Bunge lasema halijapokea barua ya Nyalandu kujiuzulu, lamvua ubunge kutokana na CCM kumfukuza uanachama

Bunge lasema halijapokea barua ya Nyalandu kujiuzulu, lamvua ubunge kutokana na CCM kumfukuza uanachama

Ukiona maharage yanatokota na kurukaruka ujuwe moto umekolea
 
Ukitaka kujua wamekurupuka, kama wakukurupuka wa Star TV ni kuwa:- wamesema, ofisi ya spika haijapokea barua, kutoka kwa aliekuwa mbunge wa singida kaskizini. Sasa nauliza, kwanini wamesema aliekuwa mbunge? Ebu waungwana isomeni vizuri hiyo barua ili muelewe!! Aliekuwa, wametengua lini mpaka waseme aliekuwa? Ilitakiwa waandike kuwa, ofisi ya spika haijapokea bado barua ya mbunge wa singida kaskazini!! Hapo jee?
 
Watanzania wa leo si wale wa Nyerere msitulishe matango pori nyalandu kajiuzuru kwa anachokiamini katika siasa sio ccm wamemwandikia barua ya kumfukuza mmechelewa na propaganda zenu

Yaani mambo mengine ni aibu.
 
Ccm, kosa la beki kurudisha mpira kwa golikipa limewagarimu. Nyalandu kaupitia mpira kabla haujamfikia kipa akaweka wavuni.
 
Mungu turehemu ina maana hiki chama kinaishi katika laana mbona mambo yake si ya akili za kawaida??
 
Aaah jamani msitufanyie hivi ccm, hivi mnazani watanzania ni mazwazwa kiasi hiko. Embu acheni kujidharaulisha bana.
 
Hahahaha hawa naona Albadir imewachanganya Akili, hata hivyo siamini kabisa kama hii barua imetoka kwenye mamlaka ya bunge
Tuache utani ingekuwa ni mtu mmoja anatenda haya tungesema ana laana,lakini kwa sasa hiki chama kinaishi katika laana.Yatupasa tuamini tu huku tukijililia sisi na watoto wetu
 
Hapa hata mtu asiye na akili atakwambia huu ni utoto..

Nimekumbuka kipindi unamtamkia mchumba wako kwamba umemuacha, analalamika,analia halafu baada ya siku mbili kuisha anakutumia ujumbe mfupi anakutaarifu hata yeye pia alishafikiria kukuacha muda mrefu sana!

Kwa lugha nyepesi hiki ni kichekesho tena cha kuvunja mbavu!

Hongera Lazaro Nyalandu, umewashika sawasawa!
Tuongezee;

Polepole anamshangaa Nyalandu kuondoka CCM inayofuata itikadi ya Ujamaa purely na kujiunga chama kisicho na itikadi
 
Back
Top Bottom