Bunge lasema halijapokea barua ya Nyalandu kujiuzulu, lamvua ubunge kutokana na CCM kumfukuza uanachama

Bunge lasema halijapokea barua ya Nyalandu kujiuzulu, lamvua ubunge kutokana na CCM kumfukuza uanachama

Sasa hapa chama kimechemka, kinaanza kuwaharibia vijana wao waliokwisha shika kasi katika kumkandika tope bwana Nyalandu.

Mbona kama Chama kina shock juu ya hili? Sioni haja ya kuendelea kutumia nguvu kubwa namna hii kwa mtu tuliyeambiwa na msemaji bwana polepole kuwa ni "mwanachama wa kawaida tu"
 
Kinachowauma CCM ni wao kupokea madiwani wa CHADEMA kwa 2M,huku CHADEMA wakimpokea mbunge wa CCM buuure!

Unaonga housegelo wa jirani kwa laki moja,huku jirani yako "akimjua" mkeo buure!

Inauma sana!
Ha ha haaa
 
View attachment 621949 Moja ya habari kubwa za sasa hivi nchini Tanzania ni Lazaro Nyalandu ambae juzi ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Ubunge wa Singida Kaskazini.

Baadae Spika Ndugai alihojiwa na vyombo vya habari na kusema kwamba pamoja na kusikia taarifa za kujiuzulu kwa Nyalandu kwenye vyombo vya habari, yeye bado hajapokea barua ya kujiuzulu kwa Mbunge huyo.

Sasa leo imetoka taarifa kutoka Ofisi ya Bunge Dodoma ikiwa imeandikwa kama inavyosomeka hapo juu..
Hata mimi ambaye sijasoma nilijua kujiuzulu kwake ni bora kuliko kubaki huko ila nilisema kilicho nyuma ya pazia anajua yeye nyalandu lakini asituambie ni mzalendo ndo maana anajiuzulu hilo si kweli.
 
Hiyo your take hiyo ndiyo umevuruga mambo kabisa;

Hata hivyo;

Amebipu wenzake wamempigia; sasa historia itasomeka kuwa CCM ndio imemmwaga Nyalandu kutokana na makando kando yake na sio yeye kukiacha chama.
Kiukweli kwa taarifa hiyo ya bunge umaarufu wa Nyalandu umeongezeka. Binafsi nilimsikiliza kwa makini Polepole alipohojiwa na Albert Kilala pale Channel ten alitamka wazi kwamba " Nyalandu ametumia haki yake ya kikatiba kuondoka CCM".......sasa haya ya kufukuzana yanatoka wapi tena?!!
 
Too low. Michezo mingine haina maana ni kujidhalilisha
 
Kiukweli kwa taarifa hiyo ya bunge umaarufu wa Nyalandu umeongezeka. Binafsi nilimsikiliza kwa makini Polepole alipohojiwa na Albert Kilala pale Channel ten alitamka wazi kwamba " Nyalandu ametumia haki yake ya kikatiba kuondoka CCM".......sasa haya ya kufukuzana yanatoka wapi tena?!!
Ajabu kweli hii mkuu, kama hayo ya kutaka kumfukuza yangekuwepo yangesemwa siku ile..

Aliyebuni hiki kituko mwenyekiti inabidi amtandike bakora!
 
Sasa kama kweli wao ndio wamemfukuza, Ndugai alikuwa anatokwa povu la nini?
 
Kiukweli kwa taarifa hiyo ya bunge umaarufu wa Nyalandu umeongezeka. Binafsi nilimsikiliza kwa makini Polepole alipohojiwa na Albert Kilala pale Channel ten alitamka wazi kwamba " Nyalandu ametumia haki yake ya kikatiba kuondoka CCM".......sasa haya ya kufukuzana yanatoka wapi tena?!!
Sawa kabisa Yohana Mbatizaji, kuna mengine huwa natofautiana na wewe , lakini hili uko sahihi kabisa. Watu akiwemo Nyalandu mwenyewe, wanaposema Bunge nalo limeingiliwa ni pamoja na kushiriki kucheza sanaa hii inayoongozwa na spika. Baada ya Nyalandu kutangaza kuachana na CCM, kuna kituo cha redio haraka haraka kilimpigia simu kumuuliza kama amepata barua ya Nyalandu, majibu aliyoyatoa yanaweza kutoa picha kamili. Wenye clip ya hayo mahojiano wanaweza kutuwekea hapa!
 
Polepole juzi hapa amesema ni haki ya mtu kujiunga na chama chochote cha siasa, kwa nini hakusema huyu alishafukuzwa?
 
1. Je,ni kweli ulikuwa ukidhibitiwa na kushughulikiwa kinidhamu ndani ya CCM kabla ya kujiuzulu na kuhama CCM?

2. Je,uliwahi kuarifiwa au hata kusikia kuwa umefukuzwa uanachama wa CCM kabla ya kutangaza kujiuzulu nafasi zote na kuhama CCM?

3. Barua yako kwa Spika uliyoiandika juzi uliituma Ofisi ya Spika kwa njia ipi na ilipokelewa lini huko? Una ushahidi gani?

4. Nini hasa kimekusukuma hadi kuachia nyadhifa zako na kuhama CCM?

5. Kisiasa,kuna tofauti gani na madhara gani kati ya kufukuzwa CCM na wewe kuhama katika kupoteza Ubunge wako?

6. Mchango gani utakaoutoa CHADEMA ambao uliutoa au haukuutoa ulipokuwa CCM?
 
Ama kwa hakika ukistaajabu ya Mussa utaona ya filauni, wale mliotoa mimacho kumshupalia Lipumba mmeyasikia ya Nyalandu kwamba alishafukuzwa huku CCM kitambo?!...... Lindi kuchele ngoma inogile!
 
3. CCM imesema Okt. 30 walimuandikia Spika barua kuwa, Nyalandu amepoteza sifa za uanachama wake na kwamba wamemvua nafasi zote za uongozi.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mbona polepole hakusema siku ile kuwa wamemfukuza? Spika ndo msemaji wa ccm sasa hivi? Nchi ina raha hii....[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Siku moja tulipanda ndege lakini nilimuona mzungu mmoja akiwa na mashaka sana hadi tulipotua japo hakukuwa na tatizo lolote. Waliojaribu kumdadisi ilikuwa ni kwa nini wakagundua eti kwa vile rubani alikuwa Mwafrika.

Iliniuma lakini nilivyotafakari nikagundua kuwa Waafrika wengi wenye uwezo wa kuionyesha dunia uwezo wao hawapati nafasi na tunabakia na wachache wanaoonekana 'front' huku wakiendelea kutuaibisha.
 
Back
Top Bottom