Bunge lapitisha sheria ya afya ya mimea. Faini ya milioni 500 kutolewa kwa watakaoikiuka

Bunge lapitisha sheria ya afya ya mimea. Faini ya milioni 500 kutolewa kwa watakaoikiuka

Kweli elimu haina mwisho nimesoma mara4 lakini mwisho nimeamua kuja kwenye comment pia wenzangunao wanasema hawajaelewa dah. Sio shida aliyeandika atueleweshe tuelewe
 
Happ ndipo tutajua kati ya DNA VS RNA nani mbabe.
 
Kwa kweli ni sheria nzuri itakayounganisha PHS(Plant health services) na TPRI(Tropical Pesticides Research Institute), na kuleta kitu kinachoitwa TPPHA(Tanzania Pesticides and Plant Health Authority).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Picha

​
SHERIA ya Afya ya Mimea 2020 imepitishwa pamoja na mambo mengine imetoa adhabu kwa Bodi ya Shirika itakalovunja sheria hiyo kupigwa faini isiyopungua Sh milioni 10 na isiyozidi Sh milioni 500.

Vile vile kwa mtu atakayevunja sheria hiyo atatozwa faini isiyopungua Sh 50,000 na isiyozidi sh milioni 10 au kwenda jela kwa kifungo kisichopungua miezi mitatu na kisichozidi miaka mitatu.

Akiwasilisha muswada huo bungeni, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema mtu akikiri kosa lake kwa kuandika mwenyewe kuwa anakiri, atatakiwa kulipa mbili ya tatu ya fedha anazotakiwa kisheria kama angekuwa amehukumiwa.

Pia alisema mtu akishindwa kulipa fedha hizo katika muda ulipangwa, Mkurugenzi Mkuu au mtu mwenye mamlaka inayohusika itamtaka mtu huyo kulipa faini na kulipa riba kutokana na kuchelewa kulipa muda ulioopangwa kisheria.

Alisema kifungu hicho kinahusiana na makosa na adhabu, fidia kwa madhara, au fidia itakanayo makosa yanayohusu mtu mwingine pamoja na mamlaka na utaratibu na Mkurugenzi Mkuu kufifilisha makosa chini ya sheria.

Alitaja makosa mbalimbali yanayoweza kufanywa na viongozi wa bodi na mtu binafsi na kutakiwa kulipa faini na kifungo kwa mujibu wa sheria hiyo ni kuwazuia maofisa kufanya ukaguzi, kukataa kutotoa habari zinazohusu ukaguzi, kuchezea takwimu zinazotakiwa kutolewa na kushindwa kutekeleza maagizo ya amri iliyotolewa kutoa habari hizo.

Pia kuchezea sampuli zinazotakiwa na maofisa au kushindwa kufika mahali anapotakiwa na uongozi, kuingiza na kusaifisha nje ya nje mimea, mazao, viatilifu na mazao mengine yanayoendana na hayo.

Kutungwa kwa sheria hiyo kunaunganisha sheria mbili ya Hifadhi ya Mimea na Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki (TPRI) ili kuondoa upungufu katika mfumo wa sasa wa kisheria na muingiliano baina ya sheria hizo zinazopendekezwa kufutwa.

Hivyo sheria hiyo itaimirisha na kusaidia kuimarisha mfumo utakaosaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo za uingizwaji na usambazaji wa viuatilifu bandia. Pia inapendekeza masharti kuhusu udhibiti wa viautilifu, usimamizi wa afya ya mimea, udhibiti wa kuziia au kuingia na kuenea kwa visumbufu vya mimea na mazao.
Ama kweli!
Siku ya kufa nyani miti yote hucheka!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom