya habari juu ya ushirikiano wa serikali na watu binafsi huku akiwaita wafanyabiashara binafsi kama wameona fursa waende wapewe. Wameshindwa nini kumpa baadhi ya njia Bakhresa au mwekezaji mwingine yoyote mzawa? Hivi mradi mdogo kama mwendokasi bado serikali itataka mwekezaji toka nje?
Zaidi ya mwaka sasa mabasi ya mwendokasi yamepungua kwa kiasi kikubwa je hatua gani zimechukuliwa na serikali zaidi ya kuwabadilisha mabosi wa mwendokasi kila kelele zikizidi ili kuwazuga wananchi. Nilitegemea bunge liiwajibishe serikali kwenye hili lakini inaonekana kama bunge nalo linalalamika tu kama raia wa kawaida wa Kimara na Mbezi.