Mpina ni jasiri ana heshima yake mbele ya jamii ya watanganyika. Kamati inasema tu ilijiridhisha na GN bila kutuwekea hicho kithibitisho ili nasi tuone, wajinga sana.
Hiyo adhabu anayopewa na wajinga haina maana kwa watanganyika kwasabau wanajielewa, wao sio wajinga.
Haiwezekani wale waliompiga vita Mpina wakiongozwa na Spika Tulia, wakishirikiana na mama Abdul leo wamtendee haki, hiyo mahakama ni batili haina fairness.
• Hii kamati inataka kutudanganya watanganyika kwamba, wakati wa dharura, serikali inaweza kuagiza sukari hata kwa kutumia kampuni zisizo na ujuzi kwenye hiyo issue ilimradi sheria iwaruhusu? na isiyo na mtaji wa kutosha kama ile stationery ya mtaji wa 1 million kuagiza sukari ya bilion 6.6?!
Kamati ya wapuuzi wanajibu hoja za Mpina kama watoto.
Spika Tulia na hiyo kamati yake wasitufanye wajinga, wao wote hawana mamlaka ya kumhoji Mpina kwa kitendo chake cha kuongea na wapiga kura wake nje ya bunge, wasitake kulifanya bunge liwe juu ya mamlaka na uhuru wa watanganyika kutoa maoni yao kikatiba.
Bunge ni lile jengo tu pale Dodoma ambapo wakiwa ndani yake ndio hutakiwa kusema chochote wasishtakiwe, lakini wakitoka nje ya lile jengo wao ni wabunge wa kawaida na raia kama tulivyo wengine, wasijikuze.
Simply Mpina ameonewa, hastahili kuadhibiwa kwani hajavunja sheria yoyote ya nchi, standing orders za bunge haziwezi kuwa juu ya katiba yetu, mafisadi walaaniwe, shame on them.
Hoja za Mpina zijibiwe, mmeshindwa kuzijibu kutuonesha nyie ni mafisadi wa vitendo na ushahidi upo, adhabu yoyote kwa Mpina haitafuta dhambi ya ufisadi wenu, aibu iwe kwenu.