Bunge ladumu kwa dakika 15 kisha kuahirishwa. Kisa, Mwigulu kutokuwepo Bungeni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kikao cha kwanza cha mkutano wa tatu wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kimeanza leo Machi 31, 2026, ambapo hata hivyo, kimedumu kwa dakika 15 pekee kisha kuahirishwa mpaka Aprili 1, 2026 saa 3:00 asubuhi.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Daniel Baran Sillo  ameongoza Kik.jpg

Sababu ya kuahirishwa ni kutokana na Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye alitakiwa kuanza kuwasilisha bajeti yake kutokuwepo bungeni akitarajiwa kuongoza Watanzania katika maziko ya aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi.

Bunge hilo linalenga kujadili na kupitisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
 
Kikao cha kwanza cha mkutano wa tatu wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kimeanza leo Machi 31, 2026, ambapo hata hivyo, kimedumu kwa dakika 15 pekee kisha kuahirishwa mpaka Aprili 1, 2026 saa 3:00 asubuhi.

Sababu ya kuahirishwa ni kutokana na Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye alitakiwa kuanza kuwasilisha bajeti yake kutokuwepo bungeni akitarajiwa kuongoza Watanzania katika maziko ya aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi.

Bunge hilo linalenga kujadili na kupitisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Na seatting allowance ya leo niaje?, italipwa???
 
MIe nnachokiona tunatawaliwa/ kuongozwa na watu ambao tumewazidi akili, wanadhani bado tuko zama zilee za zidumu fikra za mwenyekt wa chama!.
Wanafanya maamuzi ambayo kwa dunia ya leo hayana logic kabisa...ni wazi kukutana kwa dkk chache bungeni leo kulikuwa ni kwa ajili ya kuhalalisha kulipana posho tuuu na sio vinginevyo...wananchi tunatakiwa kuamka na kufanya kitu kamwe tusikubali kufanywa wajinga hv na kakikundi kadoogo ka watu kanakojiita WAHESHIMIWA!!.
 
Back
Top Bottom